Kaka habari za kazi iliyo bomba sana. Kazi yako naifagilia kaka hongera sana Naomba msaada kwenye tuta kaka.
Mi ni kijana mkiristo miaka 36 nimejikuta nimejichimbia zaidi shule namalizia Masters. Naitwa James, ni kijana mpole, mchapakazi, Mtanzania. Kwa blog yako kaka naomba kutafuta dada aliye SERIOUS TU tutakayeishi kama my waifu wangu.
Atakuwa na uchaguzi wa kunichagua kama mimi nitakavyomchagua kwamba halazimishwa kunipenda kama hatanipenda.
Na endapo atakubaliana na hilo awe tayari kupima afya zetu zaidi ya mara mbili kwa muda muafaka kabla ya kuendelea na mambo mengine.Awe na elimu ya kidato cha sita na zaidi ya hapo ni nzuri zaidi.
Awe mrefu si mnene (unene wa kawaida ni bomba), mwenye tabia mzuri, talkative, cheerful na mwenye sura ya nzuri na mkiristo Asiye na makuu anayetarajia mambo ya juu.
Mi ni mtoto tu wa mkulima ninayetafuta maisha wala si wa matawi ya juu.
Anayekubaliana na ombi langu akina dada please niandikie ndatangule@yahoo.com
na akituma picha ya full ingekuwa poa zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. well nitakuunganisha na demu wangu ambaye nimempiga chini hivi karibuni najua atakufaa. Anazo sifa zote hizo sema mimi hatukuwezana kwasababu nini hii yake ndogo kiasi hawezi mapigo yakimakonde. hata ukitumia jelly bado haikusaidia. But ukiondoa hilo she is everything!

    all the best
    Mimi hapa nakutumia email yake soon

    ReplyDelete
  2. wewe ni mkorofi tu,nahuwezi pata mchumba!miaka 36 mbona sisi tumesoma tukiwa na wachumba wachumba tu toka primary inakuaje hadi 36!labda zarau, ujeshi mwingi na ubahili wa kupindukia. review kwanza your personality.

    ReplyDelete
  3. 36??Masters??well..umeshindwa hata kukamata class-mate wa primary,0'Level,A'Level,Undergraduate au hata binti wa Mjumbe wa Nyumba 10 au hata M/kiti wa mtaa mwenye sifa hizo??anyways, you're not 2 late.ila kwa kukusaidia 2, nadhani ungeweka na photoz kadhaa ili uwape urahisi hao watahiniwa(kinadada)

    ReplyDelete
  4. Hata mimi naungana na huyo sina makosa hapo juu, huyu hana lolote ni mkorofi tuu... kwani huna ndugu au marafiki waka kuunga na rafiki zao wa kike au ndo mpaka ujianike hapa...
    Hivi watu mna tufikiriaje wanawake?? mnadhani sisi ni vyombo fulani tuu ever available au? Jiheshimu kaka!! Na kwakweli hujeshi mwingi na ubahili ndo maana huna mchumba, na wata kukimbia kwa sana tuu...
    Grow up!!
    Ni mimi, DADA LAO

    ReplyDelete
  5. Yeah!!!
    James Maembe,Thank GOD umeamua kuoa sasa.Wasalimie Canada.

    ReplyDelete
  6. Huyo kaka yaonesha kazi yake ni kuonja, onja tu kwa kila demu mpaka anakuja kustuka umri umekwenda,na kwa dunia ya sasa hakuna msichana anayependa kuchezewa,akina mwanaume hana mwelekeo anaachana naye anakimbia kwa mwenye uwelekeo.Kaka jiangalia wewe kwanza.

    ReplyDelete
  7. James, umejijuaje kama wewe ni mpole??? ati mchapa kazi!! halafu unaweka vigezo vya ajabu ajabu, "mnene wa wastani, elimu n.k" kama kweli unatafuta mywife wa kuishi naye hutakiwi kuweka "conditions" za kipuuzi puuzi. kwa sababu waweza oa mke mwembamba na baada ya muda akawa mnene, sasa sijui utamtumia tena michuzi akutafutie!! Mbaya zaidi wewe ni mkatoliki, tena mzuri tu na mpole, endapo huyo unayemtaka "akajipretend" kwa kuwa anataka mume, ghafla akanenepa na kubadilika sijui utaenda kwa paroko gani akufungishe ndoa ya mitala.
    Pili, inamaana kwa umri wako wote sijui 36 years hujawahi kuwa na "girlfriend"? Kama kweli wewe ni mpole wa kujisifia kiasi hicho wewe! hujapata kushiriki kwenye penzi hata mara moja?? na ukaridhika naye.

