mshambualiaji nyota mwenye jezi namba tisa mgongoni wa ipp media mauldi baraka wa kitenge akimvisha pete ya ndoa mkewe mpya wakati wa harusi yao hivi majuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. wee Dada ni kiboko. Nakubali kwamba wanawake ni wengi kuliko wanaume lakini hayo mambo ya uke wenza yamepitwa na wakati. Sasa usikae ukajiachia eti unaposi na bi mkubwa kwenye picha moyoni mwake hujui! Atakuwa hana raha nawewe jiandae kumkaribisha mke wa tatu wembe ni ule ule alivyo kupata wakati yuko na mke wakwanza ndo atakavyo enda kumtafuta wa tatu basi kazi kwenu. Sisi wengine macho tu

    ReplyDelete
  2. oh oh Siinglii maamuzi ya mtu lakini Maulidi mwana wa Kitenge umechemsha kutinga wa pili!!! Mie nafikiri karne hii si ya kuchangamkia wake wengi wakati 'rasilimali' tunazo chache.....Lakini yoote tuyaache Michuzi huyu jamaa namkumbuka saana tena saana, pale bongo na kipindi chake cha Muziki na Michezo, Redio one stereo....sauti yake ilikuwa inanifanya hata kama nafanya kazi niache nikimbilie redio....jamaa huyu ana Kipaji cha utangazaji kama kijana mwingine Godwin Gondwe-Double G....au Othman Milaji wa DW-Ujeruman

    ReplyDelete
  3. he we kitenge umeoa mke au mama akuleee,mbona wapenda watu wazima?

    ReplyDelete
  4. Jamani hata katika enzi hizi za UKIMWI bado kuna mambo ya kuoa wake wawili? Kitenge akiwa kama muadishi wa habari maarufu hapa Tanzania akustahili kufanya kitu kama hiki.

    ReplyDelete
  5. Bwana harusi Kitenge amevishwa pete na yeye?
    Vipi kuhusu ile pete ya mke wa kwanza itakaa kidole kilekile na ya mke no.2 au itahamia mkono wa pili?

    ReplyDelete
  6. Jamaani eehhhh maoni yenu nimeyapata, lakini wake zangu nawapenda wote.

    ReplyDelete
  7. Nakufagilia sana Kitenge umefanya jambo la maana wake zako wazuri.

    ReplyDelete
  8. Duu Kitenge yaelekea unapenda MIJIMAMA. Kwanza wasichana portable ambao ungeendana nao huwaoni? Ona sasa hao wako kama mama zako.

    ReplyDelete
  9. kitenge, hongera kwa kuweka mambo hadharani kuliko wenye wake pembeni halafu wanawabatiza jina 'nyumba ndogo'. Pamoja fuata 'nyota ya kijani!!maisha magumu bro, hakuna free lunch!!!

    ReplyDelete
  10. NO, wait a minute, Ati nini?!!! Kitenge kaoa mke wa pili? Hayo mambo yamepitwa na wakati, Kitenge please!!! Unatutia aibu!

    ReplyDelete
  11. Eti nini?? unawapenda wake zako wote?? lazima unatatizo, kwani huyo wa kwanza kakosa nini mpaka ukaleta na mwingine kama sio tabia chafu na hutaacha utaongeza tena na tena maana huo ni ulafi wa ngono, ulichokikosa kwa mke wa kwanza ndio unafikiri utakipata kwa mke wa pili huko ni kujidanganya, la muhimu ni kukaa na mkeo uliempenda na ukasema huyu ndio mke wangu mkatatua matatizo yenu yawe ya kimaisha, kistarehe au kiuchumi solution sio kuongeza mke mwingine utaweza kutimiza nyege za wanawake wawili wewe labda kama utatumia viagra, la sivyo nao akili mkichwa lazima wakajipe raha wenyewe huko na vibustani vingine. sio rahisi penzi la kweli kugawanyika unasema tu eti "NAWAPENDA WAKE ZANGU WOTE" huyo mke wa kwanza kakubali tu labda ndio dini ya kiislamu imemkolea au atakwenda wapi tena saa hizi mashine yake imeshakongolewa. sidhani karne hii ya kupiga vita ukimwi bado wewe unaendeleza shikamoo jazz band imepitwa na wakati. sasa kwanini watu walipiga vita mama Salma kwenda kuhudhuria sherehe za Mswati kule Swaziland si kwa mambo hayo hayo. sasa nawewe kaka hesabu zako ni zero, supu yako iko jikoni subiri.

