Kaka Michuzi Kwanza nakupa hongera sana kwa besidei yako ya kutimiza miaka kadhaa uliyoiadhimisha ukiwa Dodoma.
Pili naomba kupitia blog yetu hii ya jamii kumtafuta ndugu yangu aitwaye DEUSDEDIT TIRUMANYWA IZUMBA ambaye nimepotezana naye kwa muda mrefu sasa.
Mara ya mwisho alikuwa anafanya kazi Idara ya Mifugo akiwa Same. Yeyote aliye na habari zake naomba tafadhali anijulishe kupitia blog hii au tuwasiliane.
Mimi naitwa Switbert Msoga na
email yangu ni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ndugu yangu Msoga, polesana kwa kupotezana na rafiki yako kwa muda mrefu, hii inaonesha jinsi gani unavyomjali, kumthamini na milivykuwa mmeshibana na rafiki yako huyo, hata ukafikia uamuzi wa busara kutumia vyombo vya habari kumtafuta ili mzidi kuwasiliana.

    Lakini napenda kukupa ushauri wa bure juu ya jambo hili la kumsaka mtu mliyepotezana naye kwa muda mrefu.

    Ndugu yangu, sipendi kukukatisha tamaa, ila ndio hali halisi, siku hizi kama umepotezana na mtu,ama wa karibu sana au ni rafiki tu kwa kipindi hata cha miezi mitatu hivi, tafadhali ulizia habari zake kwa makini kwani matukio ni mengi siku hizi!!!

    Unaweza jikuta unajuta kuuliza, ukabaki unasononeka tuu, sina maana ya kuwa ndg unayemuulizia keshapitiwa na wimbi la matukio hayo, la hasha, ila ningekushauri siku nyingine tafadhali ama waulize rafiki tu wakaribu mlokuwa naye ama waulizie nduguze tena kwa utaratibu sana.

    Nafasi ni ndogo, ningekupa na mifano kadhaa ambayo watu wamefadhaika na kushindwa kuelewa wafanye nini pale walipoulizia jamaa zao kama unavyouliza kwa comfidence zote na wakaambiwa maaneno mabaya juu ya hao wanaowaulizia.

    Je? huna hata anwani ya kule alikokuwa anafanyia kazi ama mtu unayemjua pale ofisi za mifugo Same ambaye ana habari zake kwanza kabla ya kuchukua uamuzi huu naoweza kusema mzito???

    ReplyDelete
  2. Hamna tofauti yoyote ya kuulizia kimya kimya na kuulizia humu ndani matokeo yatakuwa ni mamoja na wala mtu hawazi kuyabadili, ukiambiwa amekufa baada ya kuulizia kimya kimya au kuulizia humu ndani ni sawa tu, sioni point yoyote hapa ambayo ilikuwa inaelezewa na huyu mtu hapo juu. Nafikiri hakufaya vibaya kuulizia humu ndani kwa vile kuna big audience ambayo ina-visit hii site and now is nearly 5 millions.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...