kampuni ya IPP Limited leo imetangaza kumteua Bi. Sakina Zainul Datoo (shoto) kuwa Mkurugenzi wa Uhariri wa magazeti ya IPP kuanzia April 7, 2008, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na katibu wa kampuni, Mh. Agapitus L. Nguma.

Kabla ya hapo Sakina alikuwa Mhariri mtendaji wa Sunday Citizen kwa miaka takriban mitatu na usheee, akiwa ametokea The Express ali8kofanya kazi miaka mitatu kama mhariri mkuu. Sakina pia ni mwenyekiti wa Editor's forum. globu hii inampongeza Sakina kwa mzigo huo ambao tuna imani kwamba kwa uzoefu ulionao utakabiria nao bila matatizo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Good luck and wish you all the best on your new endeavor.

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  2. HONGERA IPP HAPO MMELAMBA DUME MAMA YUKO JUU NAMTAKIA UFANISI MZURI KWENYE MAJUKUMU YAKE.

    ReplyDelete
  3. hongera mama Sakina m,mungu ataukusaidia,nakutakia kazi njema.

    ReplyDelete
  4. Hiyo kazi lawama? Kufanya kazi chini ya Mengi kunahitaji uvumilivu. Ninavyomjua mimi huyo mama, nampa miaka 2 tu. Mengi ni mmoja kati ya wale maboss ambao hawana mzaha. Akipita kazini kwa sisi tulioko chini kiwadhfa, tunashika adabu na mtu unajifanya busy. Labda ndio maana anamafanikio makubwa.

    ReplyDelete
  5. Michuzi niunganishie basi kwa AYOUB huyo hapo pembeni ya Mengi. Namzimia kishenzi. Lakini kama bado hajaoa!! Im serious o!

    ReplyDelete
  6. Congrats Ms Datoo!!

    All the best.

    ReplyDelete
  7. kaka ayub bado mseja...huenda kaka michuzi akiwahook up tunaweza anza kamati......kaka ayub wadogo zako tulisharekebisha.....tunasubiri zamu yako kaka yetu...tulishirikiana vyema kuanzia meru hall...tunasubiri kwa hamu ujiunge kwenye chama tuendeleze gurudumu la familia

    ReplyDelete
  8. Wadau mi nina mtazamo tofauti. Mengi ni mwenyekiti wa MOAT na huyu mama ni mwenyekiti wa jukwaa la wahariri, hatuoni kwamba taaluma hii inawekwa mikokononi mwa watu wachache? Nahisi kuna jambo nyuma ya pazia linaendelea. tutashuhudia mtu mmoja akiwa ni mdhibiti na mtawala wa habari nchini!!!!!!!!! Kalagabao...

    ReplyDelete
  9. Ayoub akitokea kwenye hii globu tu swala la kuoa linajitokeza...kweli kama hajaoa anasubiri nini??? achague mmoja aweke ndani..anaweza kuendelea kuchagua hadi 2038!!!!!!Na kwa jinsi anavyokuwa busy zaidi kama hivi ndivyo uwezekano wa kutooa ndivyo unavyozidi!!

    ReplyDelete
  10. CONGRATS DATOO!! YAANI KWA KWELI HUYO DADA YUKO JUU ANAIJUA KAZI YAKE HASWA. ALL THE BEST.

    ReplyDelete
  11. Mmh hii ofa haitapunguza kweli makali ya Sunday Citizen. Huyo mwanaharakati kachangia sana kulifanya hilo gazeti liwe mwiba kwa majasiri wa kifisadi na marafiki zao. Sasa akiondoka Sunday Citizen litakuwa endelevu kweli katika mapambano hayo? Au ndio mambo ya 'divide and rule',yaani, 'wagawe uwatawale'?

    ReplyDelete
  12. Nitafuatilia kwa karibu Critiques za magazeti ya IPP MEDIA nione kweli kuna SHIFT katika creative critical independent thinking Au ni MPIRA WA KI TENNIS TU?Pengine Sakina hakuwa na uwanja wa kutosha kuonyesha makeke yake akiwa ndani ya magazeti ya Mwananchi/Sunday Citizen!Tunajua jinsi magazeti ya Citizen/Mwananchi kwamba yapo pamoja na Magazeti ya Daily/Sunday Nation/East African ya Kenya.Na tunatambua vilevile kwamba magazeti hayo ya Kenya yanamilikiwa na nani,A.KH.,NA tunajua nani anamiliki magazeti ya RAI/MTANZANIA,na tunawajua wajumbe wote walioko katka Kamati Kuu(?),na tunajua mengi zaidi na zaidi.Pengine Sakina sasa utapumua kidogo.We value your contribution na tunayaelewa mazingira magumu sana ya kikazi yaliyo kuwa yakikukabili ulipokuwa na Sundays.Ningependa kukupongeza kwa dhati kwa jinsi unavyojituma na hususan kwa kutoa changamoto kwa waandishi wa habari wa kike kwamba hakuna lisilowezekana kwa mwanamke, ni utashi na dhamira tu ya kufanikiwa katika malengo uliojiwekea.We want to see more independentsia in reporting and in criques uncensored!With Mengiz and Ayoubuz around nothing is gonna stop the TRUTH from reaching its targetted Mission!Ur Welcome to the Main Street and the Gallows!

