ofa za fleti namaduka mtaa wa narung'ombe
kijiwe cha watoto wa mjini cha saigoni kiko vile vile ila kimezungukwa na huo msitu
mtaa wa narung'ombe karibu na lango kuu kuingilia shimoni kariakoo sokoni, cheki majumba mengine yanavyozidi kuumuka
mahoteli kibao kila kona
nyumba chache za mbazu za mbwa zimesalia kariakoo ya leo
ingawa mimi unaweza kuniita ni mtoto wa kariakoo, ama boni hia hia, lakini leo nilipopita mitaa hiyo nilishikwa na butwaa. mbavu za mbwa zote zinayoyoma na msitu mnene wa simenti unatanda kila kona. cha kustusha ni kuona kwamba wahusika wanakuwa kama hawana habari kwamba ukuaji wa kitongoji hiki si wa kuchekea na ni hatari kwa jamii siku za usoni.
yaani pamoja na maendeleo yote hayo, sijakuta sehemu hata moja ambayo miundombinu yake imeboreshwa ama imepanuliwa kulingana na maendeleo yanayoendelea. mifereji ya maji machafu ni ile ile ya mwaka 47 wakati jiji lilikuwa na wakazi si zaidi ya milioni moja. maegesho ya magari hakuna, achilia mbali ufinyu wa barabara ambazo machinga na wenye maduka wanagombea kufanyia shughuli zao. kubwa kuliko yote penye kila ujenzi wa jengo jipya utakuta ubao unaoonesha kwamba wamepata baraka zote za wahusika kufanya ujenzi huo.
isitoshe hivi sasa kariakoo haina tofauti kabisa na kitongoji cha deira kule dubai. asilimia kubwa ya wafanyabiashara ni wa kutoka uganda, zambia, kenya, malawi, zimbabwe na hadi kongo kwa kabila. kama huamini piga hodi kwenye hoteli zote na omba orodha ya wapangaji. isitoshe wengi ukiwauliza utaambiwa hawana haja tena ya kwenda dubai kwani dar inawatosheleza kwa mahitaji yao yote ya kununua bidhaa na kwenda kuuza makwao. yaani ukiacha wafanyabishara hao wa nje wanaokuja kununua bidhaa hapa dar, wapo wengine ambao wameshafanya dar ni makao yao makuu ama godauni la bidhaa wanazofuata dubai ama china na kuzirundika dar.
wengi wengine wa wafanyabiashara hao ni jamii ya wachina ambao wamejazana kariakoo kiasi cha kuzua maswali endapo kumepitishwa 'ruksa' ya wao kuja 'kuwekeza' jijini dar kwa kufanya umachinga, sambamba na wenyeji. unajiuliza endapo kama kweli wahusika wa masuala ya uhamiaji wanafanya kazi zao barabara. wakiwa na mihela kibao ya dola, wachina hao sasa wamefanya bei ya duka ama dirisha la kufanyia biashara kugota hadi dola 2000 kwa mwezi, kiasi ambacho mmatumbi wa kawaida kwake ni ndoto. ndio kusema baada ya muda si mrefu wamachinga wote kariakoo watakuwa wachina.!
Hii sio fitna bali ni hali halisi, na nimeiweka hapa kwa makusudi kwani leo waziri mkuu mh. mizengo pinda kaanza ziara ya siku nne ya kutembelea mkoa wa dar. sina uhakika kama maafisa wahusika watampitisha kariakoo ajionee mwenyewe hali halisi, sio tu ya kujaa wamachinga wa kichina tu bali pia namna ujenzi holela wa maghorofa unavyoendelea utadhani wamekatazwa kujenga nje ya kariakoo.
-michuzi





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. jamani hii kuwa na majengo malefu na wapangaji wachina si maendeleo ila ni polution tu kwani hawa watu wanaongoza kwa vitu vya fokong yaani vitu vyao ni uozo mtupu mimi naona mnakalibisha maafa tu maana msifikili vinatoka china vingine vinatengenezewa hapo hapo kisha mnadanganywa vinatoka china. kisha polisi wetu kwa mshahara wao mdogo wakistukia kipindi wanapewa $50 wanakaa kimya watatuletea balaa kama walivyofanya kule kwao wanahalibu mazingila amkeni.

    ReplyDelete
  2. mji wa dar hauna hewa nzuri tena mnazidi kuuharibu na magorofa uchwara sita kaa dar bora nikalevubi la dodoma kuliko kufa na joto nahewa chafu hapo dar,,

    unajuwa mtu ukimwambia hatakuelewa ni sawa na kumwambia kombe unatembea polepole hatakuelewa wakati yeye anajiona kakaza mwendo kwelikweli karaga baho na ubwazibwazi wenu wabongo mnaojiona wajanja na ujanja wenu msioonambele,...

