Baadhi ya mabalozi wa Usakama barabarani Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani ,Latra,Sumatra na wadau wengine wakiwa katika siku ya mabalozi wa Usalama barabarani Mkoani TangaShabani Mrai Hiki Kamishna wa Polisi kamisheni ya  Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga katika siku ya madhimishio ya mabalozi wa usalama barabaraniShaban Mrai Hiki Kamisna wa polisi wa kamisheni ya Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai,akirudishia alama za barabarani zilizofutika katika eneo la Ekenforde(Mkwakwani)mkoani Tanga Mwenyekiti wa Taasisi ya Mbalozi wa usalama barabarani Taifa  RSA John Seka akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga katika maadhimisho ya siku ya mabalozi wa usalama barabarani Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Nchini Wilbroad Mutafungwa ( SACP)akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kurudishia alama za barabarani katika eneo Ekenforde(Mkwakwani)mkoani TangaKamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Nchini Wilbroad Mutafungwa ( SACP)akirudishia alama za barabarani zilizofutika katika eneo la Ekenforde(Mkwakwani mkoani) Tanga


Na.Vero Ignatus.Tanga.

Mabalozi wa usalama barabarani,kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani, kwa pamoja wameendesha  zoezi la kurudisha alama za barabarani zilizofutika ,katika eneo la barabara ya Ekenford ambapo dhima kuu ikiwa ''Usimamizi wa pamoja wa sheria za barabarani fursa na changamoto zilizopo''

Akizungumza baada ya zoezi hilo Kamishna wa polisi Shabani Mray Hiki , Kamisheni ya uchunguzi wa Sayansi ya Jinai, amesema kuwa ajali nyingi huwa zinasababisaha vifo majeruhi na ulemavu wa kudumu ambapo kundi kubwa linaloathirika zaidi ni watembea kwa miguu na vijana

Amesema katika kuhakikisha usalama barabarani Jeshi la polisi katika kutimiza wajibu wake, linatambua umuhimu wa wadau katika ushitikishwaji wa wadau, katika kuendesha mapambano ya kutokomeza ajali  za barabarani, pamoja na kuthamini michango ya wadau, wanaoshirikiana na Jeshi hilo katika kutokomeza ajali ikiwemo (RSA)

Amepongeza jitihada zinazofanywa na mabalozi wa usalama barabarani katika kuhakikisha kuwa wanapaza sauti kwa kuelimisha,kukemea na kuripoti pale ambapo uvunjifu wa seria za usalama barabarani zinapotokea katika sehemu mbalimbali nchini.

Akizungumza mwenyekiti wa RSA Tanzania ndugu John Seka,amesema Tanzania kama nchi imejiwekea malengo kwamba itakapofika mwaka 2030, ajali za barabarani zinapungua na kufikia chini ya asilimia 50% ya ajali zinazotokea kwa sasa,ambapo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali na wadau  na taasisi binafsi bado wanalengo la kuona lengo hilo linatimia

Amesema lengo hilo liliwekwa ili litimie mwaka 2020, lakini kwa mujibu wa takwimu na tafiti mabalimmbali zinazoendelea, kwa mujibu wa sheria malengo ya kupunguza ajali 2020 kwasababu mwaka unakwenda kutimia,ambapo kidunia inatambua kwamba hata ikifika 2020 mwishoni lengo la kupunguza ajali kwa asilimia 50% litakuwa halijafikiwa, kupitia malengo ya milenia ambapo umoja wa mataifa uliamua kuongeza miaka mingine 10 

Amesema katika malengo ya kidunia kila nchi sasa itakapofika mwaka 2030 ,nchi zote ziwe zimepunguza ajali kwa 50% ,Kwa mujibu wa Shirika la afya duniani ajali zinazotokana na masuala ya barabarani duniani zinaua watu zaidi ya mil.1.3 ambapo zaidi ya hayo inaacha majeruhi zaidi tya mil.40-70 kila mwaka ,hivyo wanaposema kupunguza ajali kwa 50% inamaana kwamba ile idadi ya ajali kimataifa ipingue iwe nusu yake ambapo siyo jambo dogo kutokana na changamoto zilizopo 

''Tunapiosema ajali zinapungua hapohapo magari yanaongezeka shughuli za kibinadamu zinaongezeka,watu wengi sasa wanahamia mijini,vyombo vya usafiri navyo vimebadilika tofauti na ilivyokuwa awali ambapo pikipiki pamoja na baiskeli katika nchi za kiafrika vikiendelea kuwa cvyombo vya usafiri na waenda kwa miguu wakiongezeka pia''Alisema Seka. 

Seka amesema RSA imedhamiria kupunguza ajali kwa 50%, lakini bado wanaona kuwa kuna visababishi vya ongezeko la ajali,ambapo katika lengo hilo Jeshi la polisi ,serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na wadau wake kusimamia zoezi hili na kuhakikisha kwamba usalama baranaraniunaimarishwa 

Aidha kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO) ,iliweza kutambulisha vyanzo vikuu 5 vya ajali barabarani ikiwemo ;mwendokasi,kutokuvaa mikanda ya usalama  wawapo kwenye vyombo vya moto,matumizi ya vilevi,utumiaji wa kofia ngumu kwa waendesha bodaboda na baiskeli,kutokuwa na vizuizi vya watoto kwenye magari,ambapo vyanzo hivyo vikidhibitiwa ajali za barabarani zitapungua 

Wakati huohuo Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani nchini Tanzania Wilbrioad Mutafungwa alisema Jeshi la polisi litaendelea kushirikiana na mabalozi hao katika kuhakikisha kuwa suala la Usalama barabarani linapewa kipaumbele kuhakikisha jamii inakuwa salama bila kuwa na ajali zinazoweza kuepukika 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa sheria wizara ya mambo ya ndani ambapo pia ni mjumbe wa bodi ya (RSA) Marlin Komba, akiwasilisha mada ya ushawishi wa mabadiliko ya tabia sheria na sera za usalama ,alisema jukumu la  RSA ni kushughulika na usalama barabarani katika nyanja zote ikiwemo abiria,madereva wamiliki wa vyombo katika maeneo matatu ya kukemea kuelimisha na kutoa taarifa.

Amesema inaonekana kuwa lipo suala zima la tabia ambayo ni mazowea ambayo yanamadhara katika usalama barabarani ,ambapo sheria mpya itakapokuja haitaondoa suala la usalama barabarani wala kuondoa utaratibu sahihi zilizopo,hivyo wale ambao hawafuati utaratibu uliopo sasa hata mabadiliko ya sheria ya usalama barabarani ukikamilika wasipojirekebisha sasa mabadiliko yajayo pia watashindwa kwenda nayo sambamba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...