Kumekuwepo na taarifa za upotoshaji zinazo sambazwa katika mitandao ya kijamii kuhusu uwasilishaji wa ritani za raia wa kigeni wanaofanya kazi hapa nchini. 

Taarifa sahihi ni kwamba, ritani hizo zinapaswa kuwasilishwa kwa Kamishna wa Kazi, Dodoma kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwenye kifungu cha 16 cha Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni, Sura 436. Kwa mujibu wa utaratibu huo, waajiri wenye wafanyakazi ambao ni raia wa kigeni wanapaswa kuwasilisha ritani za wafanyakazi hao kila tarehe 30 Juni na 31 Disemba ya kila mwaka. Aidha, pale ambapo ajira ya raia wa kigeni husika imemalizika kabla ya muda wa kuwasilisha ritani, mwajiri anapaswa kutoa taarifa mapema kwa Kamishna wa Kazi kuhusu suala hilo.

Vilevile, Sheria ya Fedha ya Mwaka 2021 imerekebisha kifungu cha 16 cha Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni kwa kuongeza kifungu kidogo cha 3 ambacho kimeweka faini ya Shilingi Laki Tano  itakayotozwa kwa mtu yeyote kila mwezi au sehemu ya mwezi atakayochelewa kuwasilisha ritani.

Kwa taarifa hii, wateja wetu wanaombwa kuzipuuza taarifa za upotoshaji zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii. Aidha, wote wanaosambaza taarifa za upotoshaji wanatakiwa kuacha kufanya hivyo mara moja na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi wale watakaidi maelekezo haya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...