    ReplyDelete
  3. ule mji wa dar huwa wanatupa wapi taka??
    sasa ni hivi juzi ktk al-jazira wameonyeshwa wachina wanachinja paka huko kwao wanawachuna. sasa kama wako hapo kariakoo ngozi za paka na uchafu wao utatupwa wapi??

    jiji litanuka hilo mbona kasheshe+ uozo wao wa viwanda feki na mafuriko yakija mtanyamba kama hmtaki kutumia hakili jiji lahalibiwa hilo

    ReplyDelete
  4. inatishia amani ila twendeni hivyohiyo utastukia hao wote ni maraia wa bongo na kiswahili hawakijuwi ila kinamwajuma watakijua ki china.

    ReplyDelete
  5. Ah! Mitchu Boy, umenifikisha home hapo Sigon naona kama jana tu!.
    Ah! Aliyekufa Mungu na amrehemu!
    Hassan Juice bado yupo hapo? au siku hizi anaitwa Hassan KUKU?

    ReplyDelete
  6. Kaka Michuzi,

    Nakushukuru sana kwa makala hii. Nimependa jinsi ilivyo original na jambo unalolielezea linaigusa sana jamii yetu. Licha ya kuliweka tatizo la utitiri wa Wachina walio vamia Dar es Salaam wakifanya kazi za hovyo, vile vile umetuonyesha Kariakoo ilivyobadilika. Kwakweli makala kama hizi zingekuwa nyingi ningekuwa natembelea blog hii ya jamii kila siku. Sasa hivi nina tembelea mara moja kwa wiki.

    Nashauri utumie judgement yako ulete makala kama hivi kwasababu sio tu zitaleta uamsho bali pia zinawahabarisha wana blog hii walio nje ya nchi kama mimi. Picha moja imenikumusha mbali sana. Njia njilikuwa napita kila siku nikitoka shule kwenda kupanda basi la UDA au KAMATA kwenda Mikoroshini (eti sikuhizi wanaita Msasani).

    Mimi mdau wako nilichukua Meli siku nyingi sana. Nipo mtoni sikuhizi kwa Obama, napiga box. Vijana siku hizi wana bahati wakitaka kuja mtoni wanaenda pugu road wanapanda ndege.

    ReplyDelete
  7. MUNGU ANISAMEHE,LAKINI KATIKA VIUMBE AMBAO SIWAPENDI NI WACHINA ...JAMANI NI WAOVU WA VITENDO NA IMANI

    FULL OF FAKE THINGS,NA KULE MITAANI WAKO MACHANGUDOA WA KICHINA{HUWEZI AMINI}

    WANA ROHO MBAYA HAWA WATU,NA THEY CAN DO ANYTHING....THEY TRANSFER LOTS OF DOLLARS EVERYDAY KWENDA KWAO,WHAT KIND OF BUSINEE ARE THEY DOING ZA KUTUMA DOLLAR KIBAO KWAO KILA SIKU?KWA UMACHINGA WANAWEZA KUPANGA KODI YA DOLA 2000 KWA MWEIZ???LOL MBONA SISI NDUGU ZETU KODI YA 150,000 KWA MWEZI NANGA INAPAA

    KWAHIYO SERIKALI INAACHIA WATU WAKE WAAENDEELEE KUWA MASIKINI NA KUTAJIRISHA WENGINE

    NA SASA WAMEEANZA KUJAA WAMAREKANI HAPA JIJINI,WANAKIMBIA MATATIZO YAO YA NCHI ZAO ,WANAKUJA HUKU MASIKINI BUT IN NO TIME WANARUDI KWAO MATAJIRI...HUU NI UJINGA NA WIZI MTUPU

    ReplyDelete
  8. katika siku ambazo michuzi huwa unapositi vitu vyenye maana ni leo. hii kwa kweli umeweka mbali u-uhasama (kunradhi u-usalama wa taifa. hongera sana

