Na John Walter-Babati

Mashirika ya NGOs yameishukuru serikali kwa ushirikiano ambao wanaendelea kuuonyesha kwao kwa kuwa inawatia moyo kuendelea kuomba miradi Zaidi kutoka kwa wafadhili ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii.

Wakizungumza mara baada ya mkutano wao na mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange viongozi wa mashirika hayo wameaahidi kufanya kazi kwa kufuata misingi na taratibu za serikali ikiwa ni njia ya kuiunga mkono serikali katika shughuli za kuwaletea mendeleo wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema amekuatana na mashirika hayo ili Kujua wanafanya kazi kwenye maeneo gani,wanakumbana na changamoto gani,bajeti ambazo wamezitenga kufanya kazi kwenyemiradi yao na ikiwezekana kujua wafadhili wao wanatoka wapi kwa kuwa ili kazi zao zifanyike kwa ufasaha lazima uwajibikaji wa wananchi na serikali.

Aidha ameahidi kushirikiana na NGOs katika shughuli mbalimbali ili kuwahudumia wananchi kwa pamoja huku akiwathibitishia viongozi wa (NGOs) kuwa serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na Asasi hizo nchini.

Ameongeza kuwa amekukutana (NGOs) hizo kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi pamoja kuweka muelekeo mzuri katika jitihada za kuhakikisha yanasaidiana na Serikali kuwaletea maendeleo wananchi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Mashirika hayo yaliwasilisha taarifa za kazi wanazozifanya na changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuomba serikali iwasaidie kuzitatua.

NGOs zilizokutana na mkuu wa wilaya ni SHAMBANI SOLUTION,CSP,THRIVE AFYA,TANZANIA,MAHOCE,COSITA,RESTLESS,ZILPER FOUNDATION,WORLD VISION,MCDO,FIDE na CHEMCHEM ASSOCIATION.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...