Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

MAMLAKA  ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)  imebaini uwepo wa dawa bandia ya mifugo aina ya Alben Blue 2.5% toleo Na.019394 lililotengezwa  Nov 2019 na lenye tarehe ya mwisho wa matumizi October 2022.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Mkurugenzi Mkuu  wa TMDA, Adam Fimbo imesema  mamlaka hiyo kupitia mifumo yake ya ukaguzi  na ufuatiliaji wa bidhaa katika soko iliweza kufatilia na kugundua uwepo wa dawa hiyo bandia.

Taarifa hiyo mesema dawa hiyo katika lebo biashara inaonesha inatengenezwa na kiwanda cha Nerix Pharma kwa niaba ya Vetagro and Pulper Co.Ltd Nairobi nchini Kenya.

Aidha taarifa Mkurugenzi Mkuu ilisema kuwa  katika kufanya uchunguzi wa kimaabara ambapo matokeo ya uchunguzi yameonesha kuwa toleo hilo halina kiambata hai.

“Wote waliokutwa na toleo dawa hiyo  wamefunguliwa mashitaka katika vituo mbalimbali vya polisi na upelelezi unaendelea ili kuweza kuutambua mtandao mzima unaojihusisha na utengenezaji dawa ,usambazaji na uuzaji wa toleo hilo bandia la dawa hii,”Imesema taarifa  

Hata hivyo amesema kutokana na kubainika dawa hiyo,wafugaji wote nchini wanaotumia dawa hiyo kwaajili ya kuua minyoo wanaelekezwa kuangalia kwa makini lebo za dawa hiyo na endapo wataona namba za toleo husika watoe taarifa katika Ofisi zao.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...