Watangazaji mahiri wa Clouds FM 88.4 kupitia kipindi chao cha Leo Tena kinachorushwa hewani kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 7 kamili mchana, Dina Marios (kulia) Gea Habib a.k.a mama wa Heka heka. Habari ni kwamba Dina Marios naye ameanzisha libeneke lake linaloenda kwa jina la dinamarios.blogspot.com
--------------------------------------------
HONGERA NA CHANGAMOTO YA LIBENEKE
Hongera sana Dina Marios kwa hatua hiyo, na karibu katika libeneke la mawasiliano ya njia hii. Napenda kuchukua fursa hii kutoa changamoto kwa wadau kwamba kila aliye na nia ya kuanzisha libeneke na afanye hivyo kwani wigo ni mpana na wanalibeneke tuliopo katika gemu katu hatutoshelezi mahitaji. hivyo usikonde wala nini Dina, karibu sana katika libeneke.
Naomba nichukue nafasi hii kulitumbua jipu lililonikwama moyoni kwa muda mrefu sana, kuhusiana na jinsi tasnia ya TEKNOHAMA inavyochuliwa Bongo.
Rai yangu katika hili ni hii dhana pofu iliyotanda kila mahali kwamba fani ya globu si chanzo rasmi cha habari na kwamba vyombo vlivyozoeleka kama vile magazeti, TV na Redio ndivyo pekee vilivyo rasmi kama ambavyo baadhi ya wadau wanavyofikiria. Inauma na kukatisha tamaa sana pale unapoona mtu anabeza fani hii kwa kuhoji kwa nini i.e. mtu anatuma salamu ama hata kutafuta mchumba kupitia humu. kuna wengine wamehoji eti kwa nini sehemu nyeti kama Ikulu inatumia globu kuwasiliana na umma.
Wengine ukiwatajia neno globu ama blogu wanatoa macho utadhani umetukana. Hivi Wabongo mbona hatueleweki. Wakati wenzetu wanapiga hatua kumi mbele sie na kujifanya kujua kwetu kwa kila jambo tuna mark-time wakati tukija kupigwa bao tunalalamika.
Tatizo ni nini hasa katika hilo? Je hatujui kwama globu ama blogu ndizo zenyewe siku hizi? Na hapo sijataja vitu kama twitter, aina mpya ya mawasiliano ya chap-chap ambayo watu kama Rais Obama wa Marekani hutumia. Vile vile kuna podcast ambayo nayo iko juu kwa wenzetu
Hebu wadau na tukae chini na tujiulize:
1. Kwani tatizo liko wapi weng tunakuwa wazito kukubali kwamba globu ni chombo rasmi cha mawasiliano na anayekibeza anajibeza mwenyewe? Kwani hapa kikubwa kinachotakiwa ni aina ya chombo kinachofikisha ujumbe ama ujumbe unafika fikaje kwa wahusika tena kwa haraka na urahisi pengine kuliko hivyo vyombo vinvyojulikana ama vinavyonekana kama ni rasmi zaidi?
2. Ni lini Wabongo tutaamka na kuanza kuheshimu njia za kupashana habari kwa njia ya globu ama twitter ama podcast kama wanavyofanya wenzetu? Ona watangazaji na waandishi wote wa mashirika kama ya CNN, BBC, SKYNEWS, AL Jazeera n.k pamoja na magazeti makuu yote ulimwenguni wana globu zao ambazo wasomaji wake wanaziheshimu ile mbaya. Hata kwa watani wa jadi Kenya na Uganda waandishi wao wamechangamkia tenda hii na kila mtu ana globu yake. Sie wabongo tatizo letu nini hasa?
3. Vichekesho ni kwamba utakuta hapa Bongo ni Wapiganaji (waandishi wa habari) wachache mno ambao wameona mbali na kwenda na wakati kwa kuanzisha libeneke. Wengi wa hao wanaoendeleza libeneke ni akina sie wa 'Enzi za Mwalimu', wakati wale waandishi wa 'Kizazi Kipya' bado wana mawazo ya kutoa habari siku moja baada ya tukio kutokea na sio saa hiyo hiyo kama wanvyofanay wenzetu. Je, tatizo liko wapi?
4. Vichekesho ni kwenye wizara na idara za serikali pamoja na mashirika ya umma na binafsi. Huko asilimia kubwa TEKNOHAMA si kipaumbele katika utendaji wao. Tovuti aidh hawana na kama wanayo hakuna anayekumbuka kuiweka hai (up-date). Yaani JK anatia huruma kwa kweli, hapo utakuta wanangoja atamke kwamba jamani eeee twende na wakati tukumbatie TEKNOHAMA ndipo wazinduke. Tatizo liko wapi???
yapo mengi ya kulonga ila naomba kwa leo niishie hapa. Lakini huu ndio mwanzo wa kutaka kuamsha wadau na wabongo kwa jumla kwamba tuache ujuaji, tukubali kwamba tumechelewa kuamka na tuikumbatie TEKNOHAMA kwani ndiko dunia ielekeako. Tukibeza haya na mengi mengine tusije lalamika tukija kupiwa bao na watu kama watni wa jadi ambao wameshaanza kutuacha.
Wadau nafungua mjadala, karibu utoe dukuduku lako na pia ni vyema ukatoa na mawazo mbadala kwamba kifanyike nini ili mambo yawe mswano.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2009

