Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa akiangalia moja ya nyumba zilizoanguka katika mji mdogo wa Mto wa Mbu mkoani Arusha. Mh. Lowassa, alitoa msaada wa fedha taslimu sh milioni 3, blanketi 200 na bati 77 kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Mihela ya richmond hiyo ungetoa milioni kumi kabisa,,,safisha jina baba kazi unayo.
    kyekue

    ReplyDelete
  2. Mambo yako safi lowasa hongera kwa moyo wako wa kizalendao sasa nimeamini .Naamini sasa utakuwa na muda mzuri wakufanya kazi na wapiga kura wako baada ya kuwa bize kwa mambo ya nchi takribani 20na ushee Ibelive in you DADY

    ReplyDelete
  3. hata siku moja haitoshi. Million tatu? eti mablanket mia mbili! arudishe zote alizopata richmond kwa wananchi.
    karumekenge.

    ReplyDelete
  4. ni mfano mzuri kuwasaidia wenzetu waliofikwa na maafa kwa wale wenye uwezo jitokezeni kwa wingi ili muwasaide wenzetu waliofikwa na matatizo kama haya sio viongozi tu hata wafanya biashara na watu wenye uwezo.

    ReplyDelete
  5. endelea baba,tusahau yaliyopita.

    ReplyDelete
  6. MAALIM ISSA TUNASHUKURU KWA PICHA.."..NAKSHI.." KAMA HII NAONA MHESHIMIWA LOWASSA YUKO "..HURU.." ANATUMIKIA WANAICHI...KUMRADHI JAMANI.."..ZIMWI LIKUJUALO HALIKULI LIKAKUMALIZA.."

    ReplyDelete
  7. Waziri azomewa na wasomi

    2008-03-17 08:55:43
    Na Juma Ng\'oko, PST, Mwanza


    Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Lawrence Masha, ameonja joto ya jiwe baada ya kuzomewa na baadhi ya wahadhiri pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) cha jijini Mwanza.

    Alizomewa baada ya kujikanganya kuitetea serikali kufuatia hoja iliyotolewa na mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) Bw. Zitto Kabwe, iliyozungumzia usiri kwenye mikataba ya madini na namna ambavyo wananchi hawafahamu juu ya ukweli wa madini yao.

    Mada iliyowasilishwa na Bw. Kabwe ilielezea mafanikio pamoja na matatizo mbalimbali yanayoikabili sekta ya uchimbaji madini.

    Bw. Kabwe tofauti na Waziri Masha, aliingia ukumbini saa 6:41 mchana na kushangiliwa, alisema pamoja na mapungufu mengine serikali haiko wazi katika kutoa taarifa zinazohusu pato wala mikataba ya madini.

    Waziri Masha alizomewa hadharani kwenye mjadala aliposema serikali iko wazi katika kutangaza masuala mbalimbali yahusuyo madini.

    Alisema Watanzania wasioelewa kuhusiana na mikataba hiyo ya madini ni wale wenye uelewa mdogo na ama hawasomi magazeti au hawasikilizi redio.

    Alitoa maelezo kwenye kongamano ambalo alikuwa mgeni rasmi lililoandaliwa na SAUT ambapo pamoja na mambo mengine, alishiriki kwenye mdahalo kuhusu uimarishwaji sera ya madini, kilimo na uvuvi kuelekea katika uboreshaji wa mali asili nchini.

    ``Kama nilivyotangulia kusema, Mheshimiwa Kabwe ni rafiki yangu. Ila ninachotaka kusema ni kwamba siyo kweli kwamba watu hawasomi magazeti na hawasikilizi redio wakati serikali inapokuwa inatangaza masuala mbalimbali yanayohusu mikataba,`` alisema Bw. Masha na kuanza kuzomewa.

    PST ilikuwepo na ilishuhudia Bw. Masha akizomewa mchana saa 7:52 wakati akijaribu kufafanua mada hiyo.

    Mbunge huyo alisema kuwa karibu Watanzania wote wanaamini kwamba pato la taifa kutokana na sekta ya madini ni asilimia tatu kwa mwaka lakini bila kuwa na ufafanuzi wowote.

    Bw.Kabwe ambaye pia alikuwa mgeni mwalikwa kwenye mdahalo huo alisema kuwa hali hiyo imesababisha wananchi washindwe kuamini kwamba taifa linafaidika na sekta ya madini, kwa vile mikataba na pato litokanalo na madini ni siri ya viongozi wa juu serikalini pamoja na wawekezaji wenyewe.

    Alisema wananchi wanaoishi jirani na migodi hiyo hawafaidiki na madini hayo na kwamba wengi wao wanaishi chini ya pato la Sh. 1,000 kwa siku.

