kaka Michu!
Nilibahatika kuinasa hii. Hii ilikuwa katika 'World Summit on Art and Culture' Mkutano huo mkubwa ni kama World Cup, haujawahi kufanyika Afrika hii ni mara ya Kwanza na umefanyika Johanesburg mwezi huu September.Katika pita pita zangu nikakutana na neno KARIBU mwanzoni kabisa mwa bango hili.

kwa kweli Kiswahili kiko Juuuuuuuuuu!!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Neno ulilokutana nalo ni karibuni wala si KARIBU. Usitake kutudanganya wakati tunaona hivi hivi....

    ReplyDelete
  2. Mtowa habari Umetwambia kwa kweli Kiswahili kiko (kipo) juuuuuuuuu!!! sasa na wa swahili wenywe vipi ? kiko =ni ile paipu ya kuzutia tumbaku.

    Ukiviona vinaelea ujuwe vimeudwa.

    ReplyDelete
  3. Si unajua watanzania tulivyo wahongo kama JK vile.

    ReplyDelete
  4. Dam KUZUTIA tumbaku? iyo kali.

    ReplyDelete
  5. Hapa kadhi(kazi?)ipo (iko???) Mara 'kuzutia', mara 'wahongo'! Mimi nipo (niko?) hapa navizia ole wake wao Walugha-lugha!

    ReplyDelete
  6. Kwa mwenye akili nzuri kumcheka Kanumba na akina Janeth mwa makosa madogo ya lugha ni akili ya utumwa
    Kiswahili kinatukuzwa sana

    Asilimia 60 ya vyuo vya USA vinatumia neno karibu kuvutia wageni specially Africa.

    Kumbukeni kwamba lugha tunayo-kiswahili. English tunajilazimisha ili tuendane na dunia inayokimbia.

    Na siyejua kiingeleza si mjinga kwakuwa si lugha yetu ya asili..

    Wanaocheka watu wanaogonga kiingeleza wanalipa visasi vya wao kuchkwa na wazungu kwakuwa hata ujue vp english accent itakuua na mamtoni watakucheka na kuonesha kwamba umetoka polini.

    Na ni ukweli uliowazi kwamba 995 ya tulionje tunachekwa english yetu na tusijifanye tunaijua kuliko akina kanumba

    I love swahili na kimsingi tunayo lugha na tujivunie nayo japo bado kutokana na kukimbizwa kiuchumi tuipige english ya ugoko tufike.

    Tusichekane wala kubaguana

    ReplyDelete
  7. Ya ni kweli ndugu.
    tatizo ni wanaojifanya kujua kiingeleza wanaishia ku-wish kwamba nafasi kubwa kama za akina kanumba wangepewa wao.
    Wakae wakijua kuwa bahati na utaalam ni vitu tofauti
    Jua english yako ila kanumba yuko mjengoni na analipwa na amekuwa star wa Africa
    wat abt that?
    Kiswahili oyee
    Dont be offended kwa kutojua english
    Na wenye akili za kitumwa msimzomee mtu aliyekosea kiingeleza.
    Msilipize mnavyochekwa na wanugu

    ReplyDelete
  8. Ingekuwa bongo hata hiyo "karibuni" huioni!!! Si mnajua tena tunakwenda na wakati! Siku hizi hadi vibao vinavyoonyesha mitaa jijini Dar vile vya "MT.MOROGORO" vimengolewa na kubandikwa vipya "MOROGORO ROAD" ili tusije tukachekwa na 'wenzetu'!!!!.

    ReplyDelete
  9. mdau wa 5:53:00 sio kiingeleza ni KIINGEREZA kama ulienda st kayumba lazima aka msingi uliimba huu wimbo darasa la kwanza hii ndio RRRRRRR ipo kama _ _ _ RRRRRRR

    ReplyDelete
  10. Kiswahili kipo juu lakini sisi wenyewe hatutaki kiwe juu. Angalia viongozi wetu wanapokwenda majuu, juhudi gani wanazozifanya kukiweka katika chati ya dunia.
    Hebu viongozi siku wakifika huko wajifanye hawajui Kiingereza, ili hotuba zao zitafutiwe mkalimani, kama Kiswahili hakitawekwa kwenye lugha za kimataifa.
    Mhh, nani atafanya hivyo wakati wote ni wasomi. Msomi ujue Kiingereza bwana!

    ReplyDelete
  11. Miram3 u got the point right there hata kama haiwezi kubeba uzito uliotakiwa
    Ni jitihada za mwalimu kukifanya kiswahili iwe lugha kubwa duniani
    Actuali US wanaamini kiswahili ni lugha ya afrika na uislamu ni dini ya waafrica.

    Wamarekani weusi wanakizimia sana. Am teaching 2 of them kiswahili na wanakipenda sana. Wanaamini Ona mfano wa majina ya 2pac-Jina lake ni 2pac Omari Shukuru. Omari-Omar na Shakur ni Shukuru. Angalia maana ya Shakur kwa black Americans ni thanks (Shukuru)-Shu ina sound kama "sha" na kuru imekuwa kur kwa pronounciation zao
    Wanapenda sana Kiswahili
    bahati mbaya sisi wenyewe tunapenda kiingeleza na usipojua kiingeleza unaonekana ni krimino ama kanumba-utumwa wa akili.

    ReplyDelete
  12. NDIO MAANA YAKE KISAWAHILI KIPO JUU ZAIDI NA KINAPENDWA MNO NA WAGENI KWA KUWA WAO NI WAJANJA ILA KINA CHUKIWA NA WENYEJI WALE WARUGARUGA WALIO KUWA BADO HAWAJAFUNUKA NA KUJUA NINI KINAENDELEA KWA CHUKI ZAO BINAFSI.

    UKIONA MTU ANAKICHUKIA KISWAHILI MTIZAME MARA MBILI MBILI UTAMWONA TU KUWA HAYUPO SAWA AMA ANAINFERIORITY COMPLEX HATAKI NAYE AONEKANE HAYUPO!!SIUNAJUA TENA JEMBE NI JEMBE NA WATUMWA WA KIFIKRA?

    ReplyDelete
  13. KISWAHILI JUU JUU JUU ZAIDI

    ReplyDelete
  14. Tatizo wabongo, mazuri ya kwetu hatuyaoni, ni kujidahrau tu kwa kila kitu. tunayo pia mazuri ya kujivunia. Tuwe na mtizamo chanya kwa yale mazuri. Bongo Oyeeeh!!! Nitafia hapa hapa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...