wadau ujumbe huu mwanana umeingia sasa hivi toka newala...
Michu! Mambo vipi mshkaji?
Natumaini mzima sana. Angalia hiyo picha nimekutumia niliyopiga Starbucks. Mwezi huu wana-showcase kahawa ya Tanzania katika starbucks zote hapa New York.

Starbucks ni very popular cafe sio nyc tu bali marekani nzima na hata duniani. Wanauza kahawa na chai bei ghali sana, around $5 kwa kikombe lakini wengi bado wananunua. Sasa kila msimu fulani huwa wanauza coffee beans kwenye paketi kama ya kwenye picha kutoka nchi mbalimbali kama kenya, ethiopia, rwanda, columbia nk.

Sasa ndio wanauza ya TZ katika maduka niliyoona hapa ny. Naamini pengine wanauza katika miji mingine katika msimu huu. Kuna maduka kama 500 ny state, kama 7000 marekani nzima na kama 6000 nchi za nje. Tazama www.starbucks.com/ourcoffees utaiona kama moja ya "featured coffees". Nimeona kwamba huo mfuko unauzwa $13 hivi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2007

    Asante sana Mdau na asante Michu kwa kutotupa kapuni picha hii nzuri. Ni vema tungepata picha inayo onyesha trademark nzima. Je hiyo trademark ni ya kwao? Wanaweza pia kutumia jina Tanzania hata kama kahawa wamenunua Burundi?


    Hii ni kukiuka mkataba wa WTO unaojulikana kama TRIPS Trade Related Aspects of Intellectual Property Rights. Nadhani wadau mlifuatilia Ethiopia walivyotetea kahawa yao na sasa kahawa ya Ethiopia lazima iuzwe kwa official trademark ya kiethiopia.


    Wadu wenye picha kama hizi au za mbuga zenye majina ya Kitanzania naomba mnitumie analystmunge@yahoo.com au mtume kwa Michu tutaziona kwenye globu yetu. Asanteni

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2007

    Huwezi amini nimeiona nikainunua. Mimi sio mnywaji wa kahawa lakini I was so happy to see our country's name in that shop.

    Nadhani labda wameileta kutoka kwetu in big bulks lakini packing wakafanyia hapa. Hiyo style yao ni hiyo hiyo kwa kila coffee wanazoweka.

    Nitaenda kuifungua nione inatest vipi.

    Ila kuna duka moja lipo Hoboken, NJ. Is a gourmet coffee shop and very pricy. Wao wanauza kahawa na chai ya Tanzania na nimelijua hilo duka miaka mingi tu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2007

    ndugu zangu tuamke. mkisikia unyonyaji huu ndo unyonyaji hasa. hebu angalia kamfuko ka nusu kilo kanauzwa usd 13.- marekani wakati mkulima wa kule karagwe kilo moja ya kahawa anapewa shiling 200.- za tanzania(usd 0.15). hivyo kwa kilo moja jamaa wanapata faida ya 8,566%,sasa hata kama kuna gharama za uzalishaji,usafirishaji etc surely faida haitapungua 5000%. si kahawa tu, ndugu zangu kwa taarifa yenu kilo moja ya tumbaku inatoa pakiti 20 za sigara (zenye 20 sticks). mnyamwezi wa urambo akibahatika kilo moja ya tumbaku analipwa tsh 800.- (usd 0.75), sasa mlio ughaibuni angalieni supermarket bei ya pakiti moja ya sigara ni usd ngapi na hapo ndo mtajua unyonyaji manake nini? tujiulize hivi na hali hii kweli umaskini tutaufukuza vipi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2007

    enyi wabongo mlioko majuu tafuteni namna ya kupata mtaji tujenge viwanda vya kusaga na ku pack kahawa hapa Tanzania , hawa wazungu watatumaliza. na sisi tuuze finished goods jamani!!! vinginevyo twafwaaa, tukiendelea kuuza raw coffee,cotton, tobacco etc umaskini hautokwisha.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2007

    angalia Watanzania wasivyoweza kujiamini. OOh Michuzi nimeona Kahawa ya TZ New York, sijui dunia nzima blah blah!. Hivi huyu mdau alifikiri ile Kahawa ya Tanzania ikiuzwa inakwenda wapi? au ile Pamba inakwenda wapi? Kama sio masoko ya Ulaya na North America. Ndugu mtaelimika lini?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 30, 2007

    Anon uliandika kuhusu hilo duka la NJ kama unaweza kunipatia jina kamili au any further contact info zake nitashukuru.

