mwaka jana richa aliwakilisha bongo kwenye miss earth, na hakuna aliyetia neno....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. kaka misoup huyu msichana ni mrenbo sana na sioni kwanini asiwakilishe Tanzania wakati ni Mtanzania jamani watanzania wenzangu tuache mizengwe Colour doesnt matter so long as she was born and raised in Tanzania, as far as am concern she is Tanzanian, As a female black Tanzanian living abroad(England) where people are not jurged by the colour of their skin then i believe we should give our Richa a chance to represent our National flag, for God's sake tuko kwenye karne ya science & technology-PEACE

    ReplyDelete
  2. Kweli ka Richa ni kazuri kwa mambo fulani. We angalia hapo kunako, nadhani utathaminisha na wewe mbaguzi!!!

    ReplyDelete
  3. RICHA IS BEAUTIFUL, FULL STOP!

    ReplyDelete
  4. Miss Earth nani anayeijua? Ndio maana hatukutia neno..Sasa miss World hapo itakuwa mbwendebo..Ila anaonekana mmhh ...hebu naomba email yake

    ReplyDelete
  5. MWEZI MTUKUFU MWEZI WA TOBA.

    ReplyDelete
  6. KOKORIKOOOO!!
    Hili nalo waulizwe hao waandaaji wa haya mashindano hivi MISI DUNIA sasa anahusikanaje na kuwa nusu uchi au nusu uvaaji? ningefurahi sana angetafutwa dada shujaa zaidi aliyeteitetea DUNIA NA MAZINGIRA YAKE KWA NGUVU NA AKILI ZAKE ZOTE KULIKO WENGINE.
    Jina la Sanaa ya kutuletea Taswira za Mabinti namna hii iwe ni ya kumtafuta MISS SEMI-STRIPTEASE!!

    Mataifa tunayopinga ukoloni wa kuhusianisha uzuri wa mabinti na kuwavua nguo adharani tuamke sasa, vinginevyo kujadili na kujishebedua eti tuna hasira na wanawake wanaovaa vi micro pico-pico mini-skirts na vitop mjinjo ni UNAFIKI MKUBWA. Maana hata mke wa rais ndiye anakwenda kuwafunda watoto wa watu kujiandaa kuja wakiwa nusu utupu halafu maelfu kwa mamia tunatinga VIP na kwingineko kula chabo tukio linalofafana na mtemi Mswati-wa Infinitive, kasoro tu ni kuwa, Lundenga yeye nadhani haendi nao kwake!
    Ni nani aliyesema kuwa uzuri wa mwanamke ni mpaka abaki na chupi?? kwa nini sasa wasivue na hiyo kabisa?? Where are you TAMWA na mtandao wa kulinda haki za jinsia?
    Mimi nitamwambia binti wangu sasa awe anatembea na chupi tu na sindiria iliyokatwa kidogo kuanzia makoko hadi mkendo street hadi mkwakwani hadi Kariakoo Dar na mtu aje amguse aone nitakavyomshughulikia kisheria kwa kosa la kumzuia Miss mtarajiwa akiwa MAZOEZINI.

    SIPENDI KUTAWALIWA TENA MIMI NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO

    ReplyDelete
  7. Jamani huyu mtoto mzuri sana wabongo semeni mnavyotaka mali safi na ni mbongo kulaleki

    ReplyDelete
  8. WATANZANIA TUKUMBUKE MIAKA YA 90 TULIKUWA NA MISS TZ MGIRIKI KWAJINA EMIL ADOLF KUTOKA DODOMA HAKUNA ALIEOSHA KINYWA

    ReplyDelete
  9. mbona anafanana na Sheru? lakini kabinti kazuri kweli kweli, Tanil akahonge kazi Shiva basi

    ReplyDelete
  10. majita uko wapi? au comments zako zimeminywa???
    Duu huyo yakatakule naye ni mchambuzi wa shoka

    ReplyDelete
  11. Wewe (Anonymous wa Tarehe September 21, 2007 3:38:00 AM EAT, ) unaweza ukawa sio muelewa mzuri wa haya mashindano. Hakuna mtu anaye lazimishwa kuvaa chupi unaambiwa uvae vazi la ufukweni. Sasa kama wewe kwenu huwa unavaa vitenge au suti ukiwa ufukweni hakuna mtu atakaye kushangaa kwani ndio utamaduniwenu. Watu wanao vaa vichupi wakiwa ufukweni ndio wanao vaa hivyo kwenye mashindano na ndio maana kuna kuwa na mavazi ya jioni pia. Je wewe ukitoka jioni kwenda kwenye shufhuli au hafla unavaa traksuti?
    tuwe waungawana sio mnato malalamiko bila kujua Mchezo wenyewe.

