Meneja uvumbuzi wa kampuni ya Bia ya Sarengeti Bertha Vedastus (kulia) akipongezana na meneja mauzo wa kampuni hiyo mkoani Arsha Doreen Temba (kushoto) muda mfupi baada ya uzinduzi wa bia mpya ya Guinness smooth uliofanyika jana jijini Arusha.

Baadhi ya wageni ambao ni wauzaji na wasambazaji wa bia wakiingia katika hoteli ya Maunt Meru jijini Arusha kwa ajili ya uzindiuzi wa bia mpya ya Guinness smooth inayotengenezwa na kampuni ya bia ya Serengeti. Uzinduzi huo ulifanyika jana.

Wageni mbali mbali walioalikwa kwenye uzinduzi wa bia mpya ya Guinness smooth jijini Arusha wakisakata rhumba muda mfupi baada ya bia hiyo inayotengenezwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti Kuzinduliwa  rasmi kanda ya kaskazini

 

===== = ====== ======== =======

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imeendelea kupanua wigo wa bidhaa zake sokoni baada ya kuzindua bia mpya aina ya Guinness Smooth katika mikoa ya Moshi, Arusha Manyara na Tanga.


Katika uzinduzi wa bia hiyo mpya, wateja wa kampuni ya SBL, wauzaji wake wa bia pamoja na wenye mabaa walipata nafasi ya kuonja na kufurahia ladha ya kipekee ya bia ya Guinness smooth 


Akiongea wakati wa uzinduzi huo jijini Arusha, Meneja Uvumbuzi wa SBL Bertha Vedastus alisema “Bia hii mpya kwenye familia ya Guinness ina ladha ya kipekee ambayo inamfanya kila mnywaji afurahie kila mara anapoitumia na wakati akiwa na marafiki,” alisema


Bertha aliongeza “Ikiwa imetengenezwa kwa kumjali mnywaji wa Kitanzania, bia hii ina hadhi ya kimataifa na imetengenezwa katika kiwanda chetu cha moshi huku ikitumia malighafi za Kitanzania ikiwa ni Pamoja na shayiri inayolimwa katika mikoa ya Moshi, Arusha na mingineyo,”  


Meneja uvumbuzi huyo aliongeza kuwa familia ya Guinnness Tanzania inayo furaha kuwaletea bia hiyo wakazi wa mikoa ya Kaskazini ambao siku zote wamekuwa waaminifu kwa bidhaa za SBL na kuongeza kuwa bia ya Guinness smooth itakuwa ikipatikana kwa shilingi 1,500 tu.


“Guinness inahistoria ndefu na kongwe ya kutengeneza bia bidhaa ambazo zimefanikiwa kuteka soko la dunia na kuendelea kuwa kinara. Bia hii ni muendelezo wa Guinness kuwaleta wateja wake bidhaa ambazo zinakidhi mahitaji yao na kuenda na wakati,” alisema


Baadhi ya wateja waliohudhuria uzinduzi na kuonja bia hiyo mpya  walielezea kuvutiwa na ladha ya kipekee ya bia hiyo mpya na kusema kuwa watakuwa mabalozi wazuri.


“Bia ni nzuri na huu ni ujumbe kuwa ika kila sababu ya kufanya vizuri sokoni. Kwangu mimi kama msambazi wa bia naona ni fursa ambayo nitaitumia vyema kwa ajili ya kuweza kuongeza wigo wa wateja wangu Pamoja na kukuza biashara yangu pia,” aliongeza


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...