Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Thomas Mihayo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho ya utalii ya Afrika Mashariki yatakayofanyika mkoani Arusha, Septemba 9 hadi 16,2021.

Na Grace Gurisha

MWENYEKITI wa Bodi ya Utalii, Thomas Mihayo amesema ni wakati wa nzuri wa watanzania kujipanga vizuri ili kuonesha Tanzania ikoje na ina nini cha kujivunia katika onyesho la  kwanza la utalii la Afrika Mashariki litakalofanyika mkoani Arusha.

Mihayo amesema hayo leo Septemba 28,2021 wakati akizungumza na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari mkoani Dar Salaam kwa lengo la kuwapa historia ya onesho hilo na muelekeo wake.

Amesema muelekeo wake ni onesho la Afrika Mashariki, kwa hiyo wanatazamia wenzao wote watakuwepo secretalieti ya Afrika Mashariki ambayo inakaa Arusha watakuwepo na nchi mbali mbali zitakuwepo katika maonesho hayo.

"Tunataka Jumuiya ya  Afrika Mashariki waoneshe nini wanafanya na nini wanacho, watakuja Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na nchi zote za Afrika Mashariki kuonesha walichokuwa nacho katika tansinia ya biashara, utalii na fursa mbali mbali walizonazo katika nchi zao.''

"Sasa ni wakati wetu watanzania onesho lipo kwetu tujipange vizuri ili tuoneshe Tanzania tukoje na tuna nini cha kujivunia na si vibaya kujivunia kuzidi wenzetu, kwa sababu tunaweza tukawa na kitu kuwazidi wenzetu," amesema Mihayo.

Amesema jumla ya nchi 10 kutoka mataifa mbali mbali zinatarajiwa kushiriki maonesho ya utalii kwa nchi za Afrika Mashariki yatakayofanyika mkoani Arusha kuanzia Oktoba 9 hadi 16,2021 kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii.

Mwenyekiti hiyo, amesema siku tano nitakuwa za maonesho na siku zitakazofuata zitakuwa za ziara mbalimbali za mafunzo yaani ni safari ya kwenda kujifunza nini watanzania tunacho na kinapatikana kwa njia gani.

Mihayo amesema katika jitiada za kuvutia  utalii mawaziri wanaohusika na utalii wa Afrika Mashariki walikutana wakabuni wazo la kuwa na maonesho makubwa yanayosimamiwa na Afrika Mashariki.

"Mwanzo wazo hili walipanga kwamba liwe linafanyika mara moja katika miaka miwili, lakini wakaona hapana lifanyike kila mwaka na katika makubaliano ya kuwa nani aanze kuandaa maonesho hayo walipendekeza wafuate alphabeti, ambapo Burundi wakapewa nafasi.

" Kutokana na muda kuwa mfupi wa maandalizi hayo Burundi hawataweza kuandaa shindano kubwa kama hilo, kwa hiyo kwa sababu Waziri wetu wa utalii alikuwepo  akasema wao wapo tayari basi tukaanza mchakato, Waziri akatuita akaunda kamati ya kitaifa na kamati kishirika tukaanza maandalizi,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...