    ReplyDelete
  9. Tufike mahali watanzania tuchangie mawazo ya kujenga bila ya ghadhabu wala kisirani kuhusu hali duni ya kipato chetu kwa kuzielekeza hasira zile kwa wageni wetu ambao hawakuhusika kwa namna yoyote ile katika ufukara wetu au mfumo duni wa uwekezaji uliopo hapa nchini.Tujilaumu sisi wenyewe na tujiepushe kuwabebesha wageni kwa matatizo na udhaifu wetu.Katika kila nchi duniani utakuta mchanganyiko wa watu wa mataifa mbalimbali,siyo Tanzania pekee!Nenda Uingereza au Marekani utakuta kuna maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya wafanya biashara na wajasiriamali wa kutoka nchi zingine duniani.Katika majiji makuu duniani utakuta kuna vitongoji maalum kwa Wachina au Watu wa Mashariki ya Mbali ambao kati yao utakuta wenye migahawa,mahoteli,maduka ya nguo na mapambo na bidhaa nyinginezo!Utakuta vitongoji maalum kwa Wahindi ambao kati yao utakuta wenye mahoteli,migahawa,maduka ya nguo na huduma nyinginezo na kadhalika.Na wote hao utawakuta wanafanya shughuli zao kihalali kwa mujibu wa sheria za nchi husika.Wageni hao hawaingii nchi yoyote kinyemela na bila ya kuwa na vibali vya makazi katika nchi husika.Wakifanya hivyo watakuwa wamevunja sheria za nchi husika na wanaweza kukabiliwa na adhabu kwa mujibu wa sheria za nchi husika.Kwa hiyo siyo busara kuanza kulalamika kwa uwingi wa Wachina nchini na baadhi yao wakionekana wanajishughulisha na Umachinga BADALA YAKE tupambane na MADIWANI WETU katika maeneo husika ili kufahamu utaratibu mzima unaoruhusu wageni kufanya shughuli nyepesi ambazo hata wenyeji "wana uwezo wa kuzifanya wenyewe"na ndipo suluhu ipatikane.Kuwepo kwa Wachina kwa wingi jijini Darisalama hakuwafanyi watanzania wa Darisalama WASIWEZESHWE NA SERIKALI YAO NA TAASISI ZA FEDHA ZA NCHI YAO.Huwezi kufanya biashara isio na soko!Lazima kuna mapungufu sehemu fulani na ndiyo maana ukakuta wageni wakichanganyikana na machinga wetu katika biashara za kawaida kabisa ambazo zingestahili kupewa kipaumbele kwa wenyeji tu wa maeneo yale.Tusiwalaumu Wageni,bali Tuwalaumu Viongozi wetu wenyewe tulio wakabidhi madaraka ili watuongoze na kulinda maslahi yetu.Watakapo shindwa kutimiza wajibu wao,basi tuwawajibishe kwa kuwaondoa katika nafasi zao za Uongozi na kuwaweka wengine bora zaidi!Kuna ubaya gani na sisi Darisalama tukiwa na kitongoji maalum cha Wachina Wafanyabiashara "Small China Town",kama ilivyo katika miji mingine mikubwa duniani!Kuhusu ujenzi wa magorofa maeneo ya Kariakoo,kitu muhimu cha kuzingatia ni ujenzi wa majengo yenye kuvutia na yatakayo ongeza uzuri wa jiji letu la Darisalama.Isiwe bora kujenga gorofa tu mtu akiwa nazo mfukoni!Lazima kuwe na mpangilio maalum unaovutia na utakao lifanya jiji letu lipendeze zaidi na zaidi!

    ReplyDelete
  10. Kaka kuna mambo yanapelekea hali hiyo kuwapo

    1. rushwa ni kubwa mno manispaa na watu hawaogopi kwa sababu walaji ni wengi...kwani kuna mtu kafungwa kwa ghorofa lolote likianguka?..kwani hawajui wachina hata vibali vya kuishi hwana lakini wanauza pipi feki, juice za chemicals na karanga toka kwao?

    2. watendaji wengi wa manispaa hawakai zaidi ya 3years in one district kwhiyo akifika dar ndio sehemu ya kuchuna,,akiharibu huwa transfer kwenda nachingwea, chato (sina maana ya kukejeli wenyeji wa sehemu hizo) huko uchumi ni mdogo hapati hata mtu wa kumhonga ili afungue biashara

    3. Ukisema wewe unafikiri utasikilizwa? aseme mkuu wa nchi utasikia wanavyo harakisha maagizo ona pale dengu beach vibao vimetolewa na watu wanapaki na kupunga upepo mzuri...kuna jamaa alikua na kipikipiki pale kutwa anatembea na locki za kufunga matairi akikuta umepaki pale au umpe rushwa hatakama gari imepata break down...huo mradi sasa umekufa baada ya Rais kuwakemea watendaji wa jiji...ona coco beach baada ya Rais kusema pameota mbigiri...sasa manispaa kinondoni wametoa tender ya kuendeleza eneo hilo kuanzia la dolce vita hadi karibu na seacliff

    Naungana na wewe kaka

    ReplyDelete
  11. Hongera kwa kutuletea taswira na mada. Imesheheni ujumbe kushusu: ujenzi holela, miundombinu hafifu, kusukumwa nje kwa wazawa na watu wa kuja, ufisadi unofanywa na wapanga-mjina wakuu wa manispaa na hali ya uchumi.