    ReplyDelete
  12. Mke wangu wa kwanza alikua hazai na mimi nahitaji watoto ndio maaana nimeongeza huyu kigoli, nadhani nimeeleweka

    ReplyDelete
  13. Kitenge ma-wife wako ni wazuri, wasikubabaishe watu na vi-portable. hao portable hata ndoo ya maji hawawezi kunyayua.
    sisi ni wabantu (mke tako tako, paja paja). Sio kukimbilia visichana vinapepesuka njiani kwa upepo utadhani viko Darfur na havijala wiki 2, kisa eti vi-potable eti. mwanamke guu babu ee

    ReplyDelete
  14. umri huo una wake wawili je ukifika miaka 50? walahi utakuwa na wake 20 wewe manake huyo wa kwanza mwenyewe wala hujamwoa siku nyingi kweli wewe kaka una mambo. huna hata haya!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  15. Wewe Kitenge hujatulia, kama huyo wa kwanza hakukutosha hata huyo wa pili pia hawezi kukutosha!

    ReplyDelete
  16. Bwana Maulid Hongera sana kwa kuoa mke wa pili oa tuu kaka nafasi unayo bado wawili kaka! ila sasa inabidi trip za magomeni pale mahakama ya pweza ziongezeke maana shemeji zangu hao wameshiba na hakikisha hauna ratiba za jioni au usiku kutangaza !kamua baba kamua baaba kamua! Mimi ni Dee hakuna kuficha jina kwenye suala kama hili!

    ReplyDelete
  17. HONGERA KAKA ILA MMH UNA MAMBO... UMRI MDOGOOO WAKE WAWILI TAYARI SASA UKIFIKA 60'S WATAKUWA WANGAPIII??

    KWELI HILI NI SWALA BINAFSI LAKINI LINAUDHI NDIO MAANA WATU WANASHANGAA. KWANZA KUNA MAGONJWA, UMASKINI WA TAIFA LETU, NA COMMITMENT AND LOVE KWA HAO MABIBIE!!!

    KWANI UNATAFUTA NINI KWA WANAWAKE WAWILI WAWILI.. NA YENYEWE YALIVYO MAPIMBI YAMEKUBALI TUU NA KUTABASAMU NA MIMWANYA HIYOOOO!!! SASA AU DA REHEMA NDO ANATOA MAPESA YA UN NA HUYO MWINGINE NI MAMA WA NYUMBANI?? SIONI SABABU YA MSINGI KAMA MMOJA KASHINDIKANA MUACHE ALAFU UOE MWINGINE WATAKUZEESHA BUREEE ULIZA WENZIO WALIOTANGULIA NA MITALA...

    ILA KAMA SIO MAPEPE NA UMEPENDA UWE NAO WAWILI NI JAMBO LA BUSARA KWANI BORA WEWE UMEWEKA HADHARANI KULIKONI WALE WANAOKUWA NA MADEMU KIBAOO NJE YA NDOA. ILA UWE MAKINI KWANI WEWE UTARIDHIKA ILA KUARIDHISHA HAO WAWILI NI KAZI HIVYO ITABIDI UWARUHUSU JAMAA NJE WAKUSAIDIE
    BYEEE DEAR AND ALL THE BEST

    ReplyDelete
  18. JK pasu pasu na nchi za nje
    Ikiwa ni wiki tu aliporejea nchini baada ya ziara ya Uingereza na Qatar kwa siku tatu hizo, Rais JK anaanza tena na safari hii ni huyo Switzerland.

    Anakwenda huko kuhudhuria baraza la viongozi la kila mwaka
    kujadili hali ya uchumi, siasa na jamii duniani na utamalizika Januari 28 mwaka huu.

    Then huyo ataelekea Addis Ababa Ethiopia kuhudhuria kikao cha viongozi wa Nchi za Afrika cha Januari 29 na 30 mwaka huu.

    Pamoja na ziara kibao za hapa nchi alizofanya, baadhi ya Wabongo wanahisi kuwa JK anazungukia mno Ughaibuni kuliko kawaida.

    Tangu atinge madarakani amekuwa na safari zifuatazo kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kitaifa na kiserikali.