    ReplyDelete
  13. Kweli mimi daima nashangaa watu wanapomsifu huyu Sakina Datoo. mimi ni mwandishi wa habari wa siku nyingi lakini sijaona mtu anaanza kuzai ya uhariri mara baada ya kumaliza chuo. Sakina hajawahi kuwa ripota wa gazeti au redio au televisheni. Hajui namna ya kuandika habari ya polisi au mahakamani.

    Huyu ni mtu amepita vyuoni na kama uandishi sijawahi kusoma makala iliyoandikwa na yeye Sakina ambayo imefanyiwa kazi kwa kina.

    Amebakia tu kuzungumza kwenye jukwaa la wahariri ambalo wengi hatujui limetoka wapi.

    Lakini Sakina sasa amepata mahali pazuri pa kufanyia kazi kwani wengi wa wanaoajiriwa na IPP Meia kwa maoni yangu huwa wanapata kazi sio kwa sababu they can deliver, but because they know somebody in that company.

    If you want to waste time as a journalist, then join IPP Media. For those who have worked there, or are working there currently know what I mean.

    Kwangu Sakina Datoo ni bure na hawezi kuwekwa kwenye historia ya waandishi wa habari wa nchi hii. Hebu niambie ni nini cha ajabu alichokifanya zaidi ya wana taaluma vijana kama Danny Mwakiteleko, Jesse Kwayu, Kibanda, Ngurumo, Mgaya Kingoba na wengineo wengi vijana ambao japo hawavumi kwenye ma-TV, kazi zao ni bomba ile mbaya

    NAWAKILISHA

    ReplyDelete
  14. mdau wa April 4 1:50 naunga mkono comment zako. ukweli huyu Bi mkubwa sijui hata alikotokea kiuandishi wa habari. Amezuka tu mara mhariri wa Express. hili halishangazi kwa vile kule ni kwa wahindi wenziwe. hatujakaa vizuri mara mhariri wa S/Citizen, yale yale maana hili nalo linamilikiwa na H.H. AK. Hao wote wanaomsifu hapo juu wanamsifu kwa vile wanamuona tu kwenye runinga lakini ukiwaambia wataje makala moja ya nguvu dizaini ya Mbwambo, Kibanda, Rioba,Manyerere na wengineo wa caliber hiyo, watang'aa macho. unajikuta ukiuliza upeo wa watu waliomchagua kuwa sijui mwenyekiti wa sijui baraza sijui jukwaa la wahariri. anede kwanza field akaone habari zinavyotafutwa ndio mtoe sifa!

    ReplyDelete
  15. Ndugu anyo Friday, April 4, 1:50pm EAT.

    yeye kupewa cheo hicho, si ya maana kwamba ni mwandishi wa habari, pengine sifa kuu aliyokua nayo ni Management Style, na uwezo kuendesha kazi katika kitingo hicho cha umeneja.

    Naweza kukuuliza swali moja, Je Mengi mwenyewe ni mwandishi wa habari au ni mtu te mwenye fani ya biashara na uwezo kupata watu wenye akili kwa ajili ya kuendesha biashara zake, yeye kuwa na kiwanda cha soda, sio inamaanisha kwamba ametengeneza Juice alivyokua mdogo, au ana ujuzi wa kujua soda nzuri au mbaya, na vile vile kuwa na magazeti na kampuni ya IPP kwa ujumla siyo kwmba yeye ni mwana hariri.

    Jengine Je umeshawahi kusikia au kuona mwanasiasa kuwa Mkuregenzi mkuu wa kampuni ?

    ReplyDelete
  16. Ningependa kafahamisha wote mlichangia sio kwamba umahiri wa uandishi ndio uliomuka Sakina hapo .. ila ni ubunifu wake wa kuendesha mambo ya habari .. mimi namfahamu vizuri kabla hata ..Hajawa mwandishi tumefanya nae kazi DTV..SASA CHANEL TEN..,Sakina alikuwa creativity..wa mambo.mbalimbali ..nadhani hiyo ndio dhana iliyomfikisha hapo.. sasa nyie mnashangaa nin mbona wanamuziki wetu wameanza kupiga.. muziki, toka enzi hizo sifa zoa ni ndoga ukilinganisha na wanamuziki wa kizazi kipya...inachotakiwa ni ubunifu sio uzoefu..

    ReplyDelete
  17. Hebu acheni kumkomaza dada wa watu nani kwaambia Sakina ni mama au Bi mkubwa kama mnavyomuita au shungi tu hilo linawababisha..sakina bado binti mdogo tu tena mbunifu .

    ReplyDelete
  18. Hivi cheo alichopewa Datoo, ni cha utawala au cha uandishi... naomba msaada tafadhali.

    Ieleweke kuwa mtawala sio lazima una uwezo wa kuandika makala sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...