rais wa shirikisho la soka leodegar tenga akipongezana na bosi wa vodacom baada ya kutiliana saini ya mkataba wa udhamini wa ligi kuu inayoanza jumamosi hii wa bilioni 4 kwa miaka mitano ijayo.


leo tff limetoa mchanganuo wa udhamini huo ambapo kila mwaka italamba milioni 720.


katibu mkuu frederick mwakalebela kasema leo kwamba usafiri wa timu utagharimu 233,746,834/- ama asilimia 33, malipo ya waamuzi na makamisaa itakuwa 96,792,731/- ambayo ni asilimia 13, gharama za shughuli za tff zitakuwa 112,099,949/- ama asilimia 16 wakati zawadi zitagharimu 79,100,000/- (11%) na vifaa itakuwa 200,000,000/- (28%) ambapo jumla ni 718,739,514/- (100%).
mshindi wa kwanza atalamba milioni 56, mfungaji bora (milioni 2), kipa bora (milioni 1unusu), timu yenye nidhamu (milioni 5), mchezaji bora wa mwezi (laki 6 kila mwezi), mwamuzi bora (milioni 2 unusu) na mwalimu bora (milioni 2unusu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Jamani naomba nielimishwa, mbona sijaona fungu la wachezaji? hizi pesa sizimetolewa kwa niaba ya hawa wanaoinga uwanjani? Au ndo kama kawaida bongo yetu!!

    ReplyDelete
  2. We anon hapo juu, mdhamini hatoi fedha kwa wachezaji, anaziwezesha klabu ziweze kushiriki ligi kwa urahisi zaidi(anapunguza gharama za ushiriki). Wachezaji ni waajiriwa wa Klabu kwa maana hiyo ni Vilabu ndivyo vyenye jukumu la kushughulikia maslahi ya wachezaji. UMEELEWA AU BADO?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...