    ReplyDelete
  12. NAUNGANA NA MDAU HAPO JUU, KWA KWELI KATIKA LIST YA MABANDIKO YAKO AMBAYO HUWA UNAWEKA KILA SIKU. LEO UMENENA. UMENIGUSA HASHWA.. HAYA MAMBO TUNAFANYA KIENYEJI KAMA NCHI HAINA WENYEWE HUWA YANANICHANGANYA SANA, HAYO MAGOROFA MBALI NA KUJENGWA BILA MPANGO JARIBU KUULIZIA WAMILIKI WAMATUMBI WA ASILI NI WANGAPI..??? UTAKUTA 1 IN 100 WENGINE WOOTE NI WAJOMBA WA FISADI R.A.

    ReplyDelete
  13. Msaada tutani. Hizi picha zinaonyesha "msitu wa simenti" au "mwitu wa zege"?

    ReplyDelete
  14. Michuzi achia kushikilia maoni yangu. natuma sana lakini unaniminyia. Usipoiweka hii hutaniona tena. Swala sio maghorofa ya kariakoo tu bali uchafu ni mwingi, mbele ya maduka mifereji ya maji machafu haifanyiwi kazi. kwani hao watu wa jiji wanavyokusanya kodi zetu za nini?

    ReplyDelete
  15. WE ANONY 11:12AM MARCH 12. WE NDO ZUMBUKUKU ULIMWENGU UKO HUKU.UJUI DUNIA UNAYOISHI IKOJE POLE SANA . NENDA UGANDA MJINI KOTE NI WAGANDA WAZAWA NDO WANAMILIKI BIASHARA .
    NYIE WATANZANIA MTAISHIA KUWA MAYAYA NA MABOY WA KUTUMWA NA WACHINA.
    UNASEMA TANZANIA LEO TUWE NA MIJI YA KICHINA KAMA LONDON AU NEW YORK. HAO WACHINA NA WAHINDI WA MAREKANI NA LONDON WAMEDHIBITIWA NA WANAZITUMIKIA HIZO NCHI NA WANALIPA KODI NA UKIANGALIA MAISHAYAO NI WATU WA DARAJA LA CHINI UKILINGANISHA NA WAMAREKANI AU WAINGEREZA NA WANALIPA KODI.

    KWATANZANIA NI TOFAUTI KABISA HAO WACHINA NA WAHINDI NDO WENYE KAULI NA SISI WATANZANIA NDO MAKULI WAO HAWANA MAPENZI NA NCHI BALI KUINYONYA NI MAHARAMIA KABISA KAZI ZA KUFANAYA WAMACHINGA NDO WANAZICHUKUWA WAO.
    TANZANIA HAIJAENDELEA KIASI HICHO NA HAKUNA UDHIBITI HAO NI MAFISADI WAKUBWA WACHINA WQAHINDI WANATUTOSHA WACHINA WA NINI.
    SINA FITINA NA HAWA WAGENI MKIENDA kwao mtakaribishwa????
    WATANZANIA AMKENI WAHINDI INAELEWEKA WANA HISTORIA NDEFU TANZANIA HAO WACHINA WANAKUJA KUHUJUMU TU NCHI YAAANI HAKUNA USALAMA KABISAAAAAAA NGOJENI WASHIKE MIZIZI MUONE MTAJAMBISHWA NA KUPIGWA MIJEREDI WA MBAVU MKIWA KWENU. AMAKENI AMKENI AMKENI.

    MICHUZI NAOMBA UTOE TENA MJADALA HUU WA UHALALI WA HAO WACHINA WALIOVAMIA DAR HILO NI TATIZO KUBWA SAANA ZAIDI YA HIYO MISITU YA ZEGE NA MIUNDOMBINU.

    ReplyDelete
  16. Hili ni jambo ambalo limekuwa likinishtua na kunishangaza tangu miaka kumi iliyopita! Mabadiliko ya Kariakoo kuachiwa watu kujenga bila kujali parking lots, bustani za kupumzikia, wala vyoo, sikuona kama ni maendeleo ya karne ya 21 hata kidogo! Swala la machinga wananchi kuchukuliwa nafasi zao za kazi ni la aibu nakusikitisha sana. Serikali inabidi iingilie kati bei za kupangisha wafanya biashara wadogo wadogo Kariakoo ama sivyo hata mikopo midogo tunayopata toka serikalini tutashindwa kuilipa kwani kila baada ya miezi mitatu tunapandishiwa bei. Ukilalamika unaambiwa wapo wengi wenye uwezo na wanataka eneo hili. HII KWELI NI HAKI, NI LINI SISI TUTAJIKOMBOA HATA KAMA TUNA NIA??!! MH. KIKWETE TAFADHALI, HILI NI SWALA LA KUCHUKULIWA HATUA ZA HARAKA SANA!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...