    Januari 19-25, 2006 ? Khartoum, Sudan Mkutano AU
    Machi 23, 2006- Ziara Kigali, Rwanda.
    Machi 22, 2006- Ziara Kampala, Uganda.
    Machi 24, 2006 Ziara Nairobi, Kenya.

    Aprili 19-20, 2006 Ziara Lesotho na Swaziland.
    Aprili 21-22 , 2006 Ziara Maputo, Msumbiji.
    Aprili 28, 2006 - Ziara Harare na Bulawayo, Zimbabwe.
    Aprili 6, 2006 ? Ziara Gaborone, Botswana.

    Aprili 10-12, 2006- Ziara Widhoek, Namibia.
    Aprili 7-9, 2006 Ziara Pretoria, Afrika Kusini.
    Mei 12,2006 - Ziara ya kiserikali Uganda, alikaa Mei 13, Arabuni Mei 15, Ufaransa Mei 16-19 na Marekani Mei 21-26.

    Mei 31-Juni 3- Ziara World Economic Forum, Capetown Afrika Kusini.
    Julai 4- 2006- Mkutano wa AU,Banjul Gambia
    Julai 10-32, 2006 Capetown Afrika Kusini , Mkutano wa viongozi wa serikali ulioandaliwa na kampuni ya Microsoft ya Marekani.


    Julai 20 ? Kuhudhuria mkutano wa Leon Sullivan Summit Abuja, Nigeria.

    Julai 21 -22, 2006 ? Kucheck afya Berlin Ujerumani.
    Agosti 19-20- Mkutano wa SADC, Maseru, Lesotho.
    Agosti 21-22- Ziara Luanda, Angola.

    Septemba 12- Havana Cuba maandalizi ya kikao cha NAM
    Septemba 15, 2006 Madrid, Hispania kwenye Uwanja wa Mpira- Real Madrid.

    Septemba 15 -18, 2006 Havana Cuba, Mkutano wa NAM.
    Septemba 19-25 - Kuhudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

    Katika ziara ya JK iliyoanza Oktoba 19, 2006 alitembelea nchi za Japan, China, Korea Kusini na Falme za Kiarabu.

    ReplyDelete
  19. MH!!!!!!!!!!!!!MUNGU AKUSAIDIE!

    ReplyDelete
  20. WATU MNA ROHO NDOGO - NYOTE NYIE MLIOMSEMA MAULID NA WAKE ZAKE - MNAFANYA KAMA HAMJUI WATU WANA WAKE WAWILI? NA WANAISHI KWA AMANI - INFACT WENGI WALIOKO KWENYE NDOA ZENYE WAKE WENZA ARE HAPPIER KULIKO WALIOKO PEKE YAO - KWANI WALE WALIOKO PEKE YAO WAJUA WAME ZAO WANAVIMADA NA WANAOGOPA KULETEWA UKIMWI WACHA KUTOJUA MUME YUKO WAPI NA KUFA NA MAWAZO - PRESSURE TUPU. ESHI AT LEAST ANAJUA MAULID YUKO NA REHEMA - NA VICE VERSA. NA HATA KAMA ATAOA NA MKE WA TATU AU WA NNE, SO WHAT? DINI YAKE INAMRUHUSU NA WAKE ZAKE WANARIDHIA - NYIE INAWASUMBUA NINI? ACHENI CHOKOCHOKO - WATAKIENI WAKINA KITENGES MAISHA MEMA NA AFYA NJEMA.

    ReplyDelete
  21. Ndg yangu kitenge nakuonea huruma maana siku zijazo utajuta na kuona kuwa ulifanya maamuzi yaliyolengwa zaidi na tamaa ya macho na siyo busara.Madhara ya haya siyo "leo" ila ni "kesho".

    Mkianza kuvurugana pia mtuletee ujumbe huu miaka ijayo kwa bwana michuzi.

    Pole ,maskini kitenge!

    ReplyDelete
  22. MTOTO MZURI KUJIZEESHA NA MIMAMA,WANAKULEA NINI?KUNASIKU SAUTI ITAKAUKA NA UTASHINDWA KUTANGAZA,WAKE WAWILI MCHEZO?

    ReplyDelete
  23. mhh, mie namkumbuka Rehema kayugwa toka shule she was a beauty na roho yake ilikuwa nzuri na usikute Maulid anauona huo uzuri ndi shauri kamuoa na ndio shauri mke mwenza anpatana nae. Mungu awajalie maisha mema na ya amani pamoja.

