Na Woinde Shizza Michuzi Tv-Arusha
Waziri
wa habari michezo utamaduni na sanaa Innocent Bashungwa anatarajiwa
kufunga bonanza la Arusha cup huku watani wa jadi Simba na yanga
wakisakata kabumbu katika bonanza hilo.
Hayo
yalisemwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi wakati akiongea
na waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya bonanza hilo tangu
lilipoanza januari 31,2021 na fainali kufanyika februari 27,2021 ambapo
alisema kuwa katika michezo 24 iliyochezwa katika uwanja huo kila
michezo umeingiza timu mbili fainali na watakao ibuka kidedea
watakabidhiwa zawadu mbalimbali.
Alisema
waziri Bashungwa ameshathibitisha uwepo wake na siku ya fainali
wataanza na Mazoezi ya Arusha Jogging club na baada ya hapo michezo
mbalimbali itaendelea na baadae mtanange kati ya Simba na Yanga hivyo
wananchi wahudhurie kwa wingi kwani michezo ni afya.
Aidha
alisema kuwa serikali kupitia fainali za bonanza la super cup na kwa
kushirikishirikiana na wadau mbalimbali wataanzisha benki ya damu
mkoani Arusha pamoja ba kuendesha zoeozi la uchangiaji wa damu.
“Benki
ya damu inayotegemewa na mkoa wa Arusha ni benki ya kanda nzima ambayo
ipo Mkoani kilimanjaro lakini kupitia bonanza hili kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali tuataanzisha benki ya damu hapa ili kuisaidia serikali
kupitia wizara ya afya kuokoa maisha ya wagongwa wanaohitaji kuongezewa
damu katika hosipitali zetu,” alisema Kenan.
Alisema
bonanza hilo linalojumuhisha michezo mbalimbali ambapo zawadi ya
ng’ombe, mbuzi, medani ,vyeti pamoja na hati za pongezi kwa wale vijana
na wananchi waliojitolea ujenzi wa madarasa kwa kutambua mchango wao wa
kujitolea nguvu kazi na kuhakikisha wanaleta maendeleo katika jiji la
Arusha
Alifafanua kuwa
lengo la bonanza hilo ni kukuza vipaji na michezo pamoja ndani ya Jiji
la Arusha pamoja na kuwaleta wana Arusha pamoja hasa katika sekta ya
michezo ambapo wanatarajia Arusha iwe sehemu ya kuvumbua vipaji vyote.
Kwa
upande wake Afisa Michezo wa halmashauri ya jiji la Arusha,Benson
Maneno alisema bonanza hilo limefichua vipaji mbalimbali ikiwepo uongozi
wa mpira ambapo hadi sasa Arusha hawana chama cha soka hivyo ni vyema
wakawatumia hao kama viongozi.
“Pamoja
kuvumbua vipaji kwa bonanza hili kwa kila mchezo fainali zimeingia
timu mbilimbili ikiwa maandalizi ya mashindano haya yalianzia katika
ngazi ya vitongoji na tarafa hivyo wananchi wajitokeze kushuhudia na
kushiriki pamoja ili kuleta mdhikamano,”alisema Afisa michezo huyo.
Hata
hivyo bonanza hilo linaendelea katika viwanja vya sheikh Amri Abeid na
ni bure huku wajasiriamali wa sekta mbalimbali wakiruhusiwa kwenda
kufanya biashara katika fainali za bonanza hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...