naam, kama wadau wengi walivyoshauri, mambo ya flaviana yameisha sasa tuhamie taifa staaz inayocheza na senego jumamosi hii uwanja wa ccm kirumba, mwanza. hapo unamwona kocha wetu mbrazil marcio maximo akiingia uwanja wa karume ambapo amepageuza kuwa kituo kikuu cha mafunzo kwa timu ya taifa. kila siku asubuhi na jioni anawafua kisawasawa tayari tayari kwa mtanange ambao hata jk atahudhuria. bahati mbaya hii haina kupiga kura kama kwa flaviana. dakika 90 ndio zitaamua. hivyo tuelekezeni dua zetu kwa staaz...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2007

    Huu moyo wa kuendeleza soka wa JK wakishirikiana na huyu bwana ungekuwepo enzi za zamani wakati Tanzania ilikuwa na vipaji halisi naamini TZ tungekuwa mbali sana na mchezo wa soka. Tatizo siku hizi vijana wamejaa ubishoo hakuna uzalendo.

    GAZ

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 30, 2007

    Tatizo vijana wakishapata vi-corolla wanajisahau kabisa. Wanajua ndio wameshayaweka maisha kwenye mstari.Anyway tunahitaji kuwasupport nakuwa watanzania.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 30, 2007

    Big up Stars. Jamani tushangilie timu yetu kwa nguvu moja na tutashinda tu. Iweje kila timu inapocheza kwao hushinda iwe sisi wa kufungwa? Ukiangalia matokeo mengi mwenyeji hushinda. Ni pale tu makosa ya kutojiamini kwa wachezaji na maandalizi duni ya chama cha soka ndio hukosesha ushindi nyumbani. Shime TFF zibeni ufa unaojitokeza kati yenu na benchi la Ufundi. Wapeni makocha (Maximo na wenzake) msaada wa hamasa ili wafanye kazi yao kwa ufanisi. TFF iunde baraza la ushauri wa kiufundi likijumuisha wachezaji na makocha wakongwe ili waweze kushauri pale inapohitajika. Shime safari imeanza, tusibabaishwe na matokeo. Big up Stars. Big up Michuzi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 30, 2007

    Huyo Bwana ni m-babbaishaji tu huyo, na hao anaowafundisha bahati mbaya ni untrainable-hawafundishiki.
    Kichapo kinawasubiri tu hao!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 30, 2007

    wewe Perez inaonekana ni kocha hasa, je CV yako ikoje?Umefundisha timu gani inayojulikana?Watu wengine bwana makelele tu ya kusagia wenzao huku wao hawajui kitu

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 31, 2007

    Tatizo la soka la bongo sio mwalimu, ukweli ni kwamba hakuna mfumo bora wa kuendeleza mpira wa miguu. Mwalimu wa kiwango cha Maximo hatakiwi kufundisha watu kupiga pasi au kutuliza mpira yeye anatakiwa kutengeneza coordination tu. Amka serikali, amka TFF, start from the grass roots!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 01, 2007

    kila la kheri Taifa Stars, we pray to win 2 nil, we still have chance... its football... kama senegal waliweza kuwafunga France katika world cup ni wazi na Tanzania tunaweza kuwafunga senegal, kinachotakikana nikujiamini na kucheza mpira wa kasi, we are at home... mungu ibariki Tanzania. we love football & we love Tanzania

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 01, 2007

    Kuyu jamaa kweli anajituma na kuipenda timu ila, namuonea huruma sana very soon atatimua kwani hana timu kabisa yaani ingekuwa inaruhusiwa naona angekuja na wabrazil kuwafundishia huku wakawa stars tungefika mbali.

    Ila tumuombee mungu jamaa wabahatishe kesho maana, wachezaji wetu wasanii sana na hawafundishiki, kweni wengi hawana vision wakiisha fika simba au yanga wamemaliza na kubweteka, badala ya ku focus Europe kwenye mpira wa bingo. Matokeo yake wanakuwa hawajibiishi, kwani wakisha kuwa yanga au simba, watapata wasichana wazuri na saloon cars za mill 2 wameridhika. Kama kweli wana-vision huu ndio wakati wa kutoka sasa, wakifika Ghana Vigogo wa soka duniani watawaona ila sio Simba na Yanga kuchezea uwanja wa manumbu....

    Aaa basi niishie hapo kweli jamaa wanaudhi sana hawampi support mzee maximo ''MUNGU IBARIKI TANZANIa, KESHO HAWA JAMAA WAONE MWEZI''

    NA WAGANGA WOTE WA KESHO WAWE UWANJANI NA MAJINI YAO, MAANA HUU NDIO MPIRA WA BONGO, MTU AKISHANYWESHWA DAMU YA NJIWA NA KUPAKWA MAFUTA YA MAMBA BASI HAKAZI MAKALIO KWENYE MECHI ANADHANI NDIO BASI. ''ACHENI KUTEGEMEA VOODO'' CHEZENI KESHO MPIRA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...