    ReplyDelete
  24. Jamani mbona mnajisahau na kusahau utamaduni wenu, au kwa kuwa mko nje ya Africa. Kumbukeni kwamba serikali ya Tz haitoi monthly welfare check ambazo zinawafanya wanawake wa nchi za majuu kuwa kama walivyo. Well huo ni utamaduni wao wa kutothaminiana. Well anachokifanya Kitenge ni kuendeleza utamaduni wetu wa kiafrica wa kupendana na ku take care of each other, kama walivyofanya wazee wetu waliopita. Kumbuka baba yake Nyerere alikuwa na wake kumi, na Bill Clinton alikuwa na !!!!!. You know what Iam talking about. So who is better Late Nyerere's father or Bill Clinton? Bravo Kitenge,Usisahau kwenda kupima na wake zako kila baada ya miezi sita. Ushauri huu ni wa bure ni kwa kila mwana blog please. It does matter if your single, married with one wife or multiple wives.

    ReplyDelete
  25. Michuzi asante sana kwa picha na news unazotupatia.

    I can't believe poligyny bado inaendelea TZ. Kuna mtu amesema kwenye comment kuwa nchi zilizoendelea hazi practise hii kwa vile Govt inawapa raia wao wellfare. Lakini hiyo sio kweli. Kuna mtu amesesema kuwa babu zetu walipractise hii kwa hiyo what is wrong?

    Ukweli ni kuwa wanawake wanchi zinazoendelea wamefundishwa usawa. Pia wamefundiswa kusimama kwa miguu yao yote miwili. Peke yao bila kutegemea kuwa mwanaume ndiye atakayemtunza katika maisha yake.

    Pia kama babu zetu walipractise this thing lakini karne yao umagonjwa yalikua sio mengi kama saa hivi.

    Ila mimi nawaambia wanawake wenzangu nyumbani...Look for love not money. We should learn to be strong. Hivi kweli mtu unapenzi la kweli kuligawa mara mbili. I can't see myself sharing a man with someone else i don't even know neverthe less my best friend... That is why kila nikiona mbongo mwislamu nakimbia mbali sana...kwasababu there is no guarantee that I will be the only wife in his life.....I am sorry but it is me.....

    hey women wake up gallllllllls. What you have less to make you to accept to share a man with someone.....why.....??????


    Hongera ndugu yangu you are a very lucky man

    ReplyDelete
  26. Kitenge umesema Bi Mkubwa alikuwa hazai, je una uhakika gani kwamba Bi Mdogo atakuzalia mtoto? Na si ajabu wewe mwenyewe ukawa una tatizo la uzazi na sasa umelisukumia kwa mkeo. Ngoja tusubiri picha za harusi ya Mke wa tatu na huyo Dada wa UN atakuwa anaishia. Sasa hivi Rehema anafurahia kwa kuwa anaingia kwenyee nyumba, siku ukimwambia unamuolea mke wa tatu ndiyo siku atakayotangaza kuondoka!

    ReplyDelete
  27. "But the Jews will not be pleased with thee, neither the Christians, until thou follow their religion; say, The direction of Allah is the true direction. And verily if thou follow their desires, after the knowledge which hath been given thee, thou shalt find no patron or protector against Allah." (Qur'an, Surat Baqarah:120). Kaka Kitenge fuata moyo wako na mfuate Mungu wako achana na maneno ya walimwengu.Kama ungeamua kua na kimada nje hakuna ambae angekupinga hapa kwasababu ni mila yao ila kwasababu umefanya kitu cha kiislamu basi kwao ni kero kwao na "hawatokuridhia hadi umefuata mila zao".Mwenyezi Mungu alieruhusu hata manabii kuoa mke zaidi ya mmoja hakuwa kutengua option hiyo na hakuna hata nabii alietengua,ingawa watamsingizia nabii wa pili toka mwisho ila yeye hakuja kutengua maandiko ila kuyatimiliza. Dini yako inakuruhusu basi wewe songa na maisha yako.Hivi UKIMWI unaupata kwa kuwa na wake wawili au kutokuwa na uaminifu ktk ndoa? Nchi za uarabuni wanaoa wake wengi wengi ila hakuna UKIMWI kama Afrika, Ulaya na Marekani.Maulid nakupongeza kwa kuoa kwa ridhaa ya mke mkubwa kama dini yako inavyokuambia tofauti na waislamu-wanaume wengine wanavyofanya;BIG UP.DUMISHA UMOJA KTK NDOA ZAKO NA MKIFARAKANA MTAWAPA HAWA VISHANKUNAKU KITU CHA KUONGEA,NA HUENDA THEY ARE BEHIND YOU NOW,WATCH YOUR STEPS WITH EXTRA-CAREFULNESS.MAY GOD BLESS YOU AND YOUR WIVES AND CHILDREN AND DEFEAT ALL YOUR ENEMIES...AMEEN!

