Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali( CAG)Charles Kichere amesema mashirika 11 ya umma hayajakuliwa kutokana na kushindwa kuwasilisha taarifa za mahesabu yao kwa kuhofia huenda yakikaguliwa yatapata hati mbaya.

Akizungumza leo Aprili 8,2021 ,Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali( CAG) kichere amesema ameshindwa kutoa maoni kwa mashirika ya umma 11 kwani hakufanikiwa kukagua hesabu zake ili kutoa naoni.

" Kuna mashirika ya umma 11 hatukumaliza kuyagau kwani walishindwa kuwasilisha taarifa za mahesabu yao na wale ambao waliwasilisha walileta nje ya muda wa ukaguzi na hata tulipokagua tulibaini kuna makosa wakafanye marekebisho lakini hawakuleta tena,"amesema.

Ameyataja mashirika hayo ni Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kampuni ya Mbolea Tanzania, Mfumo wa Taifa wa Bima ya Afya, Mfuko wa UTT, Kampuni ya Magazeti ya Serikali, Shirika la Posta Tanzania, Shirika la Reli Tanzania, Kampuni ya Simu Tanzania, Shirika la Umeme Tanzania( TANESCO) Soko la Bidhaa Tanzania na Taasisi ya Mifupa  Muhimbili.

Hivyo ametoa mwito kwa Menejimenti,Bodi ya Wakurugenzi na Maofisa Masuhuli wa mashirika hayo kuhakikisha wanatimiza matakwa ya kikatiba na kisheria kuwasilisha hesabu kila mwaka kwa ajili ya kutolewa maoni ya ukaguzi.

Pia wanatakiwa kufanya mawasilisho ya hesabu ili kukaguliwa na kufikiaa kiwango cha kimataifa." Aidha wawasilishe taarifa ndani ya wakati ili tuweze kutoa maoni badala ya kuogopa kwa kutowasilisha taarifa zao kuhofia kupata hati wasizozipenda.Ni muhimu kufanyiwa ukaguzi wa mahesabu."

Wakati huo huo amesema ametoa hati mbaya kwa Halmashauri ya Shinyanga,Halmashauri ya Singida, Halmashauri ya Itigi, Halmashauri ya Igunga,Halmashauri ya Sikonge, Wilaya ya Urambo, Wilaya ya Momba, Manispaa ya Tabora, Tume ya Unesco pamoja na Hospitali ya Rufaa Morogoro .Pia amesema ametoa hati zenye mashaka kwa taasisi kwa taasisi 81.

"Katika Serikali Kuu wanajitahidi maana vitabu vyao wa mahesabu wanachukua katika mfumo ambao unaeleka lakini kwa Serikali za Mitaa vitabu vyao vya hesabu vina shida sana kwani hesabu zao ziko nje ya mfumo.

"Nitoe mwito kwa Serikali kutoa mafunzo kwa wanaohusika na kuandaa vitabu vya hesabu katika halmashauri na Wilaya ili waweze kuandaa vitabu kwa kiwango cha kimataifa kutokana na mfumo ambao tunautumia katika ukaguzi.Wanaandaa figa ili kubalansisha tu hesabu ,ukiwaambia waandike tena wanaharibu kabisa,"amesema Kichere.

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali( CAG)Charles Kichere 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...