JK na mama Salma Kikwete wakiwa kwenye game ya Wnba kati ya washington mystics(75) vs chicago sky(79) ilofanyikia verizon center downtown dc.chini mdau wakila snepu la kishikaji na jamaa kabla ya gemu hilo
MAREKANI YATANGAZA DIPLOMASIA YA
MPIRA WA KIKAPU KWA TANZANIA
Na Mwandishi Maalum

Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ijumaa, Agosti 29, 2008 alimaliza ziara ya kikazi ya siku tatu yenye mafanikio makubwa katika Marekani kwa kuhudhuria mchezo wa mpira wa kikapu wa ligi ya Marekani ya wanawake ya WNBA kati ya timu za Washington Mystics na Chicago Sky.

Kabla ya mchezo huo kwenye uwanja wa kisasa wa Verizon Center katikati ya jiji la Washington, Rais Kikwete alihudhuria shughuli fupi ya kutangazwa kwa “Diplomasia ya Mpira wa Kikapu” kwa Tanzania kwenye uwanja huo huo.

Katika shughuli hiyo ambako Rais Kikwete alifuatana na Mama Salma Kikwete, Balozi wa Marekani katika Tanzania, Mark Green, alitangaza ujio wa nyota wawili wa mpira wa kikapu katika Tanzania mwezi huu wa Septemba.

Rais Kikwete na Mama Salma wote walipata kuwa wachezaji wa mpira wa kiapu katika ujana wao.

Chini ya diplomasia hiyo, wachezaji wawili nyota wa mpira wa kikapu, watatemblea Tanzania kati ya Septemba 8 na 11 kuendesha mafunzo ya mchezo huo kwa vijana.

Shughuli hiyo inadhaminiwa na Ofisi ya Michezo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ya Sports United.

Wachezaji hao watakaotembelea Tanzania ni Jennifer Azzi, mchezaji wa zamani wa kike wa WNBA ambaye alicheza katika ligi ya NBA kwa miaka mitano akiwa na timu ya Utah Starzz.

Mama huyo, ambaye alipata shahada yake katika Chuo Kikuu cha Stanford, pia alishinda Medali ya Olimpiki ya Dhahabu akiwa na timu ya taifa ya Marekani.

Mwingine ni Matt Bonner, aliyepata shahada yake katika Chuo Kikuu cha Florida na ambaye amekuwa anacheza katika ligi ya NBA tokea mwaka 2003. Kwa sasa anachezea klabu ya San Antonio Spurs.

“Diplomasia ya Mpira wa Kikapu” inalenga kuimarisha uhusiano kati ya wananchi wa Marekani na wale wa nchi nyingine, na hasa vijana.

Mpango wa “Diplomasia ya Mpira wa Kikapu” ulianza mwaka jana kwa kuhusisha nchi ya Congo na mji wa Jerusalem.

Mwaka huu, mbali na Tanzania. wachezaji nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani watatembelea nchi za Saudi Arabia, Thailand, Kazakhstan na Kyrgyzstan chini ya mpango huo.

Katika mechi hiyo kali ya juzi kwenye uwanja wa Verizon Center, timu wenyeji ya Washington Mystics ilishindwa kwa vikapu 76-73.

Mbali na timu ya Mystics, uwanja huo pia hutumiwa na timu ya mpira wa kikapu ya wanaume ya Washington Wizards, timu ya mpira wa magongo ya Capitals, timu ya mpira wa kikapu ya Chuo Kikuu cha Georgetown na una uwezo wa kuingiza watazamaji 20,000 kwa wakati mmoja.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ana taarifa za wanafunzi kuanguka kwa kinga ya KICHOCHO?

    ReplyDelete
  2. hii picha ya mdau anayepozi kupata picha na Jk inanikumbusha scene fulani kwenye sinema ya coming to america.

    ReplyDelete
  3. Haya sasa, mnaopigaga mikelele, ooh, mama wa kwanza anavaa vilemba sijui nakazalika nakazalika, leo semeni, maza katinga vitu vya uhakika, na nyororo ka waicheki kwa mbaali!! du! maza kapendeza. Nampa big up sana.

    ReplyDelete
  4. Huyo msela ni nani?Naona ana zile staili za zamani za kupiga picha Dar es salaam railway station.Ili kijijini wakujuwe ulifika Dar.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...