    Kikwete hawezi kuwaambia waende na wakati kwa kutumia Teknohama wakati anajua Watanzania ambao hawajui mlo wa kesho utatoka wapi hawana access ya mtandao. hivi mkuu wa wilaya unajifanya hujui kwamba watanzania ni maskini kiasi kwamba unataka kuwafananisha na wamarekani? kwenye blog yako kwenyewe watu wanaokusoma asilimia tisini wako nje ya nchi ni asilimia kumi tu ya walioko Tnzania ndio ambao wanafford internent. be fair on this please

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2009

    Jamii forums leo haionekani kuna nini? Kuna mdau mwenye taarifa?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2009

    TUMEKUSIKIA MICHUZI NA WEWE KAMA KWELI UNATAKA WATU WAANZE KUHESHIMU BLOGU KAMA CHOMBO KAMILI CHA HABARI ACHA KUBAGUA HABARI.WEKA HABARI ZOTE BILA UOGA WOWOTE.HAO WAANDISHI WA HABARI WA NCHI ULIZOTAJA KINACHOWAFANYA WASOMAJI WAO WAVUTIWE NI KUTO KUWA NA UBAGUZI WA HABARI.
    SIKU UTAKUWA UNAWEZA HABARI BILA UBAGUZI NA KUWAACHA WATU WATOE MAONI YAO BILA KUWABAGUA NDIO UTAONA MITAANI WATU WANAVYO ZUNGUMZIA BLOGU.
    NAPIA SIKU MOJA NA SISI TUTAFIKA MANAKE WENZETU WAKO MBELE KWENYE MTANDAO KILA KONA NA WATU WANAUWEZO.KWA NYUMBANI SIO WOTE WENYE UWEZO KUWA KWENYE MTANDAO 24/7.
    mdau mzawa

    ReplyDelete
  4. Kaka Michuzi umelonga haswa. Usijali mradi wewe unayo blog hii sie waelewa tuko nawe mia kwa mia.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2009

    Nashukuru kwa maelezo yako hapo,lakizni nazani pia hujaangalia ni watanzania wangapi wanamawasiliano ya internet na piawanamiliki computer.Kwahiyo naona tatizo sio kuona mbele tatizo ni umiliki wa hico kitendea kazi maana hapa kwetu kinauzwa bei ya juu sana

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2009

    Wanajitahidi kwa kweli

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2009

    Safi sana kaka Michuzi, waamshe wadau na wabongo wote kwa ujumla. Hongera kwa kazi nzuri, sisi tunakushukuru kwani blogu yako kwani imekuwa kituo muhimu cha habari hususani za huko nyumbani.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2009

    Tz can teach Ugandans Swahili
    Friday, 5th June, 2009 E-mail article Print article

    BY Moses Mapesa

    LAST year I made a case for teaching Swahili as a compulsory subject in our schools and indeed all institutions of learning to ensure that Ugandans effectively use it as a national language.

    I did point out that under the East African Community, the Treaty does provide for Swahili as an official language for East Africa and underscored its importance in trade beyond the East African region and its wide use in America, Europe and Asia particularly in the media.

