Ofisi ya Jumuiya ya watumia maji kijiji cha Likuyusekamaganga ambayo itatumika kwa ajili ya uendeshaji wa mradi wa maji wa Likuyusekamaganga  utakaowanufaisha wananchi wa kijiji hicho na kijiji cha Mandela wilayani Namtumbo mradi uliotekelezwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa,

****************************************

Na Muhidin Amri,Namtumbo

WAKALA wa maji na usafi wa mazingira (Ruwasa) katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, umeokoa  kiasi cha shilingi milioni  560,000.000 kati ya  shilingi  bilioni 4,915,864.910 zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Likuyusekamaganga wilayani humo.

Kuokolewa kwa  kiasi hicho cha fedha, kumetokana na uamuzi wa  wizara ya  maji  kujenga mradi huo kwa kuwatumia mafundi wadogo chini ya usimamizi wa wakala wa maji na usafi wa mazingira(Ruwasa) kwa mfumo wa force  akaunti ambapo gharama za ujenzi zimepungua hadi kufikia  shilingi  bilioni 3,578,363.191.

Awali mradi wa maji Likuyusekamaganga ulisainiwa na kuanza kujengwa mwaka 2017 na ulitakiwa kukamilika mwaka 2020  na mkandarasi kampuni ya Elgance Developers Co Ltd kwa gharama ya shilingi bilioni 4,915,864.910.

Hata hivyo, wizara ya maji  ilivunja mkataba  mwishoni mwa mwaka uliopita kufuatia mkandarasi kushindwa  kukamilisha kwa muda uliopangwa na kukabidhi  mradi huo  kwa Ruwasa  kwa ajili  ya utekelezaji wake.

Meneja wa Ruwasa wilaya ya Namtumbo Mhandisi David Mkondya alisema, kupungua kwa gharama za wa mradi ni baada ya  Ruwasa kuanza kujenga kwa  kwa  utaratibu huo ambapo  umekamilika kwa asilimia 90 na  hadi sasa fedha zilizotumika ni bilioni 2,745,992.944.

Alisema, mradi  unalenga kutawanufaisha zaidi ya wakazi  13,320  kutoka vijiji viwili vya Likuyusekamaganga na Mandela.

Alisema tangu Ruwasa ikabidhiwe mradi, kazi zilizofanyika  ni ujenzi wa chanzo,nyumba ya mlinzi,ofisi ya  jumuiya ya watumia maji,ujenzi wa bomba kuu kutoka chanzo hadi kwenye matenki, na ujenzi wa bomba la usambazaji ambao bado unaendelea.

Alitaja kazi  nyingine  zilizokamilika  ni ujenzi wa matenki mawili,vituo 53 vya kuchotea maji,pampu ya kuvuta maji na mfumo wa umeme jua umenunuliwa na kufungwa.

Aidha, alisema  kazi ambazo bado zinaendelea ni kumalizia ujenzi wa ofisi ya jumuiya ya watumia maji,kumalizia jengo la muhudumu wa pampu,uunganishaji wa mtambo wa usambazaji maji katika vijiji husika.

Alisema, changamoto kubwa katika Utekelezaji wa mradi huo mzabuni kuchelewa kuleta bomba za kukamilisha mradi kwa awamu,lakini Ruwasa inaendelea kufuatilia kwa mzabuni kuleta bomba zilizobaki.

Kwa upande wao  baadhi ya wakazi wa kijiji cha Likuyusekamaganga, wameelezea furaha yao kwa Serikali ya awamu ya tano kwa kujenga mradi huo wa maji ambao unakwenda kumaliza changamoto ya muda mrefu  ya huduma ya maji.

Abdala Haule alisema, amefurahishwa na mkazo mkubwa uliowekwa katika ujenzi wa mradi huo hasa kutokana na ukweli kwamba  mradi ulianza kujengwa zaidi ya miaka mitano iliyopita na  bado haujakamilika.

Sihaba Baigwa alisema, msukumo uliofanywa na Ruwasa katika kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji Likuyusekamaganga ni ishara kwamba Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kumaliza kero zilizokuwepo kwa muda mrefu kwa kuboresha  huduma za kijamii na maisha ya wananc

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...