Kaka Michuzi

Habari za kazi? Leo katika ufukunyuku wangu mtandaoni nimekutana kakitu kadogo. Ni kwamba mpaka muda huu (1220hrs) watanzania wameshikilia usukani katika kumpongeza Bwana Nelson Mandela kufikisha miaka 90. Sasa sijui wadau wanaichukuliaje hii?

Tafadhali tembelea www.happybirthdaymandela.com na utaona.



Mdau Dommy

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2008

    I learned that courage was not the absence of fear, but the triumph over it. The brave man is not he who does not feel afraid, but he who conquers that fear.
    Nelson Mandela

    and

    I dream of the realization of the unity of Africa, whereby its leaders combine in their efforts to solve the problems of this continent. I dream of our vast deserts, of our forests, of all our great wildernesses.
    Nelson Mandela

    Tungekuwa na viongozi namna hii!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2008

    Nimeshangaa na kushikwa na butwaa.
    Hata sijui nisemeje? Sio tu Tanzania ya kwanza, lakini hilo 'gap' na nchi ya pili, ambayo cha ajabu ni Ujerumani.... inashangaza. Ukichukulia Afrika Kusini yenye iko mbali.. Du!
    Ngoja nisikie sababu watakazotoa wengine. Najua kuna watakaosema Upendo wa waTZ, kuna watakaoponda nk... ngoja nisubiri

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 28, 2008

    kama kawaida..... watanzania wengi hawana kazi za kufanya hivyo huwa wa kwanza kushabikia vitu kama hivi. usishangae kuona wanaongoza kwenye jambo kama hili.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 28, 2008

    Wadau hii imekaaje??

    Hivi hawa watu tnaowaheshimu nao pia wantuheshimu au wanatuona kama mbuzi tu???

    Namzungumzia mzee Mandela kwanini akafanyie birthday uingereza??? Kwamba afrika kusini hakumfai au tuelewe nini??? Anaashiria nini au ndo kasumba za mkoloni hadi kwa mandela????

    Anaona afrika hapamfai au vipi: Mbona anaudhalilisha uafrika kiasi cha kuona hatustahili sisi kusherekea nae bali wazungu tu.

    Tuweni macho s ajabu akifa ukasikia alisema akazikiwe ulaya.

    Kweli waafrika tuna mapungufu kwenye Genes zetu wala si utani wala kashfa.

    Mimi sielewi huu uzalendo wa mandela na wenzake uko wapi??? ahh bwanawe hata mandelaaa. unatukatisha tamaaaaa.

    wambie wazungu wakuambie happybirth day. Ndo utajua aipokuwa madarakani alikuwa anawatumikia wanani kati ya waafrika wenzake maskini au hao wazungu na ndo maana umaskini unaendelea south. Halaf eti anadiriki kusema zimbabwe imekosa uongozi yeye ameonyesha uongozi gani kwend akujikomba kwa malkia????

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 28, 2008

    To me I think Tanzanian we were aware of the program and from the heart we value his love to Tanzanians, he is truly friend of Tanzanians. Thats why many many of us sends him nice wishes.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 28, 2008

    Always we are good!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 28, 2008

    Hii tayari ilishatabiriwa toka kwenye vitabu vitukufu (bible&Quran) kuwa "Mfalme huwa hasifiwi nyumbani"

    Yaani kura za Tanzania ni zaidi hata zile za South Africa,nyumbani kwa Madiba na Msumbiji,ukweni kwake.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 28, 2008

    Nampenda sana Mandela kama nilivyokuwa nampenda Baba wa Taifa Hayati Mwl.Nyerere. Kweli hekima zao ni dawa kubwa kwa jamii nzima ya Kiafrika

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 28, 2008

    Wadau,
    Mie nafikiri MICHUZI-FACTOR imesaidia sana watu kuelewa siku hii muhimu ya Mzee Mandela. Hivyo wadau wa issamichuzi.blogspot.com mnastahili pongezi.

    Pia tutumie blog hii kuendeleza libeneke la kufahamishana masuala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi iwe ya Tanzania au kilimwengu.

