…………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu Mihambwe 

Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amewaonya viongozi wa Serikali za vijiji, vitongoji na Watumishi kutojihusisha na matendo ya rushwa kwa kuzingatia uadilifu na maadili ya kazi katika kuwahudumia Wananchi. 

Hayo yamebainishwa kwenye mafunzo ya siku moja ambayo yalilenga kuwakumbusha kuzingatia sheria, taratibu na kanuni katika kuzuia na kupambana na rushwa. 

“Kila mmoja ana jukumu kuu la kuzuia na kupambana na rushwa wakati wa kuwatumikia Wananchi. Pia kuwa na nidhamu na uadilifu katika miradi ya ujenzi ya kimaendeleo.” alisisitiza Gavana Shilatu ambaye alifungua na kufunga mafunzo hayo. 

Gavana Shilatu alihaidi mafunzo hayo yatakuwa endelevu ili kuhakikisha Watumishi na viongozi wengi wa halmashauri ya Serikali za vijiji na vitongoji wanafikiwa. 

Nae mtoa mafunzo hayo Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya Bw. Wilson Festo aliwataka viongozi hao kushirikiana vyema katika kuzuia na kupambana na matendo ya rushwa. 

Mmojawapo wa washiriki wa mafunzo hayo Ndugu Mussa S. Mtondo ambaye ni Mwenyekiti Kijiji cha Namunda kilichopo kata ya Kitama ameshukuru kutolewa kwa mafunzo hayo ambayo yamewajengea uwezo kufahamu miongozo na taratibu zote za kisheria. 

“Tunashukuru sana kupatiwa mafunzo haya ambayo yametujengea ufahamu na uweledi zaidi katika kujua miongozo na taratibu zote za kisheria katika kuzuia na kupambana na Rushwa. Tunaomba mafunzo haya yawe endelevu.” Alisema Ndugu Mtondo. 

Mafunzo hayo ya siku moja ambayo yalifanyika ofisi ya Mtendaji kata Kitama yaliandaliwa na ofisi ya Tarafa ya Mihambwe na mada kutolewa na Maofisa toka ofisi ya TAKUKURU wilaya yakihusisha Wenyeviti wa vijiji, Wenyeviti wa vitongoji, Watendaji kata, Watendaji vijiji na Afisa Maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...