    Recently, I read in the press that the Ministry of Education had dropped Swahili from the compulsory subjects. I also read a number of articles in support of teaching and use of Swahili which was a good encouragement.

    Many teachers, students and ordinary citizens came up in support of Swahili and in fact criticised the Ministry of Education for the decision. In its defence, the ministry argued that there are not enough qualified Swahili teachers. This is what should be addressed.

    While attending an East African Community meeting of experts in Moshi, Tanzania last week, it struck me and my Ugandan colleagues that it is very difficult to differentiate Tanzanians by tribe (or ethnic language) courtesy of Swahili. Tanzanians are Tanzanians, period—real patriotism.

    Later we got a problem at the meeting when our colleagues from Burundi could not effectively communicate in English and the rest of us (Kenya, Tanzania and Uganda) could not speak French! I later leant that at an earlier meeting in Kigali it was even worse. However, we could all at least understand Swahili and express ourselves reasonably. Note that most Ugandans have never formally attended Swahili lessons.

    This reminded me of two similar incidents. One in Paris when African states representatives wanted to consult privately and we needed English and French interpretation that had not been provided for.

    We tried out Swahili and it worked. The second was in Goma, DR Congo, when our respective ministers of Rwanda, Uganda and DR Congo could not communicate in either French or English and we had no interpreter. Again we tried Swahili and I actually assumed the role of interpreter but in Swahili for my Uganda minister, who in any case understood over 60% of Swahili as opposed to less than 1% of French.

    Much earlier in Brazil at a Global Conference, African states consultations were a nightmare when we had Arabic, French and English speakers. Translation (interpretation) at international meetings is very expensive.

    In a number of our technical meetings with DR Congo and Rwanda we have had to resort to communicating in Swahili instead of struggling with either English or French, we have exchanged e-mails in Swahili.

    So now that we have the East African Community we must cooperate in promoting teaching and use of Swahili. Uganda could request the government of the United Republic of Tanzania to avail Swahili tutors and lecturers to all our teacher training institutions and other tertiary institutions in the departments of languages and within one year we would have many Swahili teachers for all our schools.

    Uganda can also request Tanzania for Swahili lecturers to help those at the National Leadership Institute, Kyankwanzi and we undertake a Swahili crush programme for all government officials as part of the ‘Patriotism and Prosperity for All’ lessons.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2009

    Umeongea mambo balozi wa naniii, ila kuna kitu umesahau. Kama utakubaliana nami ni kuwa sie kwa namna fulani bado tuko nyuma ndio maana hata ukifungua website ya serikali au bunge utakayokutana nayo nadhani ni yale ambayo yamepitwa na wakati; na wakati huo huo idara zetu hazijaweza bado kuwa wanaweka mambo yao kwenye websites, mfano fikiria mtu unatafuta inventory ya tourist hotels za Tanzania, uki-google utakayoyaona mhh naishia hapo!! Sasa huu ni mwanzo na kama mwanzo tuutumie na kujaribu kusukumana ili tuende na tusifikiri itafanyika kwa siku moja. Bado tuko nyuma Michuzi, na nakuhakikishia jaribu kutafiti na utaona ni Watanzania wangapi ambao walau wanasoma hata blogs tu

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 07, 2009

    Naona hapo Dinna katoa point kubwa, ila kuna kitu kingine cha ziada, ukiangalia Bei za net hapo Bongo bado bado ziko juu kiasi, ingawa wanajaribukupunguza. ila ni kikwazo kwa watumiaji wadogo wadogo wa kawaida.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 07, 2009

    sio siri Dada Dinna kwenye Blog yako inaonyesha ni wewe ni mtaalamu uliebobea.
    point hizo zako nimesoma nikajaribu naona mambo yanakwenda vizuri kuliko kawaida mpaka napewa marks kubwa.
    ila naona niishie hapa manake michuzi anaweza kutia kapuni comment.

    ReplyDelete
  12. kaka nashukuru sana kutufumbua macho ila najua kuna ccm,chadema,cuf nakadhalika lakini kwa suala la maendeleo tuzike tofauti zetu tuchape kazi ni hayo kaka.

    ReplyDelete
  13. "A blog is a type of website, usually maintained by an individual with regular entries of commentary, descriptions of events, or other material such as graphics or video.

