Na WAMJW
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Abel Makubi, amesema, Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa watapimwa utendaji kazi katika ukusanyaji wa mapato, uwajibikaji, uboreshaji wa huduma, ubunifu na kushughulikia malalamiko ya wagonjwa sambamba na wanavyotekeleza maagizo ngazi wanazo wajibika nazo.

Prof. Makubi ameyasema Sepetemba 23, 2021 katika kikao na Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa, alipokuwa akifungua Mkutano wa Waganga wakuu hao.

“Tutakuwa tunawapima jinsi gani mnavyoboresha huduma, inatakiwa mteja akifika anaona kwa jinsi gani huduma zimeboreka, suala linguine ni ukusanyaji wa mapato, ni vizuri kila mmoja wenu akafikia malengo, lakini Pamoja na hayo serikali ingependa kuona kwa namna gani mnashughulikia malalamiko ya wateja wenu, amesema Prof. Makubi.

Katibu Mkuu, Makubi amewataka viongozi hao wa Hospitali za Mikoa, kutekeleza, Maagizo yanayotolewa na ngazi za juu, ikiwepo utoaji wa taarifa, inashangaza, kuona ndani ya mwezi miongozo unayoletewa unaambiwa ulete ripoti huleti hili halikubaliki alisisitiza Katibu Mkuu.

Katika atua nyingine, Prof. Makubi amesema Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuendelea kuboresha huduma za tiba na kinga ikiwemo kupanua huduma za kibingwa katika Hospitali za Wilaya.

“Serikali awamu ya sita tumedhamiria kuboresha huduma za afya huduma hizo hazikuwepo, hususani kwenye Hospitali zetu za Wilaya, tunafahamu ujenzi wa vituo vya afya vingi vilijengwa, ikiwa ni mkakati wa kuboresha miundombinu, hivyo ni muhimu kuboresha huduma zetu ikiwepo huduma za kibingwa katika Hospitali za Wilaya ambazo nazo sasa zinajengwa kwa kasi” Amesema Prof. Makubi

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia magonjwa yasiyoyakuambukiza kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye alimwakilisha Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. James Kihologwe amewataka waganga hao kupeleka mipango mikakati yao Wizarani sambamba na kuangalia mazingira ya sasa ya ugonjwa wa Uviko 19 ambao kumeibuka baadhi ya wataalam wachache wakileta changamoto kadhaa hasa katika suala la maadili kwa wafanyakazi.

“Hivi karibuni yamejitokeza matukio mengi ya matukio ya watoa huduma kufanya mambo ambayo ni kinyume na maadili na miiko inayo ongoza taaluma ya afya, nanyi katika maeneo yenu ya kazi mna mabaraza ya wataalam hawa, hivyo hakikisheni yanafanya kazi yake vizuri huku mkiyasimamia ili kuhakikisha maadili ya watoa huduma yanaimarishwa,” amesema Dkt Kihologwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...