·         Vyombo vya habari kuacha kuripoti Uzushi

 Na Immaculate Makilika- MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Watendaji wa Serikali kutoa taarifa za utendaji wa Serikali katika maeneo yao, sambamba na vyombo vya habari kutoandika habari zisizo za ukweli.

Rais Magufuli, ameyasema hayo leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua ofisi za kituo cha televisheni cha “Channel Ten” zilizopo katika jengo la “Jitegemee” na kuweka jiwe la msingi katika soko la Kisutu.

“Watendaji wa Serikali wawe wepesi kutoa taarifa sahihi kwa waandishi wa habari, utakuta yamefanyika mambo mazuri  lakini hayatolewe na wananchi hawayafahamu, tusiogope kukosolewa, lakini vyombo vya habari toeni taarifa za ukweli bila kuweka chumvi, zingatieni ukweli.” Alisema Rais Magufuli

Aliongeza kuwa licha ya Wizara na Taasisi za Serikali kuwa  Wasemaji  katika ofisi hizo bado kumekuwepo na changamoto ya utoaji taarifa kwa waandishi wa habari, na hivyo amewataka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abasi kufuatilia suala hilo.

Rais Magufuli alisema kuwa watanzania wanatakiwa kuwa wazalendo  licha ya Tanzania kuwa mojawapo wa nchi zenye vyombo vingi vya habari duniani ambapo mwaka 2015 kulikuwa na vituo 106 vya redio vilivyosajiliwa, vituo vya televisheni 25, ambapo Februari 2021, kumekuwepo na vituo vya redio vilivyosajiliwa 195 na vituo vya televisheni 46. Pamoja na redio za mtandaoni 23 na televisheni za mtandaoni 440 na magazeti na majarida 247 vimesajiliwa hadi kufikia Februari 2021.

“Vyombo vya habari mnajitahidi kutoa habari, lakini mtangulize sana uzalendo na hakikwa yule anayeandikiwa habari, kumekuwepo na uzushi sana mara fulani kafa ni mambo ya ajabu” alisema Rais Magufuli

Alisisitiza “Lakini pia katika habari ambazo taifa letu linaandikwa vibaya watu wanashabikia, uzalendo umepungua tutangulize uzalendo wa nchi yetu, niwaombe watanzania wetu tutangulize maslahi ya taifa, wajenga nchi ni sisi na wabomoa nchi ni sisi.”

Rais wa. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika studio mpya za Magic FM baada ya kuzindua rasmi jengo la Jitegemee House pamoja na Studio za Channel Ten Plu,Radio Magic FM na Radio Classic FM Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo Alhamisi Februari 25, 2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...