Meneja wa  anayesimamia miradi ya elimu katika Manispaa ya ubungo  kutoka shirika la Ocode  Digna Mushi wa kushoto akipeana mkono na Mkuu wa shule ya msingi Kibwegere Charles Kulemo  iliyopo kata ya Kibamba ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa miundombinu ya ngazi maalumu hazipo pichanai ambazo zitatumika katika kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu hususan walemavu wa viungo kuweza kupita kwa urahisi pindi wanapokwenda madarasani.

Mkuu wa Shule ya msingi Kibwegere Charles Kulemo kushoto akitoa maelekezo kwa baadhi ya viongozi wa Shirika la Ocode ambao walifika shuleni hapo kwa ajili ya kuweza kukabidhi miundonbinu ya ya ngazi ambazo waliamua kuzijengwa kwa wajili ya kuweza kuwasaidia wanafunzi ambao ni walemamvu wa viungo.

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Kibwegewe wakiwa wanaimba huku wamepiga daruti wakati wa halfa hiyo amabyo iliandaliwa na Shirika la Ocode kwa ajili ya kukabidhi minundimbinu hiyo ya majengo  ya ngazi kwa ajili ya wanafunzi ambao ni walemavu wa viuongo mbali mbali.

Mkuu wa shule ya msingi Kibwegere  Charles  Kulemo akiwa anazungumza na baadhi ya wazazi na walezi pamoja na walimu wa shule hiyo ambao walishiriki katika halfa hiyo.

Baadhi ya wazazi, walezi pamoja na walimu ambao walihudhulia katika halfa hiyo wakiwa wanashuhudia halfa hiyo ya makabidhiano ya miundombin ya ngazi zilizojengwa kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi  wenye mahitaji maalumu.

Mwenyekiti wa miradi ya elimu kutoka Manispaa ya Ubungo  ambayo inasimamiwa na Shirika la Ocode Hamza Mirambo akiwa anafafanua jambo namna na shirika hilo amabyo linawasaidia wanafunzi  na shule mbali mbali za msingi ili kuweza kuborersha sekta ya elimu.(PICHA ZOTE ZA VICTOR MASANGU)

…………………………………………………………………………………….

NA VICTOR MASANGU, KIBAMBA

KATIKA kukunga mkono juhudi za serikali ya wamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu na kuwathamini wanafunzi wenye mahitaji maalumu hususan walemavu Shirika  lisilokuwa la kiserikali la (OCODE ) limekuja na mpango kabambe ambapo limeweza kuwasaidia baaadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Kibwegere iliyopo kata ya Kibamba kwa kuwapatia vifaa mbali mbali pamoja na kuwajengea miundombinu rafiki ya majengo ili kuwarahisishia katika kutembea.

Akizungumza katika halfa fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kuweza kukabidhi baadhi ya miundombinu ambayo imejengwa kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalumu  Meneja wa  anayesimamia miradi ya elimu katika Manispaa ya ubungo  kutoka shirika la Ocode  Digna Mushi amebainisha kwamba utekelezaji wa mradi huo wa kutoa vifaa pamoja na kwuajengea ngazi utakuwa ni mkombozi kwa wanafunzi hao.

“Sisi Kama Shirika la Ocode tumekuwa tukifanya kazi ya mambo ya elimu katika manispaa hii ya Ubungo la lengo letu kubwa ni kuhakikisha watoto wetu wanaweza kusoma katika mazingira rafiki, na leo hi tupo katika shule hii ya msingi Kibwegere tumekuja kwa ajili ya kukabidhi miundombinu ya ngazi ambazo zitawez kutumika kwa wanafunzi mbali mbali amabo ni walemavu wa viungo tofauti kama vile vya mikono pamoja na miguu sambamba pia kuwapatia vifaa vitakavyoweza kuwasaidia,”alisema Digna.

Naye  Mkuu wa shule ya msingi Kibwegere amesema  kwamba Charles Kulemo amesema kwamba wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule hiyo wapo 15 na kwamba msaada huo wa walioupata kutoka Ocode wa kuwajengea miundombini rafiki ya ngazi itawasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kuweza kutembea kwa urahisi zaidi kwenda madarasani.

Mkuu huyo alibainisha kwamba shirika la Ocode limeweza kuwa mstari wa mbele katika  kusaidia kwa hali n amali katika kuboresha sekta ya elimu na kwamba msaada huo wa wa kuwajengea miundombinu ya ngazi kwa wanafunzi wa shule hiyo kutaweza kuwasaidia kwa kiais kikubwa wanafunzi ambao walikuwa wanapata shida ya kupandaili kuelekea madarasani.

“Katika shule yetu ya msingi ya Kibwegere kwa sasa tuna wanafunzi 15 ambao wana  mahitaji maalumu na kati yao walunana wapo tisa na wasicha wapo 6 hivyo kwa msaada huu wa shirika la Ocode la kujenga miundombinu ya ngazi ni jambo ambalo litaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wanafunzi wetu kuweza kupita kwa urahisi kwani hapo awali walikuwa wanapata shida katika suala zima la kupita.

Mkuu huyo katika hatua nyingine alitoa pongeza kwa Shirika la Ocode kwa kuweza kutoa msaada wa mambo mbali mbali katika shule hiyo ikiwemo kuwajengea madarasa, kuwapatia viti na meza kwa ajili ya walimu na wanafunzi lengo ikiwa ni kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri na rafiki ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingiara ambayo ni rafiki.

Kwa upande wake mmoja wa wakikilishi wa walezi wa watoto hao wenye mahitaji maalumu amebainisha kwamba mjukuu wake anayetambulika kwa jina la Mustafa Sefu mwenye umri wa miaka 10 alikuwa anakabiliwa na changamoto ya viungo vya mikono na miguu lakini kwa sasa anaweza kutembea kutoaka na msaada wa vifaa ambao amepatiwa.

Hamza Miramboi ni Mwenyekiti wa miradi wa elimu katika manispaa ya Ubungo alisema kuwa lengo lao ni kuhakikisha kwamba wnaunga juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu na kwamba kwa sasa wanaendelea kutoa misaada mbali mbali katika baadhi ya shule za msingi zilizopo Manispaa ya ubungo ikiwemo kuwapa wanafunzi umuhimu wa elimu jumuishi na kuwashirikika wazazi na walezi.

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Ocode limekuwa likiunga mkono juhudi za serikali kwa kipindi kirefu katika kuboresha sekta ya elimu hasa katika shule mbali mbali zilizopo katika Manispaa ya Ubiungo kwa kutoa vifaa mbali mbali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu  ikiwemo madawati, viti, kujenga madarasa pamoja na kutoa elimu jumuishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...