BODI ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB,) imeandaa Semina ya 23 'Research Workshop'  na kutoa mafunzo maalumu ya kuwandaa  wanafunzi wa Bodi wanaotarajiwa kufanya tafiti kabla ya kuhitimu mafunzo kutoka bodi hiyo yaliyoanza leo Sepitemba 27 hadi Oktoba 01, 2021.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Godfrey Mbanyi amesema kuwa moja ya matakwa ya CPSP ni kufanya 'Research Paper' na mwanzo wake ni huo kwa wanafunzi kuhudhuria semina na kupata mafunzo yatakayowapitisha kwa usahihi katika safari yao ya kufanya tafiti na kuhitimu vyema mafunzo hayo kwa mujibu wa bodi hiyo.

Mbanyi amesema, katika mafunzo hayo wanafunzi watapitishwa katika maeneo tofautitofauti ya mbinu za utafiti na andiko la utafiti pamoja na kuwajengea uwezo wa kuandika tafiti na ripoti mbalimbali kwa kufuata kanuni na miongozo ya PSPTB katika tafiti zao watafazozifanya.

Aidha amesema kupitia mafunzo hayo wanafunzi wataelekezwa na kujengewa uwezo wa jinsi ya kuandaa andiko la utafiti  hususani ya PSPTB ili waweze kuhitimu mafunzo hayo na kuwataka wanafunzi hao kuzingatia umuhimu wa mafunzo hayo muhimu katika tafiti zao watakazozianza mara baada ya mafunzo hayo.

''Baada ya kuhitimu mafunzo haya ya siku tano wahitimu mtapewa vyeti vya kuonesha ushiriki wenu katika mafunzo haya na kuanza kuandika research proposal/ mapendekezo ya tafiti zenu mapema iwezekanavyo.'' Amesema.

Mafunzo hayo ya siku 5 yaliyoanza leo yamewakutanisha wanafunzi zaidi ya 100 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwemo Moshi, Mtwara, Mwanza na wenyeji Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza wakati wa kufungua semina ya 23 'Research Workshop' yenye lengo la kutoa mafunzo maalumu ya kuwandaa wanafunzi wa Bodi wanaotarajiwa kufanya tafiti kabla ya kuhitimu mafunzo kutoka bodi hiyo yanayofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini  Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wanafunzi wa Bodi wanaotarajiwa kufanya tafiti  wakifuatilia hotuba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), Godfred Mbanyi alipokuwa anafungua mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku tano katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB), Godfred Mbanyi akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Bodi wanaotarajiwa kufanya tafiti waliofika kwenye semina iliyoandaliwa na Bodi hiyo iliyofanyika leo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini  Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...