    Huyo dada nimzuri kama vigezo vimetimia anahaki acheni ubaguzi, mbona amkuhoji Azzim Dewji wa simba au muhammed kwenye kamati ya ushindi ya Taifa star acheni hizo.

    Dada kamua tu umesimama kweli.

    ReplyDelete
  12. Richa hoyeeeee!
    Jamani Richa ni mrembo! wacha tuseme tu ukweli wa kile tunachokiona hapa!

    Richa uko wapiiii?? Njoo useme ahsante hapa watu wamekukubali sasa. Come on Richa,say thanks.!!!

    ReplyDelete
  13. Hivi wengi mnachonga tu kuhusu Richa sio Mtanzania wakati hata alama ya ndui anayo mkononi, kwani mlivyokubali Jack ntuyabaliwe (Kinyana Ntuyabaliwe aka Klyin) atuwakilishe miss world mlifikiri ni Mtanzania? hana Utanzania hata chembe, ni Mrundi sijui na mjerumani (not sure mzungu wa nchi lakini ni mzungu). Huyo Emily adolph yeye ni mgiriki na mzazi wake mmoja ni Mtanzania kwa hiyo powa tu kutuwakilisha.

    ReplyDelete
  14. Wabongo bwana! Mpaka tuonyeshwe vitu vya ndani ndio tukubali kwamba Richa ni mzuri. Haya mbona leo sioni yale maneno ya kashfa!! Wote mmekimbilia bafuni nyooo!! Mtoto huyu ni mzuri milazima nioe!

    ReplyDelete
  15. Mtoto ni mzuriii sana chichemi tena.ni mimi,
    majita

    ReplyDelete
  16. Miss earth ni biashara binafsi kama vile wewe ukianzisha miss michuzi, Miss TZ ni national icon kwa hiyo isiletewe masihara ya rushwa kama mwaka huu. huyu si mtanzania ni mhindi michuzi huelewi nini??

    ReplyDelete
  17. Richa....Richa....tobaaaaaaa swaumu yangu imeshaharibika tena....mamaaaaa weeeeeee...mtoto bomba sana....kulaleki huyu ni MTZ halisi....semeni mpaka mchoke! Richa...contact me please! LOL!

    ReplyDelete
  18. Jamani Flaviana ni mzuri.Tuseme ukweli,awe na nywele ndefu au kipara yuko pale pale.Natumaini atasogea mbele na kuwa super model wa ngazi za Ms Naomi Campbell au Alek Wek wa Sudan.Maana anawakilisha Tanzania vyema,100%.

    ReplyDelete
  19. Wale waliokuwa wanatoa maneno ya kibaguzi leo wote wanaongelea kichupi tu...any way ndiyo matatizo ya blog haya, tusonge mbele maana hata wendawazimu huingia kwenye blog na kuchangia.

    ReplyDelete
  20. TOAAAA, TOAAAAA, WEWEEEE, WEWEEE, PSYUUUUUU, PSYUUUUU, PSYUUUU, TOAAAA, TOAAAAA, NINI WEWEEEE, NINI WEWEE, TOAAAA, TOAAA UCHAFU HUOOOO.
    (HAPO UMEINGIA KWENYE JUMBA LA SINEMA LA MAGUNIA HALAFU MNAWEKEA PICHA MBOVU. SI KELELE NA MILUZI HIYO)

    ReplyDelete
  21. nobody is saying kwamba huyu binti sio mzuri. ni mzuri sana ila anatakiwa kuwa miss india au miss 'tanzania immigrants'...sioni kama anawakilisha uzuri wa msichana wa kitanzania (wa kibantu). thats just my opinion.

