Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JESHI
la polisi linamshikilia Antony Lugendo (34) mkulima,mkazi wa Mlandizi
kwa kosa la kumdhalilisha mtoto mdogo wa kike miaka mitatu kwa kumchezea
chezea sehemu za siri.
Aidha limekamata watuhumiwa 38 wa makosa mbalimbali na mali za wananchi zimeokolewa,ikiwemo TV,Radio,sabufa, pikipiki na laptop.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio Hilo,kamanda wa polisi mkoani Pwani ,Wankyo Nyigesa
,alisema tukio limetokea juzi saa 10 jioni ,huko Kitongoji Cha Kaloleni
kata ya Janga .
Alieleza
,mtuhumiwa alikamatwa akiwa chumbani kwake amemvua nguo zote na akiwa
anamchezea mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa chekechea .
"Mtuhumiwa tumemkamata na upelelezi unaendelea ili hatua za kisheria zichukuliwe"alisema Wankyo.
Katika
hatua nyingine, Wankyo alieleza kwa kipindi cha wiki mbili kuanzia
septemba 3 hadi 17 septemba limefanya operesheni katika wilaya zake tano
madhumuni kuzuia , kudhibiti uhalifu .
Katika
operesheni hii walifanikiwa kukamata bunduki 1 aina ya shortgun yenye
namba GP 719 na risasi moja ,bangi kwenye beg ,puli 39 ,kete 661 na
miche 24,radio 2 aina ya sony na sabufa moja na spika 6 kati ya hizo
aina ya boss 02 na aina ya sony nne.
Wankyo
alifafanua ,pia laptop moja ,mafuta ya dizel lota 230 ,petrol lita 500
,pikipiki moja aina ya boxer yenye namba za usajili MC 226 CMT rangi
nyeusi na televisheni tano aina ya Good vision ,sony , Samsung,LG na TCL
moja.
"Vitu
vingine ni desktop moja aina ya dell na CPU mbili ,gari aina ya canter
moja ,matairi mawili ya gari , camera mbili aina ya Samsung moja ,camera
monitor,mkasi wa kukatia chuma ,funguo master key na pombe ya moshi
lita 65.
Wankyo alikemea kwa jamii kuacha tabia ya unyanyasaji kwa watoto kwani kwa kufanya hivyo kuwaharibu kisaikolojia
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...