Na Amiri Kilagalila,Njombe
Halmashauri
ya mji wa Njombe imewaagiza watendaji na maafisa ugani katika ngazi za
kata kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuzingatia kanuni
za kilimo bora kisichoathiri mazingira kwa kuwa ndio msingi wa maisha ya
binadamu.
Agizo hilo
limetolewa na kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bwana Thadei Luoga
wakati akifungua kikao kazi cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi
ya awamu ya pili iliyotekelezwa na shirika la Highland Hope Umbrella
kwa ufadhili wa The Foundation for Civil Society kwenye kilimo katika
kata tano za halmashauri hiyo,hatua iliyoambatana upokeaji wa mradi
awamu ya tatu.
“Tuzingatie,tuhakikishe
tunawaelimisha wananchi wetu kuzingatia kanuni za kilimo bora na
kisichoathiri mazingira kwasababu mazingira ndio mwarobaini wa kila kitu
kwasababu pamoja na jitihada za jamii za kupanda miti na kuhifadhi
mazingira zinatufanya Njombe tuendelee kuwa na hali ya hewa
inayotuwezesha kuzalisha mazao ya mboga mboga nay ale ya nafaka”alisema
Bwana Luoga
Bathseba
Barnaba Liduke ni mkurugenzi wa asasi hiyo,amesema wamekuwa wakifanya
miradi mbali mbali ikiwemo ya elimu,afya,watoto pamoja na kilimo ambapo
katika kilimo wamefanikiwa kutekeleza kwa awamu mbili na sasa wakielekea
awamu ya tatu katika tarafa ya Igominyi kwa lengo la kuelimisha jamii
kuelewa wajibu wao kwenye kilimo.
“Lengo
kubwa ni kuhamasisha jamii iweze kuelewa kama ina wajibu gani katika
kufuatilia maswala ya kilimo na kuangalia namna kilimo kinavyoendesha
katika halmashauri yao na sio kupiga kelele tu”alisema Liduke
Vile
vile Bi,Liduke amesema zaidi ya wakulima 300 katika kata tano lengwa za
halmashauri hiyo wameweza kunufaika na utekelezwaji wa mradi.
Kwa
upande wake afisa kilimo wa halmashauri hiyo alisema licha ya
halmashauri hiyo kuendelea kupambana na kuendeleza kilimo lakini
wanakumbwa na uhaba mkubwa wa maafisa ugani huku akishukuru shirika hilo
kwa msaada ambao wamekuwa wakiutoa katika maswala ya kilimo.
“Halamsahuri
yetu ya mji wa Njombe ina upungufu mkubwa sana wa wataalamu wa kilimo
ukilinganisha na idadi ya vijiji,halmashauri ina maafisa ugani 23 na
ukijumlisha vijiji na mitaa unapata 72 na kwa kweli changamoto hii ni
kubwa sana unaweza kukuta kuna wakati afisa mgani mmoja ana fanya kazi
katika kata zaidi ya mbili.Niombe serikali itufikirie kwasababu
halmashauri ya mji Njombe ni tofauti na halmashauri zingine kwa kuwa ina
mitaa 28 halafu ina vijiji 44”alisema afisa kilimo.
Aliongeza
kuwa “Taasisi hii ya HHU inajitahidi sana kushirikiana na halmashauri
na kufuatilia utendaji kazi wa maafisa ugani wao,wanasema maswala ya
uwajibikaji”alitoa pongezi afisa kilimo
Akizungumza
kwa niaba ya washiriki wa kikao kazi hicho,diwani wa kata ya Luponde
bwana Urlick Msemwa amesema taasisi hiyo imekuwa ikifanya kazi nzuri na
kuongeza uwajibikaji kwenye kilimo katika kata tano za mradi.
“Kufanya
kazi na sisi kumeongeza uazalishaji na uwajibikaji kwenye
kilimo,tunaendelea kuwaona kama wadau muhimu sana na tunaendelea
kuwaunga mkono wakati wowote ili kuwezesha kilimo kwenye halmashauri
yetu”alisema Urlick Msemwa
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Bwana Thadei Luoga akifungua kikao cha kupokea taarifa ya utekelezwaji wa mradi pamoja na kupongeza shughuli mbali mbali zilizofanywa na shirika la HHU mjini Njombe.
:Mmoja wa watumishi kutoka shirika la HHU akieleza namna mradi awamu ya pili ulivyotekelezwa na kutambulisha mradi awamu ya tatu utakavyotekelezwa katika halmashauri hiyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...