    Mwisho wabeba-box na walavumbi hoyee!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 28, 2008

    tatizo sio kupost birthday wishes tu...hiyo ni rahisi sana tu....wasauzi na watu wamataifa mengine wanapost wishes na kudonate kakitu kidogo...so hiyo namba ya watanzania sijui ni wangapi wamedonate chochote towards charity work done by the 46664/ Nelson Mandela Foundation....

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 28, 2008

    Mandela is a great man, These are the people whose lives leave positive imprint on everybody's heart. We unayepiga madongo you don know what you are talking about. Don think all this world rallying around this one great person is crazy,watu sio kwamba hawana kazi za kufanya...Look at yourself and be ashamed of how tiny,useless and insignificant u are to this world...nobody recognizes your contribution at all,halafu unajifanya uko busy,what are you doing? Waliokuwa busy maisha yao yote wakifanya mema kwa hii dunia ndo hao dunia nzima inasimama na kuwatambua. Mature up young boy,and give respect to those who desrve it.How dare you?Mandela has a strong connection with Tz,alipotolewa gerezani tu,break ya kwanza ilikuwa Tanzania....na watanzania huwa hawasahau ukiwatendea mema.Ila ukichanganya mema na mabaya ndo hivyo tena...
    God bless the human race.
    EMERGENCYPOISON.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 28, 2008

    Kuhusu watanzania kuongoza, i agree with the person above, we have too much time in our hands and nothing much to do...
    Pili kwa ushabiki tunaongoza.
    Tatu, I don't appreciate a father figure and representative of africa to give the wakoloni the honour to host his birthday, kasumba? probably...?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 28, 2008

    Asante sana mdau uliyetuletea hii page, kwanza nimefurahi kwasababu nami nimeweza kumtakia heri katika huo umri wake mkubwaa anaoufikia sasa. Nimefurahi pia huyo ndau aliyetukumbusha kuwa NABII ASIFIKI NYUMBANI ni kweli kabisa. harafu kitu kingine ambacho nadhani watu hasa sisi waTz tumekisahau ni ule ukaribu uliokuwepo kati yake na Baba yetu wa Taifa, pili Heshima aliyokuwa nayo huyo Mzee wa watu kwetu waTz, nyinyi nmaosema hovyo hapo hivi mmesahau kuwa hata alipotoka jela tu huyu Bw, nchi ya kwanza kuitembelea ilikuwa ni Tz?. tafadhari, ndugu zangu kama hamjui kuwa history uwa inajirudia basi ndio hivi,sawa?
    NAWASILISHA HOJA. Aksanteni

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 29, 2008

    Kuna UBAYA gani kumpongeza Mtu Mzima MANDELA? Acheni hizo, Na nyie mnaotegemea Afrika Kusini iwe namba moja katika hilo, nataka niwakumbushe kuwa AFRIKA KUSINI WEUPE WENGI, na kwa kumbukumbu zangu MANDELA NI MTU MWEUSI,duh..

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 29, 2008

    Nelson Mandela,Nelson Mandela,Mwanamapinduzi huyo atazidi kuheshimika.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 29, 2008

    Mandela, Mandela, Mandela
    WITH ALL DUE RESPECT
    NILIKUWA NAMUELEWA ZAMANI LAKINI SIO SASA(WAKATI AKIPIGANIA UHURU)

    NILISTUKA BAADA YA KUFARIKI MWALIMU NYERERE HAKUJA KWENYE MSIBA!!

    MWALIMU ALIFANYA KILA KITU KUMSAIDIA IKIWA NA KUFUNDISHA VIJANA WAKE WA MSITUNI,KUWEKA MAKAZI MAKUBWA YA MAFUNZO YA MAZIMBU NA SEHEMU NYINGINE TZ

    SASA BIRTHDAY INAFANYIKA UINGEREZA!! ITS JUST STRANGE.

