mdau assah mwambene wawizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa katuletea snepu hii ya jk akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa bernard membe wakiwa katika mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika (AU) jana Mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo muda mfupi kabla jk hajachaguliwa kuwa mwenyekiti wa AU. Habari kamili soma chini.

RAIS Jakaya Kikwete amechaguliwa kwa kauli moja na wakuu wa Umoja wa Afrika (AU) kuwa Mwenyekiti mpya wa umoja huo kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao.

Baada tu ya kukabidhiwa wadhifa huo, Rais Kikwete alisema kazi kubwa ya umoja huo ni kuhakikisha inaondokana na jinamizi la kuonekana kazi yake kubwa ni kushughulikia migogoro ya kisiasa badala ya maendeleo.

Wakati wakuu wa nchi hizo walipokutana jioni baada ya mapumziko ya mchana mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Rais John Kufour wa Ghana, alimwita Balozi wa Misri katika Umoja huo, Balozi Khalid na kumtaka kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.

Balozi Khalid kwa lugha ya Kiarabu, alisema baada ya mashauriano na mabalozi wa nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao katika umoja huo, wamekubaliana kwa kauli moja kuwa Mwenyekiti wa Umoja huo atakuwa Tanzania, kwa maana ya Rais Kikwete; kisha akatangaza wasaidizi wake kuwa watatoka Libya, Lesotho na Cameroon kwa mgawanyo wa kikanda, yaani Kaskazini, Kusini na Kati.

Baada ya hapo, Rais Kufour alimwita kwenye meza kuu Rais Kikwete ambaye aliondoka kwenye kiti chake alichokuwa amekaa na kwenda meza kuu kuungana na viongozi wengine, kabla ya Rais wa Ghana kumkabidhi kirungu kama ishara ya uenyekiti huo.

Nchi nyingine zilizowahi kuwa Mwenyekiti wa AU tangu ilipoanzishwa mwaka 2002 ni Afrika Kusini (Julai 2002 hadi Julai 2003), Msumbiji (Julai 2003 hadi Julai 2004), Nigeria (Julai 2004 hadi Januari 2006), na Congo Brazzaville.

Rais Kikwete aliyeingia ukumbini jioni akiongoza wakuu wengine wa nchi akifuatana na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika, Alpha Oumar Konare, akizungumza kwa lugha ya Kiswahili baada ya kukabidhiwa madaraka hayo, alisema anaipokea nafasi hiyo kwa uenyenyekevu na akaomba ushirikiano kwa wakuu wenzake wa nchi ili kuiletea Afrika maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Sasa ndio tutamkoma kwa kusafiri kama Vasco da Gama vile !!!

    ReplyDelete
  2. Mafisadi, sasa waanza kuumbuana

    2008-01-31 15:37:37
    Na Mwandishi Wetu, Jijini


    Kama Waswahili wasemavyo kwamba Waarabu wa Pemba hujuana kwa viremba, basi ndivyo inavyotokea hivi sasa kwa wale watafunaji wa pesa za umma, almaarufu kama mafisadi.

    Kutokana na kutambuana, imeelezwa kwamba baadhi wameanza kuumbuana wao kwa wao huku wakitishiana kuanikana hadharani.

    Taarifa kutoka kwa chanzo chetu katika wizara ya Madini na Nishati zinadai vigogo kadhaa ambao awali walikuwa wakishirikiana, hivi sasa ni maji na mafuta na chanzo cha uhasama huo ni mmoja kudaiwa kumchomea utambi mwenzake.

    Imedaiwa kuwa kigogo mmoja alilikisha taarifa za mwenzake kwa mapaparazi ambao bado hawajachapisha kutokanana kuendelea kuzifanyia kazi, kitu kilichomkasirisha aliyetuhumiwa.

    ``Huyo aliyetuhumiwa inasemekana baada ya kubaini hilo, naye alianza kuwasaka waandishi ili awape data kumhusu mwenzake,`` kikaongeza chanzo hicho.

    Imedaiwa kuwa pia baadhi ya watendaji wamekuwa wakituma taarifa kibao kwenye mitandao zinazowatuhumu wenzao kwamba ni mafisadi, ingawa hawaweki majina yao wala kutaja ni wapi waliko na wana ushahidi gani wa kile wanachokisema.

    Kadhalika katika Wizara ya Fedha inadaiwa baadhi ya watendaji ambao kwa njia moja ama nyingine ndio wanawachomea utambi wenzao kutokana na kufahamu dili zao.

    ``Hakuna anayetaka kufa peke yake. Kutokana na kutoaminiana, unakuta kila mmoja anamchimba mwenzake,`` kimedai chanzo hicho.

    Imedaiwa kuwa hivi sasa katika wizara kadhaa hakuna anayemwamini mwenzake kutokana na kutofahamu nani atakuchomea utambi.

    Sakata la ufisadi lilipamba moto baada aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu kutimuliwa kazi kufuatia kubainika kwa ulaji mkubwa wa pesa za umma.

    Soo la kuwepo kwa ufisadi nchini liliibuliwa mwaka jana na Mbunge wa Karatu Dk. Wilbrod Slaa .

    ReplyDelete
  3. Tanzania inaweza nufaika sana na wakimbizi wenye taaluma toka Kenya kama Kenya ambavyo ilinufaika sana na wakimbizi wenye taaluma toka Uganda waliokimbia wakati wa Idd Amin kwenda Kenya hasa katika sekta ya Elimu.

    Kenya ilikuwa na upungufu mkubwa wa walimu kuanzia shule za msingi na sekondari.Walimu wakimbizi walipoingia Kenya nchi ya Kenya iliwaajiri kama walimu hadi maafisa elimu.Na ndio waliosaidia sana kuiweka sawa Kenya Kielimu.Raisi Museveni aliposhika madaraka alitoa amri walimu warudi haraka baada ya amani kurudi.Wakarudi wakaenda kuanzisha mashule binafsi mazuri kibao kama yale waliyosaidia kuanzisha Kenya.Kenya hadi leo watu wengi huwakumbuka walimu hao wazuri wakimbizi toka Uganda.

    Tanzania nayo isilale ichangamke iwachukue walimu iwaajiri kwenye shule za kata hizo zinazoitwa za Lowasa ambazo hazina walimu na shule zetu za binafsi chap chap.Na kama kuna wataalamu wengine wakimbizi serikali ichangamke!

    koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  4. Asante Mzee kwa kukandamiza Kiswahili!

    ReplyDelete
  5. BM: Sasa hii ya huyu jamaa kuhudhuria hapa wakati mwenzake anasema kaiba kura utawaambiaje wajumbe??
    KK: Nitauchuna tu...kwanini wenyewe wasimkataze kuja?? mambo mengine ni lawama tu zisizo na msingi..na wewe nani kakwambia mimi ndiye wa kuzungumzia hili swala?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...