    Tatu, wewe inaelekea umesoma seminari, Lakini mbona vijana waseminari wajanja tuu.?? wewe unakuwaje??

    Kama katika umri huo, mpaka umtafute mke kwenye mablog lazima una matatizo, huwezi kuishi na mke, sio siri, huwezi ishi na mke hata kidogo.Pamoja na upole na nini sijui lakini unamadhaif kibao nimeona.

    Mwisho, kama kweli ni mpole, basi omba sana mungu akupatie mke unayemfikiria awe hivyo. Kwani mke mzuri hupatiwa na mungu, mimi naamini hivyo.Ila mke wa kutafuta kwenye vyombo vya habari ndg yangu james, utakuja pata mtu ambaye hukumdhania. Jiamini, omba mungu sana na pia jichanganye na watu. ninavyoona mimi wewe ni mtu wa kufakamia kitabu tuuu, hujichanganyi na vijana.

    KIROBA

    ReplyDelete
  8. Uyu jamaa inaonekana yupo serious kutafuta mchumba naomba tumsaidie,sababu jammaa kameza meli (domo zege) usijali kijana utapata tu,omba mungu,wadau tutakusaidia kutafuta usikonde

    ReplyDelete
  9. Hilo ni jambo la kawaida kabisa unajikuta umri umekwenda mchumba hakuna. Hivyo umefanya jambo la maana nadhani mtandao huu unasomwa na watu wengi na utapata mtu. Pia maombi na usiache kujichanganya mara kwa mara. Kanisani, kwenye harusi na sherehe mbali mbali, makazini na vyuoni pia ni sehemu nzuri za kukutana na mchumba.

    ReplyDelete
  10. mwacheni j wawatu kijana miaka 36 ina shida gani bwana hao waliiooa na miaka 23 wako wapi zaidi ya mastress tu bora amejinguzia muda wa usumbufu ktk maisha wewe kaka yangu utapata tu mwanamke tena umesoma na upate kakazi kako uwongo hapo aaah asiyekutaka nani kina mareale waliokubuhu walipata vimwana vya miaka 23 akiwa kwenye forties ahh bro kwa raha zako utapata wengi tuuu ushindwe mwenyewe tuu.

    ReplyDelete
  11. MDAU NAMUUNGA MKONO KWANI HILO NI SUALA LA KAWAIDA TU,HII INATOKEA MTU UNAONA MUDA UNAKWENDA NA HUPATI MTU WA MAANA KARIBU YAKO KWA HIYO KUTANGAZA HAPA NI POA TU KWANI UTAPATA MTU MWENYE SIFA ULIZOZITOA.
    MICHUZI WACHA NA MIMI NIDANDIE,KINADADA MIMI PIA NINA 34 KAMA HUYU MDAU NA MIMI NATAFUTA MDADA ALIYESERIOUS HASWA,NIPO USA,MDADA AWE NA AGE KATI YA 24-27,HIGH SCHOOL OR COLLEGE DEGREE,LIGHT COMPLEXION SKIN,READY TO GET HIV TESTING, SHOULD WEIGH BTN 50-55 KGS,TALL ENOUGH TO APPOACH MY 5'8 FT,CHRISTIAN,ATTRACTIVE

    PLAESE MICHUZI NIMEDANDIA BUT SERIOUS ON THIS MATTER.

    NB:ONLY SERIOUS GIRLS WITH THE MINIMUM OUTLINED QUALITIES SHOULD RESPOND TO THIS,HIT ME HERE:davidmckia@yahoo.com

    ReplyDelete
  12. Inawezekana kabisa ukafika miaka 36 bila ya kuwa na mtu anayefaa kuitwa mke wako. HWote tunakubaliana kwamba upendo wa wengi umepungua sana. Unamtafuta mtu ili awe mwenza maishani, baadae unasikia katembea na mtu mwingine akiwa bado yuko kwenye uhusiano na wewe. Na mimi nadhani hili ni kosa kubwa sana ambalo halifutiki kirahisi. inawezekana kufikia umri huo bila kuwa na mtu anayefaa kuwa mwenza kama hukuwa na bahati(!?) katika mahusiano.

