ujenzi wa wanja jipya la taifa unaendela kwa kasi na panapo majaaliwa utafunguliwa februari mwakani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Leo asubuhi ndege kubwa kuliko zote duniani ikiwa imebeba jenereta ya umeme yenye uzito wa tani 120 kupeleka Tanzania imeondoka hapa RDU-North Carolina. Jenereta hiyo ina uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosheleza mji mzima. Pengine itasaidia tatizo kubwa la umeme Tanzania. Wasiwasi ni kwamba je ndege hiyo iliyobeba hiyo jenerator itaweza kutua kwenye uwanja huko Dar?

    ReplyDelete
  2. Ni Wanja jipya kwelikweli.Comrade Mkapa alimalizia muda wake kwa kupitisha bajeti ya huo uwanja.Sijui utaitwa kwa jina gani maana msije shangaa kusikia unaitwa JK Nyerere,Mkapa,JK Mrisho Internationa Stadium!!

    ReplyDelete
  3. Mnyama lazima achinjwe hapa hii leo.Uteja sasa basi na ushindi utakuwa YANGA 3-SIMBA 0.
    Gogoro litakalozuka msimbazi litakuwa la kudumu.Kaseja kutolewa kafara.

    ReplyDelete
  4. Ujenzi wa Madaraja na barabara za mikoani bila kusahau Kiwanja hiki ni moja ya vitu vizuri vilivyotuachia Mkapa. Watanzania tunaendelea kumkumbuka.Serikali ya awamu ya nne inatakiwa iendelee kujenga barabara zitasaidia kuinua uchumi wetu. Uchumi haukui kwa maneno ya majukwaani na Propaganda kama anavyotudanganya sasa Waziri wa fedha na Gavana wa BOT

    ReplyDelete
  5. sasa hivi huo uwanja unatumika kama jukwaa.wakati tanzania inacheza na burkina faso nilikaa upande huu ilipopigiwa picha hii,mbele yangu niliona wananchi kibao wakining'inia kwenye mabomba huku wakifaidi mechi.wachina nao walisimamisha kazi na kufaidi mechi.nilihofia mabomba yanaweza kuangika kama ujenzi haujakamilika,ila nilipoona wahandisi(wachina) nao wametulia wanaangalia mechi nikajua usalama upo.

    ReplyDelete
  6. Nakuunga mkono Bw. Mnajimu Mdogo kwamba leo mnyama lazima asulubiwe hapo uwanja wa taifa. Tumechoka uteja!

    ReplyDelete
  7. Anony wa kwanza hapo juu! Asante kwa kuwa informed kuhusu hilo DEGE na Generator! Lakini worry yangu ni hicho kipimo (UNIT) ulichotumia kutoa size ya generator, "umeme wa kutosha mji mzima"!! Hicho kipimo hakipo kabisa ktk umeme! je ni mji gani? Dar au Carolina au Mbeya? Tunatumia MEGA WATT kuelezea nguvu na uwezo wa generator! Naomba nijue hicho! Asante.

    ReplyDelete
  8. Yanga 0 Simba 0. Kwahiyo kuna kila dalili za Yanga kuwa mabingwa tena mwaka huu. YANGA OYEE

    ReplyDelete
  9. Uwanja mzuri sawa, what about Maji na umeme matatizo ambayo yamekubuhu, mkapa sio kwamba amefanya kazi nzuri sana walanini, ubabaishaji bongo bado upo na utaendelea kuwepo tu. What about education and Health? mkapa hiyo awamu ya nne ilisaidia vipi? kuwalundika wanafunzi chuo kikuu wasome kutoka madirishani? ooh bila pesa hupati tiba.....wabongo tumetoka wapi na tunakwenda wapi, ask your self.

    ReplyDelete
  10. WATOTO WA MJINI WAMESHARIPACHIKA JINA LISILO RASMI WANJA HILI WANALIITA 'IMARATI'.

    ReplyDelete
  11. we unaejiita mtaalam inaonekana we ni wale watu wanaopenda kulaumu kila kitu laakini vilevile huwezi kuona Mkapa amefanya nini kama upeo wako ni mdogo! kwa taarifa tu sifahamu nchi inayotoa huduma za afya bure hata nchi za scandinavia ambazo zinasifika kwa kuwadekeza raia wake raia wanachangia afya, sasa bosi chambua mambo kwa kina usukurupuke na epuka kua mvivu wa kufikilia kama umeamua kuchangia humu!

    ReplyDelete
  12. Zemarcopolo (3:41 pm)umenichekesha saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana.

    ReplyDelete
  13. Ni matumaini yangu wanaujenga huo uwanja kwa uhakika maana isije ikafika mwaka tukaanza kusikia mara kuta zinadondoka mara sijui kuna matatizo gani ambao itakuwa si kitu kizuri, Bora wachukue muda kujenga lakini wafanye kitu cha uhakika once and for all. But it looks very nice.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...