    ReplyDelete
  22. kwa jinsi nilivyosoma comment hapo juu,ni jinsi gani inavyoonyesha wabongo walivyo wanafiki,shame on yall.

    ReplyDelete
  23. ...i assume haya mambo ya umisi kuna ka element ka UTAMADUNI...kama ni hivyo, sioni tatizo la ushiriki wa MISS EARTH...lakini hii MISS TZ ndio inayonitatiza...TZ ina ASILI, shule tulifundishwa NGOMA ZA ASILI, mila na utamaduni and so forth...in order to PRESERVE these, pamoja na IDENTITY yetu, huyu mwakilishi nionavyo mimi HATUFAI kwa mtazamo wa mila, asili, identity yetu na utamaduni wetu...TZ iwakilishwe na MBANTU...kwani huyu anafit zaidi wapi, akicheza nachi au akicheza LIZOMBE?

    ReplyDelete
  24. kuna baadhi ya mambo YANAPENDEZA zaidi yakiachwa kama yalivyo...mmasai akicheza SINDIMBA itakuwa analazimisha, mchaga akicheza GOMBESUGU itakuwa ze comedy, mgogo akicheza ngoma ya wameru sijui itakuwaje...matokeo yake ndio ile taarab ya JKT kuna kabinti ka kigogo kweli kalikuwa na sauti nzuri but wagogo taarab siyo zao wakatuimbia "ewe njiwa ewe njiwa PEREKA SARAMUU"...nachosema hapa uwakilishi wa mambo ya utamaduni na identity ni vema waachiwe wahusika, inakuwa hakuna kulazimisha...ni maoni tu i am not inflicting my idea to anyone

    ReplyDelete
  25. TUHUMA
    Michuzi umebania maoni yangu mara mbili zote.Na sasa umekuja na mpya kwani umeandika maoni hapo juu na ku-sign jina langu "Majita" Wajameni hayo Maoni ..."Mtoto ni mzuri chichemi tena .."SIYO ya kwangu.Mimi sijawahi kuwa mnafiki.Nasema hivi mimi na miss.Patel hatupikwi chungu kimoja.So ananikerea tu humu kjijini.
    Majita

    ReplyDelete
  26. She's Beautiful...Nomatter what!!

    ReplyDelete
  27. yaani majita kweli chungu cha pateli sikuoni.waambie hao hata MSUFINI hakuna chungu cha patelli.

    ReplyDelete
  28. WE MWANADAMU WA 21/9 12:15
    UNAYEJIDAI KUSOMESHA WATU JUU YA MASHINDANO HAYA NA KUHUSU VAZI LA UFUKWENI HUJANISOMA VEMA KUHUSU CHANGAMOTO YA UNUSU UCHI. KWA HIYO KAMA NI HIVYO KWA MAELEZO YAKO VAZI LA HUYU 'MTANZANIA ASILIA'LA KWENDA UFUKWENI NI CHUPI???? NDO MAANA WATU WANASEMA SI MTANZANIA BASI MAANA WATAZANIA HATA HUJIFUNIKA KAKANGA HIVI!
    USITAKE KUTETEA VITU KAMA HUJUI KINAELEZWA HAPA.

    PILI TUNAPOLETEWA PICHA HII SASA JE KUSUDI KUONYESHA VAZI LA UFUKWENI AU NI KUMTANGAZA.
    JE KULIKUWA NA ULAZIMA KUJITANGANZA KWA KACHUPI?? MBONA SIKU HIYO ALIVAA MAVAZI MENGI AMBAYO YALIWAVUTIA WATU ZAIDI LA HILO?

