mabingwa wa kombe la NSSF ambao ni wachapishaji wa magazeti ya serikali ya Daily News, Sunday News na HabariLeo, leo wameitungua timu ya Mwananchi Corporation mabao 5-4 katika mchezo ambao uliamuliwa kwa matuta baada ya waamuzi kufanya wawezalo kuiangusha 'Indomitable Lions' TSN bila mafanikio. Michuano hiyo inafanyikia uwanja wa TCC Chang'ombe.
Wakicheza watu wanane baada ya kadi nyekundu zisizo na sababu kwa wachezaji wao wawili, na makamisaa kulisakama benchi lao, TSN waliibuka kidedea na kunyamazisha kelele nyingi sana sana za Mwananchi na kuelekea nusu fainali kiulaini.
Michuano hii ya NSSF inayoshirikisha vyombo vyote vya habari katika soka na netiboli ina ushindani mkubwa na timu ikifungwa chumba chake cha habari hubaki na huzuni mwezi mzima kama bila shaka itakavyokuwa Mwananchi...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera kwa ushindi kaka Michu. sasa UK tuwe na habari bila picha na huko nako? Tuwekee Video ya mechi nzima tuone mchezo wote basi.

    ReplyDelete
  2. Sorry for off point!Hongereni sana kwa ushindi wa mechi ya leo ya kiporo ya barclays premiership naona mtanange ndio umeisha hapa Anfield wazee wa bwawa la maini watani wetu wa jadi mmekomba pointi 3 muhimu baada ya ushindi wa goli 4 kwa bila,F.torres kapiga hat-trick na Gerald kapigilia msumari wa mwisho!
    Iweke inapohusika braza michu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...