    Wadau wote humu ndani, Wichita KS kuna Africafe, Chai Bora, Green Label tea (kawaida na tea bags). Sasa hivi vijana wanafikiria kusambaza throughout the mid west. Kama kuna mtu humu ndani anahitaji naomba atoea contact info zake ataletewa popote alipo ndani ya USA. Bidhaa zote hizo zipo katika vipomo vya 100g

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 30, 2007

    There is always that "feel good" factor tunapoviona vya nyumbani kwenye maduka ya ughaibuni, twajua kwamba kwa miaka mingi tumekua tukiuza kahawa, pamba na madini yetu nchi mbalimbali duniani lakini vinapoingia kwenye soko la dunia havionekani kama zimetokea Tanzania. Wakenya na wahindi wamekua wakitupiga bao kwa sana kwenye kahawa na madini ie tanzanite, wananunua hivi vitu kwa wakulima huko bush then wanavipeleka makwao afu ndo wanawauzia wazungu kwa bei kubwa. Ni miaka mingi sana tumekuwa hatuna direct access ya world market, kwa mfano ni wachimbaji wangapi wa dhahabu kule nyarugusu au tanzanite Mirereni wanauza moja kwa moja New York? Same applies kwa wakulima wa kahawa, hawana channels zaidi ya kuwasubiri wahindi wakawalalie kwa bei hizo za mia 200 kwa kilo na they can not be blamed for this. Inauma sana kuona fresh flowers in Tescos za hapa UK zina labels za Kenya but we all know that they buy them from Arusha, why cant we sell direct to Tesco? Tanzanite yapatikana kwetu tu dunia nzima lakini huko kwenye world market Kenya na India zinaongoza kwa mauzo! And of course....wazungu kibao wanajua mlima Kilimanjaro upo Kenya? Have we ever wondered why?Nafikiri its all down to the government to do more on this, tusitegemee wakulima wajinasue peke yao kwenye hili, and yes Im happy kwa hiyo kahawa kuonekana huko US in our very own name and I think the government is begining to get serious but more effort is needed.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 30, 2007

    Starbucks ni miongoni mwa makampuni yanayo nyonya sana wakulima duniani na hawarudishi faida katika society/community- hapa USA wana ita give back to the community- sababu ndiyo watu walio kununua products zako mpaka ukawa tajiri. starbucks ni wabaya sana Ila hatuna jinsi, sasa nani atanunua ? pamoja na ukweli kwamba hapa wana nyonya sana wakulima na kuwafanya kuendelea kuwa maskini milele. Hapo majuzi starbucks walilazimishwa kuwa wana toa sent moja ya dola kwa kila kikombe cha kahawa wanayo uza ili zirudishwe kwa wakulima katika nchi maskini sijui kama walifanya hivyo au la! si kampuni nzuri hata kidogo kila kona hapa Marekani utaona watu wamevaa T-Shirt zina tukana Starbucks , ni makupe hasa na wanyonyaji. lakini swali ni lile lile sasa nani atanunua ?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 30, 2007

    Na mimi naungana na wadau hapo juu, TZ na Africa tukiendelea hivi-tumekwisha (ofcourse tulishakwisha). yaani watu wanapata faida ya kukufuru! Wakati wazazi wetu wakiendelea kufa kwa umaskini. Yaani dunia ilivyotengenezwa na wajanja-its tough, sijui tufanye nini tuweze kusurvive!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 30, 2007

    Huyo mbongo alieona kahawa Starbucks na akaipiga picha anashangaza kweli. Inaelekea hajaingia Starbucks. Hiyo label imekuwa ikitumika kwa muda mrefu tu zaidi ya miaka miwili sasa, sijui muda wote huu alikuwa wapi? Kwahiyo, it is not news to have that label.

    Na huyo anaesema wabongo walio majuu wawasaidie kupata mitaji ili wajenge viwanda vya kusaga na ku pack hahawa ya TZ. Mitaji tunayo ispokuwa watu tuliowaamini kuwapa majukumu (wasasiasa) hawajui wanachokifanya. Wakati rais akisafiri majuu huenda kuomba na kutumbua kodi zetu na akirudi anadai mapesa yake wakati ni pesa za walipa kodi. Pesa zinaitwa mapesa ya Kikwete, nani kasema mapesa ya kikwete? Amezitoa wapi wakati hajaandika hata kitabu ili tusema "that is how he made his first $10 million". Muandikie Muheshimiwa rais umpe huo ushauri kwani ni ushauri mzuri tu. Kama unataka e-mail ya ikulu ingia Jambofurums kwenye articles za Mwanakijiji utapata hiyo anuani. Utaona jinsi gani hawa wanasiasa wanavyotudumaza akili. This is rude, mean, sad, and unfortune.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 30, 2007

