Meneja Vifaa Vya Intaneti wa Tigo Mkumbo Myonga Akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) mara baada ya uzinduzi wa  uzindua simu janja aina ya  Infinix Hot 10 play ambazo zitakua zikipatikana nchi nzima.Kulia kwake ni Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa.


Dar es Salaam Februari 19, 2021, Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidijitali, Tigo Tanzania, leo imeshirikiana na Infinix kwaajili ya kuzindua simu janja aina ya  Infinix Hot 10 play ambazo zitakua zikipatikana nchi nzima.

Mkumbo Myonga, Meneja Vifaa Vya Intaneti wa Tigo alisema:  “Mkakati wa makubaliano baina ya Tigo na Infinix, yanalenga kuendeleza bidhaa hiyo ambapo kwa sasa katika soko la Tanzania kuna mahitaji makubwa ya huduma ya  teknolojia ya 4G kwenye simu.

"Tumetambulisha Infinix Hot 10 play kwa ajili ya kuwaaminisha wateja wetu wote nchini kutumia mtandao wa 4G".

Myonga pia aliongeza katika uzinduzi huo wa  Infinix Hot 10 play, utasaidia kuongeza thamani sokoni kwa wafanyabiashara  kutokana na ubora wa bidhaa hiyo kwa Watanzania wote.

 “Mbali na kuwaletea wateja wetu bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na bei rahisi, Infinix Hot 10 play ni sehemu ya mikakati ya kuendelea kuleta bidhaa nzuri zaidi nchini kwa ajili ya magaeuzi ya kidijitali nchini,".

Kwa mujibu wa Myonga “Simu hizo kwa sasa zinapatikana katika maduka yote ya Tigo nchi nzima na simu itakuwa ofa ya bando ya GB 78, kwa mwaka mzima.“

Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa, alisema: “Infinix Hot Play ina kadi maalumu ya Helio G35 Chip ambayo ina michezo mbalimbali kwa ajili ya mtumiaji.

"Uwezo wake wa betri ni 6000 mAh ambayo inakaa saa 24 na utacheza game muda wote, Infinix hot 10 play ina uwezo wa 6.82 kutazama sinema na kupiga picha kamera ina  uwezo wake ni 13MP, inatumia taa ya flashi, Hot 10 play inapatikana katika maduka yote ya Infinix na  maduka ya Tigo nchi nzima”


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...