Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (watatu kushoto) akikabidhi mfano wa Hundi ya thamani ya shilingi bilioni 7.6 kama gawio kutoka benki ya CRDB kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), C.P.A. Hosea Kashimba (wanne kushoto) aliyeongozana na Mkurugenzi wa Fedha Beatrice Musa-Lupi (wapili kushoto) na Maafisa Uhusiano waandamizi wa Mfuko, Coleta Mnyamani (watano kushoto) na Fatma Elhady (Wasita kushoto) huku Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki ya CRDB, Ally Hussein Laay 9Wakwanza kulia) na wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajib Nsekela.

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba azipongez Taasisi za Umma kwa uwekezaji wa hisa kwenye benki.

Asema huo ndio utaratibu wa kuendesha uchumi kwa njia za kisasa.

NA MWANIDHI WETU

MFUKO wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umepokea gawio la zaidi ya shilingi bilioni 7.6 kutokana na uwekezaji wa hisa katika benki ya CRDB.

Hafla ya kukabidhi GAWIO kwa Serikali Kuu na Taasisi za Umma kutokana na faida ambayo benki ilipata mnamo mwaka 2020 ilifanyika Jumatatu Oktoka 25, 2021kwenye Makao Bakuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam  ambapo mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amezipongeza taasisi za Umma kwa uwekezaji huo ambao umeleta tija.

“Niwapongeze kwakweli wanahisa huu ndio utaratibu wa kuendesha uchumi kwa njia za kisasa, mnachokifanya kinaangukia kwenye sifa za uendeshaji wa uchumi wa kisasa.” Alisisitiza Waziri Nchemba.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma PSSSF, Beatrice Musa-Lupi alisema Mfuko unayo furaha kubwa kuona kwamba uwekezaji huo umeleta faida kwa wanachama.

“Uwekezaji huo unafanywa kwa kuzingatia sheria iliyoanzisha Mfuko ambayo inatoa wajibu wa kukusanya michango na wajibu wa kuwekeza ili kulinda thamani ya Michango ya Wanachama na kuleta uwajibikaji katika kulipa Mafao.” Alifafanua Lupi.

Alisema Mfuko unapofanya uwekezaji huangalia misingi ya uwekezaji kwa kuangalia mahala ambapo ni salama na CRDB ni moja ya maeneo salamaambapo hisa za Mfuko ziko salama na zinaleta faida mfano mwaka 2019 Mfuko ulipata gawio la shilingi bilioni 5.8 na mwaka 2020 gawio limeongezeka  na kufikia shilingi bilioni 7.6.

“Tunaamini CRDB itaendelea kufanya vizuri na faida itaendelea kupatikana na hivyo kuleta faida kwa wanahisa na wanachama wetu kwa ujumla.” Alisema.

Alisema Mfuko utaendelea kuwekeza, maeneo mengine ambayo ni salama na yanayoleta faida na kuchochea uchumi kwenye maeneo mbalimbali na taasisi hizo ziwe zinazofuata taratibu za nchi kama ulipaji wa kodi.

“Mfuko utaendelea kufuata vigezo vyote  na sheria inavyoelekeza kuhakikisha kuwa fedha tulizowekeza ziko salama, zinaleta faida lakini pia zinachangia katika ujenzi wa uchumi wa taifa letu.” Alisisitiza Lupi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba 
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), C.P.A. Hosea Kashimba (wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba (wakwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Fedha wa PSSSF, Beatrice Musa-Lupi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Raay.
Maafisa Uhusiano Waandamizi wa Mfuko huo, Coleta Mnyamani (wakwanza kushoto) na Fatma Elhady wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), C.P.A. Hosea Kashimba, akisalimiana na Maafisa Uhusiano Waandamizi wa Mfuko huo, Coleta Mnyamani (wakwanza kushoto) na Fatma Elhady
C.P.A Kashimba (wakwanza kushoto), akijumuika na wageni waalikwa wenzake kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Fedha PSSSF, Beatrice Musa-Lupi (kushoto) akiteta jambo na mmoja wa mameneja w aCRDB.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), C.P.A. Hosea Kashimba (aliyesimama) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba (wapili kulia) na Mkurugenzi Mtenfdaji wa Watumishi House Dkt. Fred Msemwa (wakwanza kushoto) na nyuma kidogo ni Mkurugenzi wa Fedha PSSSF, Beatrice Musa-Lupi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba  akihutubia wakati wa hafla hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...