    IT COULD BE HE WANTS TO TELL THE WORLD THAT HE IS MORE THAN THE POPE,BUSH ETC, BUT ITS ONLY OK ONCE YOU THINK OF THAT PLACE CALLED RODEN ISLAND.

    ITS AFRICANS WHO HELPED AND NEVER GAVE GAVE UP ON HIM AND SO DOING THAT ON OUR OWN MOTHERLAND COULD CEMENT THAT RESPECT AND DIGNITY OF OUR BELOVED CONTINENT.
    I ACTUALLY HAVENT HEARD HIM CONDENMING SOUTH AFRICANS RECENTLY KILLING FELLOW AFRICANS(ESPECIALLY ZIMBABWEANS)
    BURNING THEM ALIVE!!! LIKE CHICKENS,AGAIN ITS STRANGE.
    THIS IS NOT SOUTH AFRICA WE ALL FOUGHT FOR AND SENDING OUR TAXES TO LIBERATE.

    THERE SHOULD NOT BE COPY CATS ON THIS

    F.M
    USA

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 29, 2008

    With all due respect

    i wonder if he doesnt have dimentia of some sort

    it doesnt make any sence at all

    African in the making
    Boston
    USA

    ReplyDelete
  18. KUNA MAONONI WAMENISIKITISHA HAPA WANAJIAMBIA KWAMBA SISI WATANZANIA HATUNA KITU CHA KUFANYA NDIO MAANA MAONI YAO KWA MANDELA YAMEKUWA MENGI. HEMBU FIKIRIA SIKU YA MAAFALI YAKO AU BIRTHDAY YAKO WATU WANAJUMUIKA NA WEWE KWA SABABU HAWANA KAZI YA KUFANYA, WANAKUTUMIA KADI NA SALAMU ZA NYONGEZA SABABU HAWANA KAZI ZA KUFANYA. WAKATI MR EBO ALIPOKUWA ANAWAULIZA HUKO BIZE NI WAPI MBONA HAJAWAHI KUFIKA MLIKUWA HAMUELEWI. TUNAOMBA MJIZIKE WENYEWE SIKU YA KUFA ILI UBIZE UEENDELE.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 29, 2008

    XENOPHIBIA

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 29, 2008

    nyie ma-annon mnaolalamika kwamba kwa nini kafanyia Birthday Uingereza, manajua kwamba birthday zake zote toka alipotoka gerezani alifanyia South Africa??? Sasa kuna ubaya gani sasa hivi kufanyia Uingereza? Mbona hamfanyi research kabla ya kupayuka?? No research no right to speak!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 29, 2008

    anonymous wa june 29/08.4:41

    mimi pia naungana na wewe ila mandela hakuweza kuhudhuria msiba wa nyerere on time kwakile alichokiita mstuko alipatwa mstuko mkubwa baada ya kupata msiba ule ila baadae alienda butiama na akapewa ng'ombe wa urithi kama ndungu wa karibu.

    nilikuwa nampenda sana pia mzee yule ila kanivunja nguvu sana kwanini hakusema chochote wakati watuwake walipoanza kuuwa majilani?? imenisikitisha sana na hii imepelekea mapenzi yangu kupungua sana kwake

    nilizani niko peke yangu niliyejisikia vibaya juu ya ukimya wake wakati watu wanauliwa tena watu waliomsaidia yeye na watu wake!! any way mungu wake anajuwa ukweli wake kama nae ni roho mbaya au hakujari n.k

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 29, 2008

    Wabongo kwa kulalamika...ati hakuja on time....kafanyiwa birrthday London.....bla bla bla...basi kwa taarifa yenu tarehe 18 ndio siku kamili ....kama na nyie mnataka kamfanyieni bongo ziko siku nyingi sana kabla ya tarehe 18 ...hata belated sio mbaya...huko London wamemfanyia na nyie kama mnazo mwandalieni mumkaribishe.....mwacheni babu wa watu ...

    Na kumbukeni tenda wema uende zako ...sio kwavile tulikua mstari wa mbele kwa mapinduzi yao basi tumshike shingo kwa kila atakalofanya...akichelewa kwenye msiba iwe taaabu ....akienda kufanyiwa party London muimbe.....


