walimu wa chuo cha sanaa bagamoyo ambao pia ni wakongwe wa ngoma za asili wakimwaga 'gobogobo, jukwaani jana usiku

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  2. Michuzi asante sana kwa picha, na wasalimie sana huko Bagamoyo!Itabidi niende Bagamoyo College kuchuka refresher course ya ngoma. Nilikuwa mcheza ngoma JKT baada ya kupita kruta stage! Tulicheza ngoma nyingi sana..SANGULA, GOBOGOBO, moja ya waKurya nimeshau jina, nyingine ya Wahaya. Walihakikisha tunajifunza ngoma ya kutoka kwenye kila mkoa.

    ReplyDelete
  3. huu ndiyo utamaduni wa mwafrika? mbona huyu shoga bill powers anasema siyo huu?

    ReplyDelete
  4. Wazee wazima hao......Michuzi naomba picha za "MDUMANGE" mwanangu. Watoto hawajui hawa....Chemi Che Mponda....mdumange uliucheza wewe.

    ReplyDelete
  5. Mimi naona mwenye matatizo ni MICHUZI kwa sababu amekuwa akipiga kelele kila mara watu wasitumie lugha ya matusi katika blog yake lakini imeshindikana, sasa ningemshauri kama kuna utaalamu angefanya ili message za matusi zisiweze kuwa posted basi tungefurahi sana. Sijaona ubaya wa picha hata moja iliyo kuwa posted na bwana MICHUZI lakini naona aibu sana kwa kusoma matusi machafu na hakuna hatua anazo chokua kuifanya hii blog isiwe na hayo matusi. Bwana MICHUZI wengine tuna watoto wa umri mdogo ambao kila mara wanapenda kuingia katika blog yako kujionea maendeleo ya Tanzania ukizingatia wameondoka wakiwa bado wadogo na wanaipenda bado nchi yao sasa wanapokutana na matusi mazito katika blog yako na wewe kama mmiliki wa hii blog umeshindwa kabisa kuonya kwamba yeyote atakaye ingia katika hii blog na kupambana na matusi ni hiari yake! Nakushauri Mzee michuzi utafute mbinu kitaalamu kuzuia haya matusi kwa kweli yanawa affect sana watu ambao una post picha zao, na wengine sisi tunao ingia kwa nia njema kuangalia blog yako. Usipo angalia italeta chuki miongoni mwao na wewe mwenyewe. Kuna blog nyingi zinaweza kuchuja comments za watu kabla ya ku postiwa kwa hiyo hata wewe MICHUZI ungeweza kufanya vivyo hivyo. ASANTE SANA BROTHER MICHUZI NINATOA MAONI TU

    ReplyDelete
  6. Mr. Mgoswe,

    Huenda nilicheza. Tulicheza nyingi kweli. Sindimba etc.

    Nakumbuka kuna siku tulikuwa tunacheza moja ya kukata kiuno kweli kweli! Basi jamaa katoka kwenye audience naye kaanza kucheza nyuma yangu, hamna haja ya kueleza alikuwa anafanya nini! Audience walishangilia na mimi nilitoka huko kwa aibu!

    ReplyDelete
  7. Kutoka kushoto ni mwl ,John Mponda Major Dance graduate of Modern and Contemopary Dance in the U.S ,mwl Luiza john Traditional Dance teacher, mwl Issa Acrobats teacher graduate from China mwisho kulia ni Mwl Nkwabi Ngangasamala Major Drama,Mime and Movement Specialist also a Graduate from the U.S.A hawa ndo Bagamoyo players.
    Aliko

    ReplyDelete
  8. Chemi uliamua kutafuta chaka la ngoma jeshini au sanaa iko kwenye damu? Maana watu walikuwa wanaogopa jembe vibaya sana wanaamua kutafuta chaka la usanii, lakini huko wanakuta shughuli ni pevu kuliko hata mraba au gwaride.

    ReplyDelete
  9. Nililima miraba enezi za kruta. Hakuna dawa. Huko nilipokuwa ilikuwa huwezi kusema eti mimi nitacheza ngoma. Hapana, tulifanya majaribio (wazungu wanasema audition) kucheza na kuimba na kuigiza. Lakini nilifanya kazi kwenye kombania ya Ujenzi. Nilijifunza skills nyingi huko.

    ReplyDelete
  10. Aliko,

    Nimejaribu kumtazama mwl Issa bila kumgundua ni nani, akili yote inaniambia ni Joseph Mkodo labda karudi, Duh asante kwa listi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...