MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini, imeendesha warsha ya siku moja kwa wanahabari kuhusu mwelekeo wa mvua za msimu kwa kipindi cha mwezi Novemba 2021 hadi Aprili 2022 nchini.

Akizungumza wakati akifungua warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi amesema katika kuhakikisha nchi inaendelea kufikia lengo la ukuaji wa uchumi wa viwanda, wameanza kuto utabiri mdogomdogo kwa wilaya 63 zilizopo katika ukanda unaopata mvua za msimu wa Novemba hadi Aprili kila mwaka utakwa ukuaji wa uchumi wa viwanda,

Warsha hii ni muendelezo wa juhudi za mamlaka kutaka kuhakikisha taarifa za Utabiri wa hali ya hewa zinawafikia walengwa kwa uhakika, usahihi na kwa wakati, amesema Dkt. Kijazi

Amesema mvua hizi za msimu ambazo ni mahususi kwa maeneo ya Magharibi, nyanda za juu Kusini Magharibi, Pwani ya Kaskazini na Kusini mwa nchi yetu ambayo hupata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.

Mvua hizi katika maeneo haya zina mchango mkubwa katika sekta mbali mbali ikiwemo za kilimo, nishati, maji na nyinginezo nyingi kwani miongoni mwa maeneo yanayopata mvua za msimu, kuna mikoa inayotegemewa katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kwa nchi huku na nyanzo vya maji na mabwawa ya kuzalisha umeme ikiwemo Bwawa la Mtera,

"Taarifa sahihi za hali ya hewa ni muhimu kupatikana kwa a wakati ili kuwezesha jamii na wadau kujipanga na kuandaa shughuli za kiuchumi na kijana katika maeneo yao.

Amesema, kupatikana kwa Utabiri kwa usahihi na kwa wakati nitachangia katika jitihada za serikali ya awamu ya sita katika kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, nchi kwa ujumla pamoja na kuboresha miundombinu na huduma za kijamii". Amesema dkt. Kijazi

Aidha amesema, kanuni za sheria namba 2,2019 iliyoanzisha mamlaka zimeishasainiwa kutendo ambacho kitaipa nguvu mamlaka kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu na hivyo kukidhi mahitaji ya huduma za hali ya hewa kwa jamii na hivyo kuchangia katika kufikia Maendeleo endelevu ya nchi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Mgeni Rasmi, Dkt. Buruhani Nyenzi akikabidhi zawadi kwa mwandishi bora wa habari za TMA leo mjini Kibaha. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akifafanua jambo kwa wanahabari wakati wa warsha ya siku moja kwa wanahabari wao kuelekea nm Utabiri wa msimu wa mvua wa Novemba 2021 hadi Aprili 2022. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa
Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa akifafanua jambo katika warsha hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...