Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. ABUBAKAR KUNENGE amesema wataalamu wa Kilimo na Mifugo watapimwa kwa mikakati ya kuongeza uzalishaji.

RC Kunenge ametoa rai hiyo Julai 14, 2021  wakati akizungumza na Wataalamu wa Kilimo na Mifugo wa Ofisi yake kikao  kilichoshirikisha Maafisa kutoka Benki ya Kilimo, Bodi ya Korosho na Kituo cha Utafiti TARI Nailiendele.

Kunenge ameeleza kutoridhishwa kwa hali ya uzalishaji wa mazao ya Kilimo na Mifugo, amewataka Wataalamu hao kuandaa Mikakati ya namna ya kusimamia mazao ya kilimo na mifugo ili kukuza uzalishaji. Amewataka Uongozi wote Mkoani hapo kusimamia Mikakati hiyo kila mmoja kwenye eneo lake.

"Nataka tujue tuko wapi na tunataka nini kwenye kilimo ili tusimamie  na kutekeleza Mikakati ya kukuza uzalishaji na kupiga hatua. Ametaka Mikakati hiyo ipimike na atawapima Wataalamu hao kupitia utekelezaji wa  Mikakati hiyo. Lazima tupimane alisisitiza Kunenge.

Amewataka wahusika wote kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo na mifugo kutekeleza na kusimamia Mikakati ya kukuza mazao. Ameeleza kuwa Wajibu  Wananchi kwenye Kilimo cha Korosho kwa muda huu ni kusafisha mashamba, "wasafishe mashamba yao".







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...