Charles James, Michuzi TV

NAIBU Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa na utawala bora Deogratius Ndejembi ametoa maagizo kwa maafisa elimu mikoa ,wilaya na maafisa TAKUKURU, kuhakikisha wanatenga muda wa kuelimisha vijana na jamii kwa ujumla kuhusu madhara ya rushwa.

Ndejembi amebainisha hayo jijini Dodoma katika uzinduzi wa Mwongozo kwa wawezeshaji kufundisha vijana wa skauti kuzuia na kupambana na rushwa na madhara ya RUSHWA kwa Jamii.

Amesema kuwa  rushwa imekuwa ikikwamisha maendeleo ikiwemo huduma mbalimbali za kijamii ambazo ni Elimu,Maji,Afya na nyinginezo hivyo kupitia Elimu huyo Vijana watawwza kuachana na vitendo vya rushwa.

"Rushwa imekuwa ikiwanyima haki Watu na hivyo kufanya hata maendeleo kurudi nyuma hasa katika masuala ya usimamizi wa miradi ya maendeleo kama shule na mingineyo mingi kutokana na baadhi ya Watu kukosa uzalendo,"Amesema.

Aidha amesema wao kama Serikali wanaunga mkono juhudi za TAKUKURU  na skauti kutokana na ushirikiano huo wakutoa Elimu kuhusu mapambano dhidi ya rushwa kwani itasaifia kutokomeza suala hilo katika Jamii.
 
Awali  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa  TAKUKURU Neema Mwakalyelye amesema mwaka 2019 walisaini mkataba wa makubaliano na chama cha Skauti Tanzania katika mapambano dhini ya rushwa na malengo ya mashirikiano hayo ni kuelimisha jamii madhara ya rushwa katika jamii .

Amesema lengo ni kuhakikisha Vijana waliopo vyuoni na shule kusaidia kutoa taarifa dhidi ya vitendo vya rushwa katika chaguzi na maeneo mbalimbali.

"Kupitia mkakati wa utekelezaji wa mwongozo huo,wanatarajia kuongeza upana wa makundi ya mapambano dhidi ya rushwa nchini ambapo kuna takriban vijana 105 wamenufaika na mafunzo hayo",Amesema.

Kwa upande wake Skauti Mkuu Tanzania, Mwantumu Mahiza amesema mwongozo huo wa kufundishia masuala ya rushwa utakuwa na tija kubwa kwani vijana walio wengi hususan shuleni ndio waathirika wa rushwa kwa sababu rushwa huchelewesha maendeleo.

Aidha,amesema haiwezekani Tanzania tangu ipate uhuru mwaka 1961 bado inahangaika na miundombinu ya zahanati ,barabara kwani nchi zilizoendelea kuna masuala walishaacha na kujikita mambo mengine ya maendeleo.

Hata hivyo, ameiomba Serikali kuwatumia Skauti hasa pale inapowahitaji vijana maskauti ikiwemo Tasisi ziwaruhusu na kuwawezesha kwani wanafanya kazi kubwa kwa maendeleo ya taifa.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...