    Alitoa mfano kwamba tafiti zinaonesha kwamba Wilaya ya Geita mkoani humu, ndiyo ilikuwa ya mwisho mwaka 2005 kwa umasikini wa kipato kitaifa.

    `` Kwa mfano, takwimu zinaonyesha kwamba mwaka 2005 Geita ndiyo ilikuwa wilaya ya mwisho kwa umasikini miongoni mwa wilaya zenye madini ambapo asilimia 62 ya wakazi wake waliishi chini ya Sh.1,000 kwa siku,`` alisema Bw. Kabwe

    ReplyDelete
  8. TAKUKURU wazomewa Tanga

    Na Dege Masoli, PST Tanga


    Mkutano uliyoitishwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) jijini hapa, umevunjika kabla ya wakati baada ya wananchi waliokusanyika kuwazomea maafisa wa taasisi hiyo wakiwataka waeleze kwanza hatua walizozichukua kwa vigogo waliodaiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

    Wananchi hao waliokusanyika jana katika mkutano huo ulioandaliwa na TAKUKURU kwenye uwanja vya Tangamano kwa lengo la kuwataka kutoa kero zao, uliingia sura mpya baada ya wakazi hao kuweka sharti la kutowataja walarushwa wengine hadi wale waliotajwa awali kuelezwa hatua walizokwishachukuliwa.

    Tafrani hiyo ya kuzomewa ilianza wakati Kamanda wa TAKUKURU wa wilaya ya Tanga, Bi. Bibiana Bundala aliposimama na kueleza lengo la mkutano huo la kutaka kujua kero zinazowakabili na kuwataka kutoa dukuduku zao, kauli ambayo ilizua mtafaruku mkubwa.

    Wananchi waliokusanyika katika mkutano huo kabla ya kuanza kuzomea walimtaka Kamanda wa TAKUKURU kueleza ni hatua gani zimeshachukuliwa dhidi ya watu ambao walishawaripoti kwao kwa makosa mbalimbali yanayohusiana na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

    Kutokana na hali hiyo, Kamanda Bundala alilazimika kuwaeleza kuwa taasisi hiyo bado inaendelea na uchunguzi juu ya kero zilizokwisha ripotiwa na kudai kwamba kila atakaethibitika atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

    Hata hivyo, kauli ya Kamanda huyo iliibua tafrani baada ya wananchi hao kudai kuwa ni majibu ya kisiasa kwani kero kadhaa zilisharipotiwa bila wahusika kuchukuliwa hatua na kudai kuwa taasisi hiyo imekuwa ikiwajibika sana kwa walalahoi badala ya vigogo ambao ndiyo wanaojihusisha na rushwa kubwa kubwa.

    Walisema kuwa kufuatia kwa hali hiyo hawana imani na utendaji kazi wa Taasisi hiyo na kuahidi kutotoa ushirikiano hadi kero zao walizokwisha ziwasilisha zipatiwe majibu.

    Akiwasihi wananchi hao na kuwataka waendeleze uhusiano nzuri na Taasisi hiyo, Kamanda Bundala alisema kutopewa matokeo ya awali kusiwafanye waache kuendelea kutoa kero zao mpya, kauli ambayo ilizusha vurugu za kuzomea, hali iliyosababisha kuvunjika kwa mkutano huo kabla ya wakati.

    Akiongea na waandishi wa habari baada ya kuvunjika kwa mkutano huo, Kamanda Bundala alisema hali hiyo imetokana na uelewa mdogo wa wananchi juu ya utendaji kazi wa taasisi yake na kuahidi kutafuta mbinu za kutoa elimu ya kutosha.

    Wakati huo huo, Patrick Chambo wa PST anaripoti kutoka Hai kwamba wananchi wa Bomang?ombe Wilaya ya Hai, wamelazimisha kuahirishwa kwa mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), wakishinikiza vigogo wa wilaya hiyo kuhudhuria mkutano.

    Vigogo waliodaiwa kukosekana katika mkutano huo ni Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Polisi (OCD), Hakimu wa Wilaya, Meneja wa TANESCO na maofisa wengine.

    Wananchi hao walidai kuwa, viongozi wa serikali walioambatana na TAKUKURU kujibu kero zao hawana mamlaka katika serikali hivyo hawawezi kutoa majibu ya maswali ya kero zao.?

    Tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni baada ya Ofisa Mtendaji kata ya Hai Mjini, Bi. Neema Lema kufungua mkutano huo wa hadhara uliondaliwa na TAKUKURU wilaya ya Hai kwa lengo la kukusanya kero za wananchi na kuwaelimisha juu ya rushwa.?

    Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Hai, Bi. Zawadi Ngailo alielezea madhara ya rushwa na sheria mpya ya kupambana na rushwa ndipo alipowataka wananchi wawe huru kutoa kero zao dhidi ya idara na taasisi za serikali wanapodaiwa rushwa ili kupata huduma.

    Baada ya kamanda wa TAKUKURU kutoa maelezo hayo na kukaribisha hoja kutoka kwa wananchi, ndipo hoja ya kuwataka viongozi hao wawepo ili wananchi watoe kero zao ikaibuka.

    ``Ndugu kamanda, TAKUKURU inayo malengo mazuri lakini simuoni OCD wetu, mkuu wa wilaya, hakimu wa wilaya daktari wetu wa wilaya na maofisa wengine.

    Mmemleta ofisa ardhi tu, ina maana kero zetu hapa Hai ni ardhi tu?? alihoji Bw. Robert Massawe na kuomba mkutano huo uahirishwe mpaka viongozi hao wawepo.

    Wananchi walimpigia makofi kuonyesha wanamuunga mkono ndipo Bw. Philip Lema na Sajenti Mstaafu Bw. Seph Mkambele walipoiomba TAKUKURU kuahirisha kikao hicho kwa kuwa kero walizonazo wananchi zinahusu idara hizo na hivyo kuzijadili bila kuwepo wakuu hao ni kufanya majungu.

    Kamanda wa TAKUKURU, Bi. Ngailo alikubaliana na hoja za wananchi na kuamua kuahirisha mkutano huku akishangiliwa na wananchi hao.

    ReplyDelete
  9. Big up baba!!!!!!!! Wacha waseme lakini monduli tutakuja tu. Watubiri mwaka 2015 tutamtoa raisi na sio waziri mkuu tena. Wanasema wamtunyamazisha lakini kumbe ndio kwanza wamewasha moto

    ReplyDelete
  10. Mwacheni Lowassa wa watu!Yalipokuwa yakitendeka yote hayo tokea mwanzo Kikwete alikuwa hajui?Urais tulimpa wa nini basi?Mwacheni apange maisha yake ya baadaye.Kuvunjika kwa Koleo siyo mwisho wa Uhunzi!

    ReplyDelete
  11. hongera baba saidia tu ila hizo milion 3 kidogo sana heeeeeee suti ikowapi?

    ReplyDelete
  12. kazi kweli kweli wataka nini tena baba na sisa wewe bye bye????ungetulia tu ulinde chako maaana hata ulichovuna kinakutoshaa..achia wenye moyo safi na uzalendoo..............watanzania amkenii eehhhh

    ReplyDelete
  13. Switzerland all ready to help on EPA funds

    2008-04-04 09:06:51
    By Guardian Reporter


    Switzerland has offered to help the Bank of Tanzania get back any money swindled from its external payment arrears (EPA) account and moved to the European country.

    The newly arrived Swiss Ambassador to Tanzania, Adrian Schlaepfer, told this paper in a recent interview in Dar es Salaam that his country was committed to working closely with Tanzania on the issue.

    ``Corruption is a development killer and we are committed to helping the Tanzanian government recover any money that was illegally gained and may have been moved abroad, including to my country,`` he said.

    The envoy said recent reports of scandals and the way state organs, particularly Parliament, had handled them had shown Tanzania as a beacon of stability and good governance.

    He noted that the way the scandals were being handled also showed that democracy and good governance were working in Tanzania.

    Ambassador Schlaepfer explained that, contrary to the prevailing stereotype about the Swiss financial system, his country had stringent legislation making it impossible for stolen assets to be hidden away in banks there.

    The envoy said, corruption was, naturally, a big concern to Swiss tax payers, who ultimately pay for the country`s ambassadors` development work.

    ``They want to be assured that their money is used properly and reaches those in need,`` he stressed.

    Meanwhile, he also underlined the need for foreign diplomats on assignment in developing countries to disabuse themselves of what he called a one-sided perception and start going out to meet people.

    He said it was important for expatriates from developed countries ``to visit as much of the country as possible and learn at first hand about how best to work with ordinary Tanzanian partners to reduce poverty``.

    The ambassador, who spent most of his career as an aid specialist before assuming his present responsibilities, said he has chosen for himself to show the way by touring Ifakara - one of Morogoro Region`s peripheral district centers.

    He said he saw Tanzania having great potential and significant natural and human resources as well as standing out as being stable and peaceful and an African showcase.

    The country still needs massive financial resources to cope with widespread poverty, he pointed out, cautioning that efficiency and effectiveness of aid were not necessarily a matter of size.


    SOURCE: Guardian

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...