Na Rahma Khamis \Issa Mzee Maelezo Zanzibar

Waandishi wa habari Nchini wametakiwa kutoa habari zinazohusu uvunjifu wa haki za binaadamu ili kuwasaidia wananchi kufikisha malalamiko yao sehemu husika ili kukuza ustawi wa jamii nchini.

Akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari katika warsha iliyoandaliwa na Mkufunzi kutoka Shirika la Waandishi wa Habari wa Haki za Binaadamu Sami Awami katika Hoteli ya Golden Tulip iliopo Kibweni amesema ipo haja kwa waandishi wa habari kupata mafunzo hayo ili kusaidia katika upatikananji wa haki za binadamu nchini.

Akiwasilisha mada ya haki za bindamu na corona asmesema kuibuka kwa maradhi ya Corona duniani kumesababisha kutokea kwa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu kwa baadhi ya raia wa mataifa mbalimbali jambo ambalo limeleta athari kubwa kwa watu wengi hasa wananwake na watoto.

Akitoa mfano wa vitendo uvunjaji wa haki za binaadamu ambavo vimejitokeza baada ya karantini iliyowekwa kwa baadhi ya mataifa amesema ubakaji kwa wanawake na watoto,kupigwa pamoja na unyang’anyi ni miongoni mwa vitendo vinavyofanyika nchi nyingi Duniani.

Amesema kuwa kutokana na muanguko wa kiuchumi uliosababishwa na corona umepelekea kutokea kwa vitendo hivyo na kuwataka waandishi wa habari kuzipa kipaombele habari zinazohusu haki za binadamu ili kutomeza janga hilo Duniani.

Aidha amefahamisha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika na janga hilo na kupelekea kuzorota kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na kusababisha baadhi ya wanawake na watoto kuvunjiwa haki zao za msingi na kudhalilishwa.

Alifafanua kuwa kutokana na kutojua haki na sheria ya haki za binadamu ya Tanzania na uwepo wa baadhi ya viongozi wanaokiuka sheria ni miongoni mwa sababu zinazopelekea vitendo vya uvunjivu wa haki za binadamu ikiwemo udhalilishaji.

Pia amefahamisha kuwa ni wajibu wa kila mtu Duniani kote kupata haki za msingi za binaadamu na kuwataka wandishi wa habari kuisaidia jamii katika kufahamu haki zao za msingi ili kuondokana na vitendo vya uvunjifu wa haki hizo.

Nao washiriki katika mafunzo hayo wameeleza kuwa wanawake ndio waathirika wakubwa wa vitendo vya uvunjifu wa haki za binaadamu kwani hufanyiwa vitendo mbalimbali ikiwemo kubakwa hivyo lazima waripoti habari hizo ili kusaidia katika kuviondoa uvunjifu huo Nchini.

Wamefahamisha kuwa katika kipindi cha mwanzo cha maradhi ya Corona jamii ilikuwa ina hofu sana dhidi ya janga hilo kutokana na ugeni wa maradhi hayo pamoja na athari zake na kupeleka watuhumiwa wengi wa maradhi hayo kunyanyapaliwa jambo ambalo ni uvunjivu wa haki za binadamu.

Wakizungumzia kuhusu haki ya mwananchi washirriki hao wamesema kuwa jamii bado haijui haki na wajibu wa kujikinga na kujilinda kutokana na maradhi hayo hivyo ipo haja kwa Serikali kutoa elimu khusu haki za binadamu.Aidha wamefahamisha kuwa katika kupambana janga hilo hakuna kubudi kwa vyombo vya habari na jamii kwa ujumla kutoa elimu zaidi na kuandaa vipindi vinavyohusu haki za binadamu na corona ili wananchi wapate haki zao licha ya kukumbwa na janga la hili.


Mwandishi wa Habari wa Zbc Redio Hinja Haji pongwa wapili kulia akitoa mchango wake katika Semina ya Mafunzo kuhusiana na Haki za Binaadamu na COV 19 Iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya GOLDEN TULIP Kibweni jijini Zanzibar.

Mwandishi wa Habari wa Star Tv Abdalla Pandu kulia akitoa mchango wake katika Semina ya Mafunzo kuhusiana na Haki za Binaadamu na COV 19 Iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya GOLDEN TULIP Kibweni jijini Zanzibar.
Mkufunzi wa Mafunzo ya Haki za binaadamu ambae ni mwandishi wa Habari wa Al jazira Sami Awami akitoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Haki za Binaadamu na COV 19 Iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya GOLDEN TULIP Kibweni jijini Zanzibar.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...