jk akiwa na Askofu mkuu wa kanisa la Orthodox Tanzania Jeronymos Muzeeyi muda mfupi baada ya Rais kuweka jiwe la msingi katika hospitali hiyo huko Kitendaguro,katika manispaa ya Bukoba, inayojengwa na kanisa hilo eneo la Kitendaguro katika manispaa ya Bukoba jana mchana.

Akizungumza wakati hafla hiyo Rais aliushukuru uongozi wa kanisa hilo kwa uamuzi wa kujenga hospitali hiyo Bukoba akisema kuwa itakapokamilika itawapunguzia wakazi wa mji wa Bukoba na maeneo mengine mkoani Kagera adha ya kwenda hospitali ya Rufaa Bugando kwa matibabu ya magonjwa makubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Haiusiani na Hii hapo juu.

    Ukweli kuna jamaa flani wafanyakazi wa CRDB hapa Arusha Branch, Njia panda ya unga limited kweli wameniboa sana.

    eti mi nlikua nataka nijisajili NBAA kwa kulipia kwanza registration Fee ili nipewe hiyo namba,
    Wao benki wang'ang'ania lazima niwe na hiyo namba kwanza ndio nilipie, ntakua nayo vipi bila kulipia kwanza na kukubaliwa??!!!.

    nimejaribu kuwaelewesha kua namba sina, mpaka nikilipia nikakubaliwa ndo nitapata lakin hawakuelewa kabisa na kung'ang'ania kutonisajili.

    nimeenda mpaka kwa Customer services Manager wao aitwae David kwa mshangao nae bila hata ya aibu akakubaliana na teller wake.

    lakin nimeenda mapato house branch wamekubali bila kipingamizi chochote,

    Sasa kwa kumuonyesha alikua wrong nimempelekea slip nilizolipia nazo mapato ili azione akabaki anatoa macho tu, hana la kusema.

    Mtu kama hujui kitu si useme tu, kuliko kurudisha wateja kwa kitu usicho na uhakika nacho tu.

    Samahani kwa kuingizia hii topic

    ReplyDelete
  2. Namwona Mzee wa Tour vasco da gama kwa sasa anapiga ndogo ndogo za nyumbani(BK) kabla hajaanza za masafa huko ughaibuni..sijui lini atarudi kwa Ikulu kumaliza matatizo ya MAFISADI..zis time tumepata rais mpenda safari..

    ReplyDelete
  3. HIvi Orthodox huwa ni kitu gani hasa? Maana huwa sielewi kabisa! Israel kuna watu wanaitwa wa-orthodox na wengine wako East Europe. Kwa anayejua anisaidie kuelewaa. Kwa anayejua tu tafdhali.

    ReplyDelete
  4. Orthodox means correct teachings in Greek. Kuna Jewish Orthodox na pia kuna Christian Orthodox.

    Sikujua kuwa hilo dhehebu lipo bongo.

    Na nilikua sijui habari zao mpaka siku ya mazishi ya John Paul the second ndio nikagoogle kujua more about them. Sijui walikua Orthdox Roman Catholic walivaa hivyo hiyo. Ila wanavyosali kama wajewish.

    Naona walianzia Greece

    ReplyDelete
  5. Hizo nguo nyeusi na hilo joto la bongo inakuwaje?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...