    Many blogs provide commentary or news on a particular subject; others function as more personal online diaries."

    Quoting from Wikipedia.

    Sijui watu wengine wanakuwa na chuki binafsi or something else ila kama blogger ambaye ni mchanga kabisa, post yoyote tu ile inakubalika inategemea blog yako inahusu nini. Ila wapo watu tu watakushusha na kile unachokifanya.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 07, 2009

    hi,mr michuzi kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kwa heshima kubwa sana uliyotupatia hasa watanzania wote kwa ujumla,mie bwana issa naishi nje ya nchi,chombo cha kwanza kunipatia news ni blog hii ya jamii zamani nilikuwa nahangaika sana kupata news kutoka back home,nilikuwa najaribu kucheck magazeti yote ya bongo,vibaya zaidi habari zilikuwa zinatake kama siku mbili au tatu,kupata habari mpya.kwa hivyo basi maada yangu ni kwamba hao watu wanaokubeza,achana nao wewe songa mbele.usiyumbishwe na watu wachache.so far so good unajitahidi sana,mfano wengi wa watu ambao tuko nje ya nchi.chombo chako kinatupatia,very,very breaking news then even hizo za mabwana wakubwa.marlesa mussa wa 22.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 08, 2009

    asante sana mdau kwakuhamasisha silo kwakweli bongo inatia huruma saana.kunawasomi wanamaliza vyuo vikuu saizi bongo hana habari kabisa na mambo ya technologia hata kufungua email adress na kuandika email nakutuma hawezi ukimwambia anashangaaa ni nini hicho.
    mi naona tatizo kubwa ni kwamba internate servisee kwa tz bado iko chini sana kwanza iko low pili ni expensive so watu wanakwenda net kwa shuhuli maalum saana.tofauti na nchi za wenzetu net iko speed sana na ni cheep.
    lmda huduma hii ingefanywa cheep zaidi watu wengi wangeitumia,
    naumaskini wetu wa bongo sasa mtu anafikiria ni chakula atanunua au ni internate anatakwenda?
    kwanza mashuleni kungekua na Computer lab na ziwe na internate na vyuoni vilevile nadhani inaweza kusaidia

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 08, 2009

    KWA TANZANIA BADO NI GAZETI NA REDIO.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 08, 2009

    Nimekua nikisoma maoni mbalimbali ya watanzania kwa kipingi cha wiki sasa. Kikubwa nilichogundua ni kua asilimia 90 ya watoa maoni, wamejaa wivu kuona maendeleo ya watu, wengi narrow minded, wengi hawana international/national exposure,na kikubwa pia ni kua watoa maoni wengi humu wanadharauliana watanzania kwa watanzania.badala ya kuchangia wazo zuri la mtu, wanakua negative nalo.Blog hii ni njia nzuri ya kufanya "brain storming".badala yake wengi ni wivu,majungu na kama ulivyosema,wanazidi kujirudisha nyuma.wenzetu wanakimbia mbele,wao wanakimbilia nyuma. Inasikitisha sana. Nilisikitishwa sana na maoni ya watu kuhusu blog mpya ya mzee mmoja(simkumbuki jina)ambayo ulionyesha picha wakiwa wanaizundua. 98% ya maoni,walikua against nayo,wivu,hawataki maendeleo ya watu wengine,wanaona watafaida,nk. Inabidi hawa watu wafumbue macho,waamke na kama wanataka kuwa against na kitu,basi na wao watoe kilicho bora zaidi ya hao wanaowakandia.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 08, 2009

    Naomba kuuliza wewendiye dina wa DINAHICIOUS BLOG, au ni majina kufanana,lakini kama mtofautilakini yaonekana wote mnashabihiana ki fani. Hongereni sana

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 08, 2009

    Dina Marrios wa Clouds FM ni tofauti na Dinahicious wa Bongo Radio. Mmoja yuko Bongo na mwingine yuko UK, lakini wote wako kwenye fani ya kutuhabarisha kwa sauti nzuri.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 25, 2009

    Dinah wa bongo radio sio jimama ni mdogomdogo fulani hivi naukitaka kumuona nenda facebuk pia sauti zao hazifanani hata kidogo yule wa bongoradio ni moto wa kuotea mbali unaweza kubaki redioni siku nzima.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...