    ReplyDelete
  28. wewe mama anon wa January 25, 2007 10:58:11 PM, naona unachemka! Siyo kwamba Kitenge ni lucky man, isipokuwa hao wanawake ndiyo wako lucky, maana kijana kama huyo kuna wanawake wengine 1,000,000 wangetamani kuwa mke wa tatu, leave alone kuwa 'nyumba ndogo'. Wanawake wa mamtoni wanasemekana 'wamejikomboa' na kusimama kwa miguu yao kama ulivyosema, lakini unajua number one killing disease kwa wakina mama mfano USA? HEART DISEASES (hasa yanayotokana na depression). Research zimeshaonesha kuwa wanawake ma single (hasa single mothers), ndiyo the biggest risk group kuliko walio kwenye ndoa ya furaha. Walio kwenye ndoa ya mke mmoja wako more susceptible to cheating (hiyo hata kwenye nchi zilizoendelea), ndiyo maana kesi za kuuana mke/mume USA ni kubwa mno. Mtu anakuwa amepata kimada, anaogopa kuvunja ndoa yake akiogopa kuwa kutakuwa na child support/au anaogopa dini yake/atakosa custody ya watoto, anaamua kupanga na kimada wake au mtu mwingine kumuua mwenzie. Nadhani hiyo ni dhambi kubwa zaidi kuliko alichofanya Maulidi Kitenge. Kwa hiyo inabidi uangalie kwa mapana, ukizingatia kuwa huyu jamaa amekuwa muwazi.

    ReplyDelete
  29. Maskini mie mlalahoi niseme lugha gani Maulidi mwana wa kang anielewe.....maskini jamani, mie machozi yananitoka..
    Mpaka sasa sensa inaonyesha kuwa wanapinga Maulidi kuoa ni isilimia 68.18( kura 15 kati ya 22) na wanaokataa ni asilimia 18.18(kura 4), na wale wanaoegamia kote ni asilimia 13.64!(3)

    Takwimu ni sahihi
    Source: wachangiaji

    ReplyDelete
  30. Nyie binadamu, msijidai kumpaka matope Maulidi eti mjinga na hao wake zake, kwanza ni maisha yake ameamua mwenyewe sioni kama ni tatizo, pili wanawake wanajidai hawapendi uke wenza wkt kazi yao kubwa ni kutembea na waume za watu sas ahuo kama sio uke wenza ni nini??? ni kwamba labda hamja formalize ndio sababu. Mimi wka upeo wangu i think mtu aachwe afanye aachodhani wka maisha yake its right for him, rehema has been married once na ana watoto she is a nice woman let he rlead her life the way she thinks its right for her, the same applies to Maulid and Eshe tu.
    Maulidi hongera sana ishi unavyotaka afterall yote ni maneno na uelewe kila mtu ana kuwa na mawazo yake wote hatuwezi kuwa sawa hata siku moja ndio maana wengine hawaoi kabisa. mimi skushauri ujibu haya mashambulizi humu yasome kwa raha na amani . mimi nakutakia kila la kheri kaka yangu!!!! kama ni hela za rehema kuleni kwa raha zenu she is ur wife . tanua babu!!!

    ReplyDelete
  31. Mwanya ,Pengo ? Mjomba Kitenge hawa wote wivu tu ! Mwanaume gani angekataa kuwa na wanawake wawili wote wake !
    Lakini mjomba inaelekea mgonjwa wa mwianya (wingi wa mwanya !)
    Naona wote wanao !

    ReplyDelete
  32. Dume la Kiafrika ni mithili ya wildebeest (gnu) bull. Lakusanya majike!

    ReplyDelete
  33. Hii picha inasema yote. Bibi anavalishwa ring lakini macho yako kwingine....sijui anamwangalia bibi mkubwa nakumwambia now what......

