Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV


MCHEZAJI wa zamani wa Klabu ya Simba Emmauel Anold Okwi ameibukia katika  Simba Day na kuibua shangwe kwa mashabiki na wapenzi wa Simba waliojitokea maelfu kwa maelfu Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Slaam.

Okwi ambaye alijiunga na Simba mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 18 ameichezea klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi kwa mafanikio makubwa hasa kutokana na uwezo wake wa kusakata kabumbu uwanjani. Aliondoka Simba 2019 lakini hadi leo amebaki kuwa kipenzi cha wana Simba.

Hivyo tangu alipoondoka hajawahi kuonekana katika Uwanja wa Mkapa na mbele ya Wana Simba hadi leo Septemba 19,2021  ambako ameibuka na kuanza kuzunguka uwanjani  akisalimia mashabiki.

Okwi aliingia uwanjani saa 8:15 mchana ambapo alianza kusalimia wana Simba kuanzia upande wa kulia  na kisha kuelekea upande wa kushoto wa Uwanja wa Mkapa na wakati anasalimia alivaa jezi ya Simba .Muda wote wakati anapita uwanjani alikuwa akisalimia kwa kunyosha mikono juu .

Wakati wote huo mashabiki wa Simba waliamua kumuonesha heshima ya upendo kwa kusimama muda wote huku wakimshangilia.

Mbali ya Okwi kusalimia mashabiki wa Simba,aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Mzee Hassan Dalali alipata nafasi ya kupita uwanjani akisalimia mashabiki.Mzee Dalila alizunguka uwanja mzima huku akionesha kutopita na wakati kwani kuna nyakati alikuwa akisakata Singeli kiasi cha kufanya Wana Simba kumshalingilia.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...