Na.Khadija Seif, Michuzi TV.
WABUNIFU
Wa Kizanzibar wameahidi kutumia fursa ya jukwaa la Mavazi ya Kiasili
kusaidia Serikali ya Zanzibar kutangaza na kukuza pato la Taifa.
Akizungumza
na Michuzi, Mbunifu Mkongwe kutoka Visiwani Zanzibar ambae pia ni
Muasisi wa jukwaa la ubunifu (Zanzibar fashion island) Waiz Shelukindo
amesema Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi julai
mwaka huu likiwa na lengo la kutangaza utalii visiwani na Mavazi ya
Kiasili.
"Sanaa ya
Ubunifu wa Mavazi lazima ikue hivyo lazima kuwepo Kwa Matamasha ambayo
yanakumbusha na Kuonyesha vitu vipya hivyo tumeamua kutangaza utalii
kwenye jukwaa la ubunifu wa Mavazi linalotarajiwa kufanyika julai 29
Hadi 30 mwaka huu katika ukumbi wa front ocean Visiwani Zanzibar."
Aidha
ameeleza kuwa jukwaa hilo litakuwa la wazi Ili kuwapa fursa watu
kuhudhuria Kwa wingi na kuona Kwa jinsi gani Kuna baadhi ya Mavazi ya
Kiasili na kitamaduni hayapewi nafasi Kwa Sasa kutokana na utandawazi na
tamaduni za kizungu.
"Kuna
baadhi ya Mavazi mara nyingi yamekua hayaonekani lakini wabunifu
kutokana na kazi zao wamekuwa wakitengeneza hivyo jukwaa hilo litaweza
kuwapa fursa wabunifu kuonyesha Mavazi hayo."
Pia
Waiz amesema kupitia jukwaa hilo litashirikisha wabunifu wa ndani na
nje ya nchi ikiwemo Visiwa vya Comoro,Kenya, Uganda na nchi zingine
nyingi Visiwani Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...