Njombe

Hatimaye kilio cha miaka mingi cha kukosa nishati ya umeme kwa wakazi wa kijiji cha Mfereke kata ya Utalingolo halmashauri ya mji wa Njombe tangu kijiji hicho kilipoanza huku nguzo za umeme zikiwa zimepita kijijini hapo kuelekea maeneo mengine kimeanza kupungua baada ya serikali kufikisha umeme kwa mara ya kwanza huku wananchi wakiishukuru serikali kusikia kilio chao.

Kwa hatua ya awali umeme huo umefikishwa katika kanisa la Roman Catholiki Mfereke ambapo baadhi ya wananchi wa kijiji hicho akiwemo Walter Mwanyika,Juliana Mlowe na Flouris Mwanyika wameshukuru kwa hatua hiyo huku wakihoji masuala mbalimbali pamoja na kuomba umeme huo kupelekwa kwa wananchi.

Diwani wa Kata ya Utalingolo Erasto Mpete ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe anatumia fursa hiyo kuwataka wananchi kwenda kunufaika kimaendeleo kupitia nishati hiyo huku akimshukuru Rais kwa hatua hiyo pamoja na Mbunge Deo Mwanyika.

“Leo wanamfereke tumefurahi,nah ii furaha yetu ni kwamba Mh Rais anasimamia vizuri kuhakikisha maenedeleo yanawafikia wananchi wote,Mfereke ilikuwa kama kisiwa kwamba mjini pamoja na Utalingolo kuna umeme halafu hapa hakuna lakini kuanzia leo umekwishafika”alisema Erasto Mpete

Maofisa kutoka shirika la Umeme Tanzania Tanesco mkoa wa Njombe wamefika kutoa elimu kwa wananchi juu ya Matumizi ya umeme huo ambapo Mhandisi mkuu wa Mkoa Meshack Laurent na Desmond Komba Wanabainisha Faida na hasara za umeme pindi utakapowafikia hadi majumbani mwao.

“Mfereke unaenda kuwa mji sasa maana yake hiyo ni faida amabayo mnakwenda kuipata tunachoomba wananchi kuwa makini na miti hasa wakati wa kukata ili isiangaukie miundombinu ya umeme”alisema Meshack

Kwa upande wake afisa uhusiano wa Tanesco mkoa wa Njombe Neema Lyakurwa anawataka wananchi wa Mfereke kuwa makini na vishoka watakaowafuata kutaka kuwaunganishia umeme ndani ya nyumba zao.

Kijiji cha Mfereke kilichopo umbali wa takribani Km 6 toka mjini Njombe kilikosa umeme kwa miaka mingi ilihali vijiji vingine vya kata ya Utalingolo kikiwemo Utalingolo yenyewe kilipata nishati hiyo kipindi kirefu.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...