    Hapa ni baadhi ya makampuni yalikuwa chni ya wabongo na tukayauwa na kuuza , je wewe ndugu hapo juu unasema eti tutume pesa ili tufungua viwanda zaidi , plz plz plz tizama kama hivi viwanda vipo wapi sasa Kiwanda cha nguo (motex), Chama Kikuu cha Ushirika, kiwanda cha kutengeneza radio (Philips ya arusha), Mamlaka ya kahawa Moshi, kiwanda cha Sukari (TPC na Mtibwa), Kiwanda cha Dhahabu (mwadui) Kiwanda cha nguo (Ubungo). Pia tulikwa na tunategeneza viatu na duka kubwa karibia bongo yote ilikuwa ni Bora shoes, mashamba ya katani (Tanga) , National Housing Corporation na Mlima Kilimnjaro pia wakenya wanasema upo upandewao pia kwa ajili wanavyoutangazia duniani, Muuulize mtu yoyote kuwa unajua bongo, wengi wanakuwa wapafahamu ili ukisema ipo karibia na Kenya, hapo ndio wengi wasema ndio ndio. bongo hii watu wanaofahamu ni kwa ajili ya baba yetu mwalimu enzi hizo na sasa wanafahamu kwa ajili wale mjitu ya kishetani waliofanya mambo yao ubalozi wa usa ndio news ilipotokea kila mahali ilipotapakaa. Swala tizama kuanzia mwaka 1962 mpaka sasa kuna viongozi wapo kwenye madaraka mpaka sasa ndio maana wanaona kuwa watoto wa walalaoi wakipata nafasi ya kusoma nje ndio watakuja kungombea uongozi so njia rahisi kuwafanya wajinga waendea kuwa na ujinga nawenye pesa waendelea kuwa napesa ili wasomeshe watoto wao . Mzalendo

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 31, 2007

    Anoy 5:15 labda hujaishi nje ya cnhi. Hivyo vyote unavyosema vinaunzwa nje ya nchi lakini huwezi amini huwezi kuona label kam hii ki urahisi. Wakishaileta huku basi jina limebadilishwa na kuitwa colombian coffe au jina lingine.

    Miaka ya nyuma ukieka jina la nchi hata haijulikani au hamna anayesifia au kutangaza watu hawanunui. labda hata wameanza kuuza siku nyingi tu lakini hawakuonyesha kuwa imetoka Tanzania.

    Consumer psychology

    Kwa hiyo sio kuwa hatujaelimika ila hata vikija huku haviekwi label yetu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 31, 2007

    Baadhi ya wana-blog wametoa kero zao jinsi tunavyonywa na makampuni ya wakubwa, kama ilivyo kahawa yetu na Starbucks ya Amerika.

    Mazao ghafi yetu, toka madini hadi magogo ya mbao, ni sawa na yale yanayoisibu kahawa yetu.

    Rais Museveni Kaguta wa Uganda anaamini kuwa Afrika inatoa "misaada" kwa nchi zilizoendelea.

    Museveni aliyasema hayo kwa kujieleza Septemba 21, 2005 katika mahojiano na Princeton N. Lyman (balozi wa zamani huko South Afrika na Nigeria) Ralph Bunche Senior Fellow for Africa Policy Studies, Steven Radelet, Senior Fellow, Centre for Global Development na Leonard H. Robinson, Jr., President and Chief Executive Officer, The Africa Society, wote wa kutoka Council on Foreign Relations ya hapa Amerika.

    Wataalamu hao walimwuliza Museveni maswali mengi. Museveni aliyajibu ikiwa ni pamoja na jibu lifuatalo kuhusu “misaada” hiyo ya nchi za Kiafrika:

    “You normally hear that Western governments are aiding Africa. The truth is that Africa is aiding the Western countries. Africans are the donors. How do they donate? How does Uganda donate to Britain, for instance? When you sell a kilo of coffee in Uganda, we’ll get $1 per kilo when we sell bean coffee and process the beans—coffee beans. The same kilogram, when it is processed, it goes for about 10 or $11 or 12 or even more. Therefore, in every kilogram of coffee, Uganda is donating $9 to Britain. (Laughter.) That is the situation for cotton, situation for all raw materials.”