    ReplyDelete
  13. Mimi nawashangaa sana watu wanaomponda huyu jamaa, mimi nasoma Europe, sasa hivi niko kwenye early 30's girlfriend wangu niliyekuwa naye ambaye nilikuwa nategemea kumuoa, nimekuja kustuka anatembea na jamaa mwingine, sasa kwa mimi hilo kosa siwezi kumsamehe, nimeona niachane naye na nitafute mwingine priority awe ni Mbongo mwenzangu, at least high school and above.
    Mdau,
    mctz2000@yahoo.com
    Ughaibuni.

    ReplyDelete
  14. kumbe mpo wengi! lakini hakuna ubaya kuweka mambo hadharani kuwa unatafuta mchumba, tunaishi zama za uwazi ambapo unaweza kuwasiliana na watu wengi popote duani. Akina dada msijivunge, hawa jamaa wanamaanisha wanachosema.

    ReplyDelete
  15. mimi nimewatumia picha za rafiki wangu wenyesifa kama wanazotaka hao wawili hapo juu,cha kushangaza hawasemi kama wamezipata au hata asante sasa sielewi kama kweli wanania au ni kejeri tu.

    ReplyDelete
  16. Watu wanaomkandia huyu mtu honesty labda hawajatoka nje ya nchi na wanaona kuwa 36yrs old ni too old. I can't blame them kwa vile nchi yetu life expectancy yeke ni only 46 kwa hiyo huyu anaonekana kama grandpa vile.....lakini kwa ukweli mbona umri wake ni wakawaida tu ...kwanza hapo mpaka apate mtu wake anaweza kuhit 37 yrs old..... mpaka wafahamiane vizuri na kuweka mambo yao clean anaweza kuwa 38 and up ...na bado it is pretty good....

    I just turned 38yrs old in August - I have been married for almost 3yrs now. My hubby is 42 yrs old and will be 43 when we have our little one.

    This will be our first - and feel great and I am glad we didn't start any sooner.

    I think it may be a bit easier {physically} on some of the younger couples, but we are so grateful for the experiences we had before we "settled down". We had a chance to travel, build our careers, etc.

    Honesty, I feel good about being in the "older" category.

    Good luck James!

    ReplyDelete
  17. Anonym.wa 10.47 Naona huna point, wataka kutuonesha unajua kiingereza sana na umeishi nje, kuishi nje ya bongo sio tija. Elewa kila mmoja ana mtazamo wake. Ninalotaka kukuambia, siku nyingine toa point. Huu sio uwanja wa michemsho.Ala.

    Q

    ReplyDelete
  18. NaFiliri huyu Mchumba atakufaa sana,kwanza hana njaa kabisa,pia ni Msomi mkali,Pesa kwake si Tatizo:
    "Hi
    My name is Cassandra Moloy,Im 28 yrs old and i have no kids and im single. I have 5 degrees and a very successful business enterprise all over S.A.
    My wish is to meet a loving,kind,honest and carring to share my wealth and love with.Iam willing to accept his kids and if he's unemployed or fired it's not a problem! money is not a problem.I have a fleet of cars including a Hammer,Golf5 Nissan Navara,and BMW Anaconda.I love pet dogs and nature.I have 2 houses in Bedfordview and Bassonia and 4 holiday homes overseas. I also love travelling but so far there has been no companion as men often feel intermidation by my weath.
    Im not arrofant. iam beatiful,sexy,witty have a good sense of humor,and a lovely smile.
    if you are interestedor have brother or friend that might be, call on 084 774 2062 Wishing to meet you soon."

    ReplyDelete
  19. wakati mwingine ni kweli unaweza kuwa na mchumba na uchumba ukadumu kwa miaka mingi then ukagundua ana uhusiano na mtu mwingine ambaye pengine mwanzo alikutambulisha kama ndugu yake kumbe mume mwenzio. so miaka 36 kama uliwahi kukutana na cases kama hizo si ajabu wadau mwenyewe yamenikuta.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...