Serikali imemteua Hajaat Kijakazi R. Mtengwa kuwa Mwenyekiti mpya ya bodi ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa), zamani Chuo Cha Sanaa Bagamoyo.

Taarifa toka wizara ya habari, utamaduni na michezo iliyosainiwa na msemaji wa wizara hiyo mzee Jacob Tesha, kwa mujibu wa sheria za wakala wa serikali namba 9 ya mwaka 1997, waziri Mh. Kapt. Goeroge Mkuchika pia amewateua wajumbe wanane wa bodi hio.

Taarifa imewataja wajumbe hao kuwa ni pamoja na Bi. Rose Sayore, Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Utamaduni, Mkurugenzi wa Utamaduni Mstaafu, Dk Daniel Kyaruzi Ndagala, Dk Herbert Francis Makoye ambaye ni mhadhiri Chuo Kikuu Dar na Profesa Hermes J. Mwansoko, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni.

Waajumbe wengine wa bodi hiyo ni Bi Judica Haikase Kida Omari, ambaye ni mchumi mwandamizi, Mh. Ramadhani A. Maneno, Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Profesa Elias Elieza Jengo, Mhadhiri UDSM na gwiji la sanaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 15, 2008

    HONGERA MAMA MTENGWA!! TUNAKUTAKIA MAFANIKIO MEMA KTK MAJUKUMU MAPYA ULIYOPEWA!!!

    NDEMA MAPUNDA, THESSALONIKI, GREECE

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 15, 2008

    hivi neno HAJAAT ni jina au ni cheo? ajuaye anijibu please.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 16, 2008

    Neno HAJAAT ni sawa na ALHAJ yaani mtu aliyewahi kwenda MAKKAH kuhiji.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 17, 2008

    huyu mama Mchapa kazi sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...