    TATU KAMA SUALA NI KUONYESHA VAZI LA UFUKWENI BASI MTU ATAINGIA NA VAZI HILO AMENINGÍNIZA KWENYE 'HANGER'!!
    MPAKA KESHO, SUALA LA MJADALA WA KUONYESHA VICHUPI AU VIKANGA AU VIKOI N.K NI DEBATABLE KATIKA ANGA ZA JUU ZA MEDANI YA FANI HII. FANYA ASSIGNMENT ZAKO KATIKA BEAUTY PAGEANT STATS NA KATIKA ACADEMIC PAPERS WALIZOANDIKA WENZAKO WANADHUONI JUU YA SUALA HILO KABLA YA KUKURUPUKA NA KUFIKIRI KUWA NI ISSUE YA USHAMBA AU ETI MTU KUTOJUA MASHINDANO HAYA. HII NI FANI NA NI TAALUMA THAT WILL CONTINUE TO BE SHAPED TO UNCOVER UNNECESSARY BURDENS! HATA SUALA LA WEMBAMBA LINAJADILIWA SANA NA MPAKA SASA AKINA DADA ZETU WAMESHAONYWA KUWA WALE WANAOPEPESUKA NA UPEPO WATATUPWA NJE!! NA BADO USIFIKIRI MCHEZO; SWALI ZA MZURI NI NANI LAZIMA LIWE TOFAUTI NA SUALI ZA NANI AMEVAA AU AMETENGENEZA VAZI ZURI UPO HAPOO WEWE MSHAMBA.
    NITAJIE CHUO CHAKO NIJE NIWAPE WALAU VIONJO VYA ADV. LECTURE OF MA. DEGREE IN MODELING, PEGEANTOPOLIS & MISSOSOLOGY (Hakuna cha bure Lundenga awalipie fee!) .

    HAKUNA UBISHI KWAMBA MASHINDANO HAYA BADO YANA CHECHE ZA UKOLONI NA AU UTAMADUNI WA SEHEMU FULANI ZAIDI KULIKO WENGINE.
    DID YOU KNOW THAT MISS WORLD STARTED AS THE FESTIVAL BIKINI CONTESTS & THAT MISS WORLD CHAIRPERSON JULIA MORLEY SCRAPPED THE SWIMSUIT COMPETITION FROM THE FINALS IN 1998 AND SHE SAID THAT BEACH WEARS MUST BE WON ON BEACHES ONLY?
    NDUGU YANGU ACHA UJUVI MWOLOLO WA KUWAFIKIRI WADAU WA HII BLOGU ETI WOTE NI WASHAMBA AU KWAMBA HATUJUI TUNACHOANDIKA, UKILETA HAKO KASOMO KA BIKINI SCIENCE, G-STRINGOLOGY HATA WET -TSHIRT COMPETITIONS MBONA UTAKESHA HAPA MAANA HAPO UTATAKIWA UNIVUE 'Doctoraal' YANGU!!

    NAKWAMBIA KUWA BADO YAKO MASWALI MENGI SANA JUU YA VIGEZO VYA KUMPATA MISS WORLD NA SASA TUNATAFUTA KUFUTA HIYO BEACH BEAUTY MAANA WENGINE TUNADAI IWEPO NA KITCHEN BEAUTY NA FARM BEAUTY N.K. KAMA SOMO HILI BADO HALIJAKUKUNA BASI KAULIZE KWA NINI HATA TZ PALIANZISHWA MISS BANTU??

    HUWEZI KULAZIMISHA WATU WOTE KUKENUA MENO WAKATI MIFUPA ISIYO NA NYAMA INASUGUANA KAMA VILE HAINA MAFUTA MLAINISHO!! BINTI MREMBO KWA WENGINE NI YULE AMBAYE UKIMWANGA MAJI MGONGONI LAZIMA YATUAME KIDOGO NA SIO KUPITILIZA AU KWA MAELEZO MENGINE KIMWANA NI YULE MWENYE SIFA YA KUMBEBA MTOTO MGONGONI HATA BILA MBELEKO!

    Kaka Michu tafadhali rusha hili gazeti langu likiwa ni somo la III kwa waosha toka kwangu mimi,
    Nyakatakule unyilisya echalo

    ReplyDelete
  29. Annonymous wa Sept/22/'07,12:00am amesema yote,ninakubaliana nawe moja kwa moja.
    Hao majaji wa hii contest wanatakiwa wakaelimishwe maana nafikiri hawajui wanachofanya zaidi ya KULA!!

    ReplyDelete
  30. wacheni ubaguzi. Richa is Tanzanian na so are wazazi wake.
    Wazalendo kama mimi na wewe.
    So no nonsense ' tanzanian immigrant'.
    Jamm Mnanikorofisha. Nchi yetu Tanzania is not a tribal country kama wajirani wetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...