    Linganisha jibu hilo la Museveni na yale aliyosema Rais Robert Gabriel Mugabe, “Give us a break, defiant Mugabe tells the West”, kama ilivyoandikwa kwenye gazeti la Nation, Kenya, la Alhamisi tarehe 21 Mei, 2007, wakati wa kufungua Mkutano wa 12 wa Viongozi wa Nchi za COMESA, ambapo alichaguliwa Makamu wa Rais.

    Dr. Mugabe aliitaka Afrika ibadilike isiwe tu wazalishaji wa mali ghafi tu bali pia wasindikaji wa mazao yetu ili kuyapatia bei ya juu:

    “Prices paid by us are fixed by others upon valuation by others. They are the great ones and we are the small ones…I have been wanting to know which part of Britain tea is grown and up to now I have not found it. Nobody ever recognises us for that although the products play a great role in economy where they are sold…”

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 31, 2007

    Hey anoy unayetaka adrress nikienda Hoboken nitaangalia. Lakini wao hawauzi zile zilizopakiwa kama za bongo. Wao wanaparckage zao nzuri tu. Na mimi naendaga huko mara kwa mara kwa vile wanavyopark ni ready to give as a gift. Wameweka label ya duka lao na jina la nchi ilikotoka. Ila chai yao kutoka TZ ni nzuri sana sasa sijui wanaadd something.

    Niliwaulizaga wakasema wanaendaga kwenye hizo nchi twice a year minimum kununua wenyewe. Sasa sijui kweli kwa vile wana aina nyingi kutoka kila sehemu za ulimwenguni zinazotoa kahawa na sio TZ yenyewe.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 31, 2007

    Hey labda wStarbucks waliintroduce kwenye Starbucks nyingine na nyingine ndio wameadd. Mimi kituo changu cha train kuna moja kwa hiyo pretty much kila asubuhi naingia kuchukua kahawa lakini walikua hawana. Ndio nimeanza kuiona hivi karibuni pia.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 31, 2007

    Kwa kifupi hii ni mara ya kwanza kwa Starbucks kuweka kahawa hii kutoka bongo na wameiweka marekani nzima kama kahawa ya mwezi.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 31, 2007

    Nimefaidi sana michango yenu ya mawazo.

    Nilisema naomba TRADEMARK au LABEL za bidhaa hizo. Kimsingi mikataba mingi ya biashara za kimataifa inalinda zaidi label kuliko bidhaa yenyewe. Kwa mfano neno Mc Donald linalindwa kuliko maandazi milioni kumi yanayopikwa kila siku kote duniani.

    Watanzania tunahitaji kutumia mikataba hii kuwa na label za kitaifa. Ni rahisi kutumia mashirika yasiyo ya kiserikali kuwaambia ukinunua kahawa yenye lable fulani una ISAIDIA TZ moja kwa moja na ukinunua yenye label fulani UNASAIDIA UNYONYAJI. Ethiopia wameweza sisi tunashindwa nini?

    Hata tukiishiwa kahawa, nembo yetu itaendelea kuwa mali na tunaweza kuikodisha "licencing" kwa watu wengine.

    Hili lilishindikana kwa swala la Tanzanite kutokana na RUSHWA. Watu tulipiga kelele weeee, andika kwenye magazeti hakuna anaye sikia. Sasa watu wana laumu Kenya kupata zawadi ya Tanzanite wakati haizalishi . Isipate vipi? Kwani Tanzanite yenu ina alama?

    Kuna anon amesema kuwa hatumii kahawa ila alipo ona TANZANIA akaamua kununua. THATS IT!!! A trademark is a property!! Ndiyo Intellectual Property yenyewe tunayoizungumzia. Coca Cola, Mc Donald, Toyota...you name it! Hata katika mavazi, bei ya nguo haitokani na ubora inatokana na CHATA!!

    Kwanini nasisi tusiwe na chata yetu ya kahawa na ya chai na ya Tanzanite?? Ni rahisi sana kitangazia dunia kuwa our official trademark is...na wakatii bila shida!

    Tusaidiane: analystmunge@yahoo.com

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 01, 2007

    Siyo Kweli, nimeiona hii miaka mitatu iliyopita hapa Marekani.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 01, 2007

    Hawa watu wa huku wanafanya biashara zao kufuata Demographic Geography. Kuna miji mingine wataiweka as a flavor of the month ikiisha tu wataiondoa na kutouza tena kabisa kwa vile hamna mnunuzi. Kam mnasema ni flavor of the month mimi nimeona mifuko sio zaidi ya mitano tu sasa sijui imenunuliwa kwa wingi au ????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...