    ReplyDelete
  34. haya wewe anon wa jan 25,2007 10:58pm, mbona hata hujui unaongea pumba gani????!! unasema unapomuona mbongo mwisilamu unakimbia mbali sana,sasa bora kuoa wake wawili au kuwa na kimada pembeni,hebu wacheni kuona gere kama kuoa ameoa yeye nyinyi inawakereketa nini wacheni roho mbaya zenu musitie vijineno vyenu mwacheni kitenge atanue na wake zake wawili hongera kitenge bado nafasi mbili zimebaki ukipata nafasi pia zitumie

    ReplyDelete
  35. Kwa wale wenye kulilia usawa wa jinsia (gender equality), itawabidi kufanya mapinduzi ya kilingwistiki:

    Mwanaume ni Mtendaji:

    1. Mwanaume anaoa!
    2. Mwanaume ana...a!
    3. Mwanaume = active voice!
    4. Mwanaume = independent variable!

    Mwanamke ni Mtendewa:

    1. Mwanamke anaolewa!
    2. Mwanamke anato...wa!
    3. Mwanamke = passive voice!
    4. Mwanamke = dependent variable!

    ReplyDelete
  36. anony wa jan 28, 2007 12:15:00 AM ni bingwa wa pumba za kila nafaka.What is civilization to you? Kwa Kiswahili ni "ustaARABU", yaani kuwa au kufanya kama waarabu au kiarabu(katazame nenp "ista'arab" ktk lugha ya kiarabu ambako tumelikopi) na kwa msingi huo Kitenge kastaarabika.Hakuna hata hoja ya msingi umeitoa.Eti "hata waislamu wenyewe siku hizi washaona kuoa mke wa pili sio ishu".Nataka kukujulisha na kuwafahamisha watu wengine wasiofahamu kwamba sheria,mila na desturi za Islam hazitokani na mtu mwingine,muislam mwingine au mabadiliko flan duniani;HAPANA.UISLAMU upo vilevile na sheria zake zote hadi siku ya KIAMA.HII NI TOFAUTI SANA NA DINI NYINGINE AMBAZO ZINABADILIKABADILIKA "ILI KUENDANA NA WAKATI".SEMENI MTAKAVYOSEMA,KITENGE YUKO RIGHT KWA 100%.KINACHOONEKANA HAPA NI CHUKI DHIDI YAKE,WAKE ZAKE NA DINI YAKE KAMA MAONI MENGI YANAVYOONYESHA.PILIPILI USOILA YAKWASHIANIIIIIIIIIIII????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????????

    ReplyDelete
  37. Weee anoy jan 28 12: 15 unaongea nini. Nani anachuki na Kitenge au nini....Mimi ni mmoja wa watu tuliotoa maoni lakini kitenge simjui na wala [wa]mkewe si wafahamu ..saa uchungu niwe nao waniniiiiii

    Hii picha na idea ya ndoa mbili ndio watu wanazungumzia hamna hata mmoja mwenye person issue na kitenge wala niniiii

    hao wanaosema watu wa tanga oh... sijui majinguuuu... naona mmekunywa maji tu.....

    Hii picha inarepresent life style ya TZ na ndio maana watu wameandika.....sasa kama wewe imekutouch personal kwa vile watu wamesema kuwa dini yake inaruhusu ...ni kweli dini yake inamruhusu kuoa wake wawili ....sasa ...kama mtu kwa adili za dini na economy status ndio watu wanachangia idea zao....napenda kueleza ukweli

    Mimi nimeondoka bongo miaka mingi sana na nimerudi three time only na nikija ni mda mfupi sana na wala siishi dar sasa huyu KITENGE kama unamjua wee mimi simjui kabisa.... TY

    ReplyDelete
  38. mmmh!!! huyo Maulid hajatulia kabisa ana PEPO YA NGONO huyo! mie hapa nawajua wanawake alionao tena baada ya ndoa ya pili kibao kama wa 3 hivi na ameahidi kumuoa mmoja wapo... anadai eti dini inakubali wake wanne! kazi kwenu mutasema mutachoka labda mumpe tiba ya pepo ya ngono huyo... But tuwe wakweli kijana ni Handsome na hiyo blackspot usoni utadhani kaweka doa la wanja!!!! ila kaka Mau.. fainali uzeeni kiuno hicho!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...