    Hapa greeting msgs kwa vile mnamuda wa kuziandika basi mtasema hawaoni upendo wetu??....ouch....hebu jadilini mambo ya maana.....

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 29, 2008

    Hao wengine wamewish na kudonate sasa wabongo easy kusend greetings tu bila kudonate chochote ndio maana zetu nyingi...duuuu

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 29, 2008

    wanajikomba ili wasauzi wawaondoe kwenye ile list ya watu wasiotakiwa nchini kwao...teh teh teh teh

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 30, 2008

    Nelson Rolihlahla Mandela was born in Transkei, South Africa on July 18, 1918.
    Hivyo birth day yake ni tarehe 18 july...hivyo waTanzania hamjachelewa kama mnamhitaji atakuja kufanyia kwenu...lakini wote mnaolalamika sielewi kwa nini, mbona nyie hamjawahi kufanyia birtday zenu vijijini kwenu?

    London amekuja kwa ajili ya kuchangisha pesa kwa ajili ya watu waishio na virusi vya ukimwi na alichagua london kwa ajili ya uwezo wa watu wa kuchangia na nisehemu ambayo inafikika na watu wengi wenye uwezo, nia na moyo wa kutoa, tumeshuhudia watu wengi wenye nia na uwezo wa kutoa wakimiminika kutoka sehemu zote za dunia kuja kuchangia na hata sisi wengine tumeingia kumuona kwa tupound kadhaa.
    Niimani yangu kuwa pamoja na mapenzi mema ya wabongo, uwezo wa kuwahost watu wote waliokuwa hapa London siku hiyo bado hatujafikia kiwango hicho....hii kwetu ingekuwa ni changamoto kubwa.
    Hivyo, nia yake kubwa ilikuwa ni hela na siyo "show off", hivyo na dhani ukiangalia na thamani ya £, ndiyo maana alichagua london, vile vile London nao huwa wanamuonyesha jinsi wanavyompenda maana ni juzi tu alikuwepo hapa kuzindua sanamu yake.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 30, 2008

    TANGU LINI BINADAMU AKAWA NYAMA CHOMA?


    Bla bla blaaaaaa
    Haya wapenzi wa kuchonga mdomo nendeni Sauzi basi mkachemshwe mwenye mafuta ya moto mkome au mchomwe hai!!!

    Nchi ni Tanzania tu na Mwalimu tazama tunavyoheshimiana na tunavyoheshimu wageni wowote

    Mambo ya kuchoma watu namna hiyo kulikoni?

    Aanapaswa kukaa kwake akemee upuzi badala ya kupanda masteji wakati sifa ya nchi yao imetiwa dosari kubwa namna hiyo.

    Itakuwaje kutaja tu ukimwi wa mtu mwingine kuwa unauwa wakati ndani ya nyumba yako kuna mtu ndugu yako anauwa mgeni wake na usiseme kitu?

    Kipi kifo kizuri? Bila shaka hakuna kizuri kuliko kingine, kifo ni kifo tu, ni kibaya.

    Nilikuwa na t-shirts zenye jina south Africa watu wananiuliza nawee umetokea huko ?? ikabidi nizitupe.

    Anafahamika, anasifika na anastahili lakini nchi yake imeporomosha sifa yao yote.

    Poa wadau tuendelee kuchonga tu lakini mwalimu alisema ukibagua mgeni na kumuua utambagua jirani na kumuua halafu ndugu yako na kumuua halafu mkeoa au mmeo na kumuua na watoto wako mwenyewe n.k n.k , halafu unakuwa ni jitu lipuuzi na liuaji tu,na hautaacha, utaendelea kuua ,nikweli kabisa

    Respect

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 30, 2008

    Just a point of correction ...!!!!

    Mandela hakuipeleka birthday yake Uingereza yeye mwenyewe

    Ni waingereza wameomba wamfanyie hiyo BD huko kwao na yeye hakuwa na sababu ya kukataa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...