Naibu waziri wa Fedha na Mipango Hamad Hassan Chande amewasihi wawekezaji hapa nchini kuendelea kutumia fursa za uwekezaji zilizopo ikiwemo za kibiashara na utalii sambamba na kutanua wigo wa biasahara zao ndani ya nchi, Afrika Mashariki pamoja na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika.

Mhe. Chande ametoa wito huo Jijini Dar es Salaam katika hafla maalum ya Umoja wa Maafisa Watendaji Wakuu wa Makampuni Binafsi nchini (CEOs roundtable) ikiwa na lengo la kujadili maendeleo ya sekta binafsi katika bara la Africa.

Ameeleza kuwa Sekta Binafsi ina mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa lolote na kwamba Serikali inatambua na kuthamini mchango wao katika nyanja mbalimbali ikiwemo uwekezaji.

Hata hivyo Mhe. Chande amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Sekta Binafsi ili kukuza sekta ya uchumi, kutatau tatizo la ajira na kuongeza ustawi wa maendeleo ya nchi.

Katika hatua nyngine Naibu waziri huyo amewataka wadau wa Sekta Binafsi nchini kutumia mifumo maalumu ya utoaji malalamiko na mapendekezo kwa Serikali juu ya sera na sheria za uwekezaji badala ya kutumia njia nyingine zisizo rasmi kutoa kero zao ikiwemo mitandao ya kijamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Watendaji wakuu (CEOrt) David Tarimo amesema sambamba na maboresho ya sheria za uwekezaji yanayofanywa na Serikali CEOrt itahakikisha uwekezaji unaendelea kufanyika kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...