Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Sara Msafiri akizungumza na wadau wa Maziwa wakati alipofungua mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika kwa wafugaji wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani
Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Uthibiti Ubora TBS Baraka Mbajige, akizungumza na wadau wa Maziwa wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika kwa wafugaji wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani
Meneja Utafiti na Mafunzo Sudi Mwanansela, akizungumza na wadau wa Maziwa wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika kwa wafugaji wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.
Baadhi ya wadau sekta ya maziwa pia ni wajasiriamali wakisikiliza kwa makini


Na Khadija Kalili, Kibaha
KAIMU Mkuu wa Kitengo Cha Uthibiti Ubora wa Shirika la Viwango nchini (TBS) Baraka Mbajige amewaonya wafugaji na wauzaji wa maziwa kuacha tabia ya kuweka maji kwa sababu ni kinyume cha sheria.

Alisema hayo katika mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na TBS kwa wafugaji wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani kuwa adhabu ya mfugaji anayeweka maji kwenye maziwa ni faini ama kufungiwa.

Kwaupande wake  Meneja Utafiti wa Mafunzo Sudi Mwanansela alisema kuwa TBS wamefanya mafunzo hayo ikiwa na lengo la kuwapa elimu ya namna ya usindikaji, ubebaji Ili kuweza kuyapandisha thamani sokoni na kwa mlaji kwa ujumla.

"Tutakuwa na mafunzo kwa siku mbili. hapa Kibaha ambapo tutajifunza kwa kutoa elimu na pia tutakwenda kuwafundisha kwa vitendo ambapo tutakwenda kuwatembelea kwenye maeneo ya na kuona namna wanavyofuga na kung'amua changamoto wanazozipitia Ili tuone namna ya kuweza kuwasaidia kuzitatua" alisema Mwanansela.

Mafunzo hayo yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ambapo amewataka wafugaji hao kuondoka na maazimio ya kukua katika sekta hiyo ya maziwa na kuwataka wakati ujao waweze kuandaa Kongamano kubwa ambapo pia waweze kuwaita wadau wakubwa wakiwemo Idara ya Lishe ambao wataweza kujadili kwa kina suala.la udumavu na umuhimu wa unywaji maziwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...