Na.Khadija Seif, Michuzi TV

MSANII wa Bongofleva wa Miondoko ya Hip hop nchini Rashid Abdallah maarufu kwa jina la kisanii Chid Benz ameachia Albam yake mpya "Wa2 wangu" Huku akiwashukuru Mashabiki wake kumpokea vizuri kwenye ramani ya Muziki baada ya kupitia kwenye changamoti ya kiafya Kwa muda mrefu.

Akizungumza na Michuzi tv, Chid Benz mara baada ya kutambulisha Albam yake mpya " Wa2 wangu" ambapo ni Albam ya 3 tangu kuanza kwake Mziki iliyosheheni nyimbo takribani 18,amewashukuru Mashabiki kuendelea kumpokea vizuri tangu alipofikwa na Matatizo ambayo yalimsababishia  kupotea kwenye ramani ya Mziki huo.

"Kilichonisukuma kutoa Albam ni kuona Kwa jinsi gani Mashabiki wangu bado wapo na wanaendelea kutamani kusikia na kuona kazi zangu japo nilipotea kutokana na Matatizo niliyopitia Kwa muda mrefu hivyo nimetambulisha rasmi "Wa2 wangu" iliyosheheni wimbo 18 na baadhi ya Wasanii nimewashirikisha akiwemo Kijana anaefanya vizuri Baddest."

Hata hivyo Chid ametaja Miongoni mwa vitu vinavofanya Muziki wa Bongofleva kutopata nafasi ya kuonekana Kwa baadhi ya Wasanii ambao wanafanya vizuri nje ya nchi Huku akimtaja Msanii MB Dog kama Msanii ambae anamkubali na anatamani arudi kwenye ramani ya Muziki.

"Wasanii wetu wanajigawa kimakundi inapelekea kundi hilo kusaidiana wenyewe kwa wenyewe kutokana na uwezo ama mianya ya kujuana na watu mbalimbali nje na ndani hivyo unakuta kuna uwepesi wa Kazi zao kuwepo Mitandaoni pamoja kupenya katika vyombo husika vinavotoa nafasi ya kucheza Muziki yao .

Hata hivyo Chid amepata nafasi ya kuwaomba na kuwasihi Waandishi Wahabari pamoja na Wadau wa Muziki kuacha ubaguzi wa kusaidia wasanii katika kazi zao.

Msanii wa Muziki wa Hip hop Rashid Abdallah maarufu kama Chid Benz akizungumza na waandishi Wahabari mara baada ya kutambulisha rasmi Albam yake aliyoipa jina la "Wa2 wangu" yenye nyimbo takribani 18

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...