Msanii wa Muziki wa RNB hapa nchini, Juma Mussa Mkambala maarufu kama Juma Jux akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo Februari 06, 2023.

MSANII wa Muziki wa RNB hapa nchini, Juma Mussa Mkambala maarufu kama Juma Jux ameeleza namna alivyopata fursa ya kutembelea Ufaransa katika mji mkuu wa Nchi hiyo Paris ambao huzalisha kinywaji aina Hennessy.

Amesema ziara hiyo ilimpatia fursa muhimu ya kupanua upeo wake na kupata maarifa mapya kuhusu ulimwengu wa bidhaa hiyo yenye maarufu dunia nzima.

Uzoefu aliyeoupata ameeleza unaweza kuwa na manufaa makubwa kwa wasanii Tanzania pia kuhamasisha mawazo mapya ya kibunifu na kuwasaidia kuinua sanaa na chapa zao.

"Nimefurahi kutembelea Paris na kujifunza juu ya chapa kubwa ya Hennessy. Uzoefu huu una uwezo wa kubadilisha maisha yangu kama msanii, na nina hamu ya kuleta mambo mapya kwa ajili ya jamii na maarifa niliyo shuhudia na kuona katika hii Ziara.” Ameeleza

Amesema Ratiba ya safari ya yake iliandaliwa kwa uangalifu ili kutoa nafasi ya kuongeza uzoefu na wa kina wa chapa ya Hennessy. Amesema Safari ilianzia Chateau Bagnolet, kiwanda cha kutengeneza kinywaji hicho, ambapo aliweza kuona mchakato wa uzalishaji wa Hennessy na kujifunza juu ya historia ya utengenezaji wa kinywaji hicho maarufu cha Hennessy.

"Mchakato wa utengenezaji wa Hennessy ni wa ajabu na wenye umaridadi sana kwani kwa kiasi kikubwa umejaa ubobezi wa ukweli, umakini na ufundi uliotumika unaoingia kwenye kila chupa ya kinywaji hichi ni cha ubora wa kustaajabisha. Nina shukuru kwa Kampuni inayozalisha kinjwaji hiki siwezi kusubiri kufananisha uzoefu nilioupata na Wasanii wengine wa nchi mbalimbali.” Amesema Jux

Pia Jux amesema kuwa waliweza kutembelea Viwanja vya mpira wa kikapu pamoja kutazama na kucheza mchezo wa huo na walifanya ziara ya kwenye uwanja wa Trevise Court, uwanja mkongwe zaidi wa mpira wa vikapu unaojulikana huko Paris.

"Mimi ni shabiki mkubwa wa mpira wa kikapu, na ilikuwa ndoto ambayo imetimia kutembelea uwanja mkongwe zaidi wa mpira wa kikapu huku Paris. Nguvu na msisimko wa mchezo huo ulikuwa dhahiri, na nilifurahishwa kuwa sehemu yao. Kuweza kuchanganya mapenzi yangu kwa mpira wa kikapu na upendo wangu kwa kinywaji cha Hennessy na hii imefanya safari hii kuwa ya pekee zaidi."

Ameeleza Kilele cha ziara hiyoilikuwa ni kutazama mechi ya kusisimua ya mpira wa kikapu kati ya Chicago Bulls na Detroit Pistons, ambapo Hennessy ni kinywaji rasmi cha NBA na huendelea kutoa zaidi ushirikiano katika mchezo huo.
"Sitasahau kamwe safari hii ya ajabu, Umaridadi na ustadi wa chapa ya Hennessy kwa kweli ulizidi matarajio yangu, na ninashukuru chapa hii kwa kufanikisha safari hii."

Kupitia ziara hiyo Jux ameeleza kuwa imemhamasisha kusaidia wasanii wengine hapa nchini na kuonesha uwezekano wa ukuaji unaotokana na kuchunguza uzoefu na tamaduni mpya

Amesema Hennessy inatarajia kuwasaidia wasanii wa ndani nchini Tanzania, kama sehemu ya dhamira yake inayoendelea ya kukuza na kusaidia sanaa mbalimbali hususani muziki. Ziara hii ni moja tu ya mipango mingi ambayo Hennessy ameifanya kusaidia wasanii kufikia uwezo wao kamili na kufikia ndoto zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...