Salamu za Waziri Mhe. Innocent Bashungwa wakati wa Ziara ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Jijini Dar
es Salam.
Ziara hiyo iliyofanyika Februari 25, 2021 Jijini Da es
Salaam ilikua na lengo la kuzindua Jengo la Jitegemee House lenye
Studio za Channel Ten, Channel Ten Plus, Redio Magic FM na Classic FM
pamoja na Soko la Kisutu.
Katika ziara hiyo Waziri Mhe. Bashungwa
amekishukuru Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwekeza katika tasnia ya
Habari ambayo ni sekta inayosaidia wananchi kupata habari za ukweli na
uhakika kuhusu utekelezaji wa Serikali kwa wananchi wake.
"Nitumie
fursa hii kukaribisha Chama cha Mapinduzi kwenye tasnia ya michezo na
Sanaa kama mlivyowekeza kwenye tasnia ya habari, ipo pia fursa kubwa ya
kuwekeza kwenye michezo kwani tuna viwanja vya michezo vingi sehemu
mbalimbali hapa nchini, wawekezaji wagonge hodi kwenye Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo. Ikiwezekana tutumie 'PPP-Public Private
Patnership' (Ubia kati ya Serikali na Mashirika Binafsi) kuwekeza kwenye
viwanja ili visaidie kwenye soka na sanaa kwa ujumla," alisema Mhe.
Bashungwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...